Naona watu wanapiga kelele tu hadi mtu makini kamaa The bold nae anaandika vitu kwa ushabiki, ile tunzo ilikuwa ni people's choice, ndomana kila aliengoza kwenye kura ndie aliekuwa mshindi katika mabara yote, sasa huku Africa aongoze alikiba alafu apewe Wizkid wala haijakaa poa kabisa, bora ile ya worldwide act ndo majaji wa mtvmama ndio walimchagua wizkid kuwa mshindi
Na kitu cha ajabu ni kwamba mtvema wali indicate kuwa Alikiba ndio mshindi ila mtvmama wakaingilia kati na kumtangaza mshindi wizkid, mbona hili wala halina kosa kwa upande wa Alikiba bali kuna tatizo upande wa waandaji wa tuzo, kwanini ashinde mwingine na apewe mwingine wakati kigezo kilikuwa ni kimoja tu ambacho ni wingi wa kura
Pia huyu wizkid alishawahi kuzitolea kashfa hizi tuzo kuwa wasanii wa kushinda waga wanaandaliwa ila yeye kabeba vipengele vyote ambavyo alikuwa kwenye nomination mtvmama na kama hiyo haitoshi mtvmama wanaenda kumpa tena tuzo ambayo hastahili hapa razima mtu uhoji kunani, endapo kama teamkiba wangeuchuna ndio ingekuwa imetoka
Kosa lipo tu kwa washabiki kwenda kutukana kwenye page ya Wizkid tofauti na hapo me sijaona tatizo na wala hakuna tuzo ambazo hazina figisu duniani kote, tushaona mara kinao wasanii kama chrisbrown, justin Bieber, nick minaj wakizipigia kelele tuzo hadi za grammy alafu uje ushangae kwa kiba kama sio unafki ni nini, wiz kafuta hadi tuzo za mama kwakuwa kajishtukia kuwa ataonekana ata hizo hajashinda kihalali so mtvmama wamemdharirisha wizkid pia wamejidharirisha wao pia