Kama mada inavyojieleza hapo juu natamani tuondokane na siasa za mihemko tuje kwenye siasa za hoja. Kuna wanaJF wanatamani kuamua nani wamchague na nani kwa sababu zipi. Nataka tusaidiane kupata sababu za kuacha watu.
Kwa mfano mimi nakaa Goba kwenye huu mtaa naichukia sana CCM kwa kuacha kutatua kero ya maji kwa makusudi kabisa.
Juzi kati hapa kaja Aweso yametoka siku mbili halafu yamepotea. Kwa hali hii lazima niwaadhibu
Moja kwa moja
1. Rushwa na ufisadi wa viongozi bila kuchukuliwa hatua zozote
2. Kupokwa viwanja au kuvunjiwa nyumba wananchi huko Mapinga, Bunju, Mabwepande, Mbopo kwa vitisho na dhuluma za wazi
3. Barabara mbovu huko Makabe, Msakuzi, Mpiji Magoe, Msumi, Mbopo, Bunju,
4. Gharama za umeme juu
5. Gharama za kuunganisha umeme juu
6. Huduma za afya duni na wahudumu hawana utendaji wenye 'hospitality' kwa wagonjwa
7. Huduma duni ya maji
8. Viongozi kutosikiliza kero za wananchi na kutafuta utatuzi kwa muda na wananchi wakaona jitihada zimefanyika
9. Michango mingi kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi sekondari bila sababu za msingi zinazohalalisha licha ya kuambiwa elimu isiyo na malipo
10. Viongozi wasio wajibika kwa wapiga kura wao, wakijineemesha na posho kutokana na kodi za wananchi
11. Maadili mabovu kutamalaki bila kukemewa na viongozi kwa kisingizio eti ni enzi za utandawazi na demokrasia
12. Viongozi kufanya makosa ya kimaadili na jinai bila kuchukuliwa hatua stahiki kwa mjibu wa sheria wakati huo huo mwananchi wa kawaida akitenda kosa kama hilo anashitakiwa na kuhukumiwa kwa adhabu kali bila kujali chochote.