Tuweke wazi, uwezo wa akili ni mmoja tu hakuna tofauti

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,911
Reaction score
28,469
Nilishawahi kuona na kusikia kwamba huyu ni "jiniazi" sijui hasomagi! Mara kameza madesa yote!

Kipindi tuko mashuleni tuliamini ni kweli na huenda mpaka sasa baadhi au wengi mnaamini hivyo lakini ukweli ni kwamba
√binadamu wote wana akili sawa!

Tatizo ni jinsi binadamu tunavyozitumia akili zetu, wengine wataitumia kuvumbua vitu usiku na mchana, na wengine wataitumia kuwaza mwajuma msambwanda atampa lini au mudi mpemba atampata lini. Sasa umeona tofauti

Binadamu anatumia asilimia 2% tu kufikiri nje ya Box, hizo zilizobaki zinaendesha mwili, wakati huo kuna wengine wanajitesa na kutumia mpaka asilimia 4% kufikiria na hata kusoma mashuleni. Wengi wao walianza tangu wakiwa wadogo kwa wazazi wao,
√anafundishwa yeye ni nani kabla hata hajaanza shule (wahindi huwa wanafanya Sana)

√ anafundishwa pia kuhusu mahitaji yake kimwili na kiakili. Kwamba Labda vitu anavyopewa na wazazi wake vimetafutwa, tena kwa akili na nguvu, hivyo nae ajiandae ku Copy Style ya baba yake. Sasa baba na mama unakuta wanatukanana na kuitana vibamia unategemea nini kwa mtoto?

Pia kama unataka mwanao awe na uwezo darasani peleka shule za gharama kama pesa ipo! Kwanini? Nitakupa mfano mmoja.

John alipoanza shule ya awali iliyopo mtaani kwao.mwalimu wao aliwafundisha kusoma kwa sauti kubwa ili waweze kukariri, mwalimu aliamini wasiposoma kwa sauti watoto hawatoelewa. Hivyo hali hii ikapelekea john awe anasoma kwa sauti kubwa au ya chini ndio aweze kuelewa! Sasa amekuwa mtu mzima, ofisini kwake hata meseji ya simu lazima asome kwa sauti kubwa. Hivyo john alikaririshwa kuelewa kitu. Hii ilimfanya atumie nguvu kusoma kuliko mfano.

Junior alianza kuletewa picha na michoro na baba yake ili awe anapaka rangi picha hizo,alikuwa bado hajapelekwa shule (hajaanza)
Hivyo junior alizoeshwa kushika kalamu na penseli tangu hajaanza shule, taratibu alijikuta anaanza kujifunza silabi zilizokuwa kwenye picha hizo A, B, C nk.

Shuleni kwao mwalimu wao aliwafundisha kwanza kulipenda somo kiasi kwamba watoto walipenda kuja shuleni kila siku. Darasa lilikuwa na kelele pale watoto wanapoimba nyimbo za michezo basi na si vinginevyo. Automatic wakajikuta wanapenda masomo na kuyaelewa na sio kukariri. Wala hawakuwa wanachapwa sembuse kufinywa. Hii ilipelekea junior awe mbunifu zaidi na masomo sababu aliyapenda. Na wala hakutumia nguvu kuyasoma.

Hivyo akili zetu zinafanana shida ni jinsi zilivyozoeshwa toka udogoni. Wapo waliosoma kwa kukariri ni asilimia kubwa sana. Hutakiwi kukariri kitu kipende kwanza automatic kitakaa akilini. Hebu tuone mfano.

Mbona umekariri nyimbo mpya kwa siku moja tu? Na wala hukufanya juhudi yoyote kukariri?

Jibu ni kuwa uliipenda nyimbo kwanza.

Pia akili ni rahisi kusahau kitu kwa masaa manane mbele kuliko mwaka mmoja. Ukifanikiwa kuelewa kitu ndani ya masaa nane hutoweza kusahau maisha yako yote.

"panchito baba paula"
 
Hapa umeongelea sana vaguely na sio katika point of view ya science. Haujafanya research/study yoyote bali umeweka opinions zako tu (You are not objective).

Kihalisia ni kuwa binadamu achilia mbali na kuwa na size tofauti za ubongo (brain size) pia tunatofautiana thinking capabilities na intelligence.

All human beings are born free and equal in dignity and rights only.

Kwenye mambo mengine kila mtu ana tofauti na mwingine labda tu ungesema wapo watu ambao wanashindwa ku realize potential zao kwa uzembe.
 
Ina maana wataka uondoe uhalali wa wale great thinkers wa hapa jamii forum??
 
Hakuna cha great thinkers mkuu hapa
siri ni kutafuta maarifa yaliyopo maandishini na kuyaweka kichwani wamefanikiwa na wapo wameshindwa
 
Hapa umeongelea sana vaguely na sio katika point of view ya science. Haujafanya research/study yoyote bali umeweka opinions zako tu (You are not objective).

Kihalisia ni kuwa binadamu achilia mbali na kuwa na size tofauti za ubongo (brain size) pia tunatofautiana thinking capabilities na intelligence.

All human beings are born free and equal in dignity and rights only.

Kwenye mambo mengine kila mtu ana tofauti na mwingine labda tu ungesema wapo watu ambao wanashindwa ku realize potential zao kwa uzembe.
Rahisi tu nawe naomba ushahidi mkuu
La sivyo nawe pia umetoa opinion kama mimi tu
 
Kwa elimu yetu nashindwa kuelewa wale tunaojua ni vipanga ni kweli vipanga au wana biggest hippocampus (big memory)...
 
Lowell Thomas kwa kutumia kitabu chake kiichoitwa How to win friends and influence peoples ambapo alimnukuu vibaya mwanasaikolojia William James ambapo aliwahi kusema “average person specifically develops only 10% percent of his/her latent ability” ambapo kiuhalisia James alikua amezungumzia “our latent mental energy” lakini pia inaonekana kua nadharia hii pia ilichagizwa pia kuenea na mtalamu wa ubongo (Neurosurgeon) Wilder Penfield ambapo aligundua silent cotex mnamo mwaka 1930’s ambapo alisema kua silent cotex haina kazi kwenye ubongo mpaka ishituliwe na na umeme lakini kiuhalisia hiyo sehemu siku hizi imegundulika kua inafanya kazi.

Wanasayansi wengi wanasema kua nadharia hii ni uongo! Bnaadamu wote tunatumi 100% ya ubongo wetu, vifaa vya kisasa kama brain scanning vinaonyesha ubongo wetu unafanya kazimuda wote kwa kupitia viungo vyote hata tukiwa tumepumzika zipo tafiti nyingi zimefanywa zinaonyesha kua binaadamu tunatumia 100% ya ubongo wetu.
vinvi wa kwa mpalangee hapa nimekubali
that's what i said
Akili zetu wote zinafanya kazi sawa!
 
Kwa elimu yetu nashindwa kuelewa wale tunaojua ni vipanga ni kweli vipanga au wana biggest hippocampus (big memory)...
Wamekipenda kwanza wanachokisoma
hakiwezi kutoka kichwani.

Umeshawahi kitu unachokipenda?
 
Yale maphysics wanayapenda? Thubutuuu lol, ni kumeza kwa kwenda mbele( cramming)
Kuhusu physics Mara nyingi kuanzia advance kuna vijana wanakariri kishenzi
ila unakuta o level physics aliipenda
 
Back
Top Bottom