Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Unaweza ukamkejeli kadri unavyojisikia kwamba alikuwa mtesaji, alikuwa mkabila alikuwa mkatili. Unaweza ukamsimanga kadri ya uwezo wa akili yako utakavyokuwezesha, hataweza kukujibu amelala usingizi wa milele na hataweza kuamka.
Amepumzika nyumbani kwake Chato, na siku alipokuwa njiani kuelekea huko, kina Mama walimtandikia kanga njiani na wakalia machozi halisi ya kutoka moyoni na sio yale ya usoni ya kutimiza wajibu. Ameacha ushahidi mwingi wa kazi yake, ambazo kwa kweli zilikuwa ni kazi zenye ugumu wake katika kuzianzisha.
Unaweza ukasema alijfufua shirika la ndege kwa kodi zetu, lakini kuweza kufanya hivyo mpaka shirika likasimama kulihitaji ujasiri mkubwa, siku zote kuwa na mtaji wa kuanzisha shirika la ndege katikati ya majukumu mengine mengi ya kitaifa kunautaka uwezo wa ziada wa kuiongozi ambao hayati JPM alikuwa nao.
Kuweza kusimama mpaka viwanja vya ndege vikaweza kujengwa karibu nchi nzima huku majukumu hayo akiwapa TANROAD badala ya mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania, ni sehemu ya maamuzi magumu yasiyoweza kueleweka miongoni mwa wengi wetu wenye mawazo ya kirasimu ya jumla jumla. Alikuwa na uthubutu na ukampatia umaarufu dunia nzima.
Kuweza kuanzisha ujenzi wa SGR kutoka hapa Dar mpaka mikoa ya kanda ya ziwa, ni zaidi ya maamuzi ya kishujaa, watangulizi wake wengi walipita wakishindwa kufanya maamuzi ambayo ni lazima yaumize sehemu ya uchumi wetu lakini katika kipindi cha muda mredu unaokuja yanakuwa na faida kwa Taifa zima. Mtaji wa kufanya hivyo kuupata haikuwa ni suala jepesi tu.
Kuwakoromea watu wa madini mpaka bosi wa BARRICK akafunga safari kutoka Canada mpaka Ikulu pale Magogoni, yalikuwa ni maamuzi ya kijasiri yaliyompaisha kimataifa, kwamba Tanzania imepata mtetezi wa kweli wa rasilimali zake, watangulizi wake walishindwa au hawakupenda kuonyesha msimamo unaojisimamia katika maswali yanayogusa hatima za mamilioni ya wanaowaongoza na ni hapa ndio JPM anapojitofautisha na kizazi cha viongozi wengi wa kiafrika.
Nimemuelewa Rais Samia kuuheshimu hadharani mchango mpana sana wa mtangulizi wake hayati JPM. Hakukuwa na sababu ya kujikweza na ameonyesha uungwana wa kiuongozi wa kuheshimu kazi nzito iliyofanywa na hayati japokuwa akiwa ni msaidizi wake mkuu walifanya mengi kwa pamoja.
Madaraja anayoyamalizia kuyajenga Rais SSH yalianzwa kujengwa na hayati, miradi inayoisha kwa sasa ni jasho la JPM pamoja na marais waliomtangulia. Ni suala la haki kabisa kwamba jema linalofanyika siku zote huwa na malipo mema hata kama anayelitenda anakuwa keshatangulia mbele za haki. Na hii ni maana ya uongozi kwa mapana yake.
Haufanyi haya yote kwa malengo binafsi, kiongozi mwenye maono na mwenye uthubutu huyafanya mengi yanayokuja kumtetea hata akiwa ndani ya kaburi kwa miaka na miaka. Kiongozi wa kweli hajali sana dhihaka za wanaompinga na maneno mengi ya kebehi na yenye kumkatisha tamaa, husimamia katika utimizaji wa maono yake.
Na siku zote watu huangalia maumivu ya leo hii na huja na riwaya ndefu za kuipinga mikakati inayotazama mbali. Wakati wa ujenzi wa barabara ya Ubungo mpaka KIbaha waliolia ni wengi lakini akashikilia mpaka imalizike. Leo imerahisisha sana uwezo wa kuifika Dar kutoka maeneo ya Chalinze.
Wakati daraja la Oysterbay mpaka Aga Khan linataka kuanza kujengwa, wadau walipiga sana kelele mitandaoni, leo hii saa za jioni wanaendesha kwa raha na amani wakiikwepa foleni ya daraja la Salendar, hayo ni maono ya JPM.
Wapo walioelewa maana ya maono ya JPM na wakawa na utayari wa kuipa muda mipango inayotazama mbali lakini wapo ambao wanatazama leo tu, hawakumuelewa kabisa hayati. Rais SSH kwenda kupokea tuzo huko Afrika Magharibi na akajinyenyekeza akisema kwamba watangulizi wake ndio wenye kustahili ni kauli ya sawia kabisa.
Ni ushahidi kuwa JPM aliipenda sana Tanzania na hakuthamini starehe zozote zinazokwenda pamoja na mamlaka ya urais aliyokuwa nayo, Hakuthamini anasa na matanuzi ya kuishi kama wafalme fulani katika dunia ambayo pumzi ni kama kiatu cha kuazima, muda wowote ule kinarudishwa kwa mmiliki. Nadhani hata ule umati uliomsindikiza mpaka uwanja wa Ndege akiwa ndani ya jeneza, uliitambua nafsi yake isiyo na makuu, isiyopenda utajiri wa haraka haraka kwa gharama ya mateso ya wengi.
Alikuwa na upungufu wake wa kushindwa kuweka mipaka ya maamuzi yake, akajikuta anaumiza hata wasio na kosa katika kutekeleza kile alichoamini kinaifaa Tanzania. Alikuwa na udhaifu wa kumtazama huyu ni kijana wa nyumbani anayeongea lugha moja na mimi ngoja nimsaidie kila iwezekanavyo japokuwa jamaa zake hao hakusita kuwafukuza kazi alipoona ufanisi wao hauendani na matarajio.
Tuzo aliyoipokea Rais SSH ughaibuni, nadhani ni ya kwanza kutoka katika mataifa yanayotanguliza mizania ya haki ya kupima ufanisi wa viongozi wa kiafrika. Kama JPM humu hatumuoni wa maana, wapo waafrika wenzetu wanaotambua mantiki ya baadhi ya maamuzi ya kiutendaji serikalini.
Na waafrika hao wala hawajui kuwa wapo wananchi wa nchi yake mwenyewe wasioelewa maana ya kazi zake za kizalendo zinazoongea siku zote kwa niaba yake.
Endelea kupumzika kwa amani JPM.