Pre GE2025 Tuwekee kero za mtaani kwako zinazokufanya uichukie CCM na usiipe kura chaguzi zinazokuja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama mada inavyojieleza hapo juu natamani tuondokane na siasa za mihemko tuje kwenye siasa za hoja. Kuna wanaJF wanatamani kuamua nani wamchague na nani kwa sababu zipi. Nataka tusaidiane kupata sababu za kuacha watu.

Kwa mfano mimi nakaa Goba kwenye huu mtaa naichukia sana CCM kwa kuacha kutatua kero ya maji kwa makusudi kabisa.

Juzi kati hapa kaja Aweso yametoka siku mbili halafu yamepotea. Kwa hali hii lazima niwaadhibu
Moja kwa moja
1. Rushwa na ufisadi wa viongozi bila kuchukuliwa hatua zozote
2. Kupokwa viwanja au kuvunjiwa nyumba wananchi huko Mapinga, Bunju, Mabwepande, Mbopo kwa vitisho na dhuluma za wazi
3. Barabara mbovu huko Makabe, Msakuzi, Mpiji Magoe, Msumi, Mbopo, Bunju,
4. Gharama za umeme juu
5. Gharama za kuunganisha umeme juu
6. Huduma za afya duni na wahudumu hawana utendaji wenye 'hospitality' kwa wagonjwa
7. Huduma duni ya maji
8. Viongozi kutosikiliza kero za wananchi na kutafuta utatuzi kwa muda na wananchi wakaona jitihada zimefanyika
9. Michango mingi kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi sekondari bila sababu za msingi zinazohalalisha licha ya kuambiwa elimu isiyo na malipo
10. Viongozi wasio wajibika kwa wapiga kura wao, wakijineemesha na posho kutokana na kodi za wananchi
11. Maadili mabovu kutamalaki bila kukemewa na viongozi kwa kisingizio eti ni enzi za utandawazi na demokrasia
12. Viongozi kufanya makosa ya kimaadili na jinai bila kuchukuliwa hatua stahiki kwa mjibu wa sheria wakati huo huo mwananchi wa kawaida akitenda kosa kama hilo anashitakiwa na kuhukumiwa kwa adhabu kali bila kujali chochote.
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu natamani tuondokane na siasa za mihemko tuje kwenye siasa za hoja. Kuna wanaJF wanatamani kuamua nani wamchague na nani kwa sababu zipi. Nataka tusaidiane kupata sababu za kuacha watu.

Kwa mfano mimi nakaa Goba kwenye huu mtaa naichukia sana CCM kwa kuacha kutatua kero ya maji kwa makusudi kabisa.

Juzi kati hapa kaja Aweso yametoka siku mbili halafu yamepotea. Kwa hali hii lazima niwaadhibu
Hizo zitakuwa mambo ya kuwa danganyia wapiga kura kwa uongo ule ninaoufahamu au ni mzalendo mwenye nia ya kujua kero na kujitosa uchaguzini.Na iwapo umepanga kuwa mgombea na wakati huu ndio unatafuta kujua kero ni zipi mtaani kwa ama kwenye eneo unalolenga kuwa mgombea hautufai,ushauri kama unafikiri kupata nafasi ni kupata kula kwa urefu wa kamba sahau,maisha yalisha pinda tena kwa kasi ya 7G🫠
 
Kwani kama nia yangu ni kujua kero ni ili nigombee nafasi ipi sasa maana jf ipo nchi nzima
 
Juzi kati hapa kaja Aweso yametoka siku mbili halafu yamepotea. Kwa hali hii lazima niwaadhibu
Kwa hio hapo mwenye makosa ni nani Aweso, Mbunge wenu anaaeenda kugongwa Meza tu kule bungeni hasemi chochote kuwahusu Wananchi wa Jimbo lake, Diwani wenu anaetumbua tu hasemi chochote kwa watu wa Maji au ni nini Serikali ifanye ifukuze Wafanyakazi wote wa DAWASA ndio furaha yako?
 
Furaha yangu maji yapatikane muda wote na kwa kuwa hawa waliopo hilo limewashinda wanastahili adhabu
 
Back
Top Bottom