Tuzo ya Best African Act aliyopewa Wiz Kid imerudishwa kwa mshindi halali Ali Kiba

Sasa ule mkwanja wa tuzo Wiz atarudsha? Au ndio yale mambo ya wakuu wa mikoa na mwenge.

BTW hawa jamaa wanaondaa tuzo wamejidhalilisha sana na wamemuumiza sana Wizkid kwenye hili.
Nitafurahi Kiba akiikataa ili kutunza heshima yake pia.
Hahahah aikatae wkt anajua akisusa kuja tena kuchukua kashazeeka
 
Mahaba
 
Naona watu wanapiga kelele tu hadi mtu makini kamaa The bold nae anaandika vitu kwa ushabiki, ile tunzo ilikuwa ni people's choice, ndomana kila aliengoza kwenye kura ndie aliekuwa mshindi katika mabara yote, sasa huku Africa aongoze alikiba alafu apewe Wizkid wala haijakaa poa kabisa, bora ile ya worldwide act ndo majaji wa mtvmama ndio walimchagua wizkid kuwa mshindi

Na kitu cha ajabu ni kwamba mtvema wali indicate kuwa Alikiba ndio mshindi ila mtvmama wakaingilia kati na kumtangaza mshindi wizkid, mbona hili wala halina kosa kwa upande wa Alikiba bali kuna tatizo upande wa waandaji wa tuzo, kwanini ashinde mwingine na apewe mwingine wakati kigezo kilikuwa ni kimoja tu ambacho ni wingi wa kura

Pia huyu wizkid alishawahi kuzitolea kashfa hizi tuzo kuwa wasanii wa kushinda waga wanaandaliwa ila yeye kabeba vipengele vyote ambavyo alikuwa kwenye nomination mtvmama na kama hiyo haitoshi mtvmama wanaenda kumpa tena tuzo ambayo hastahili hapa razima mtu uhoji kunani, endapo kama teamkiba wangeuchuna ndio ingekuwa imetoka

Kosa lipo tu kwa washabiki kwenda kutukana kwenye page ya Wizkid tofauti na hapo me sijaona tatizo na wala hakuna tuzo ambazo hazina figisu duniani kote, tushaona mara kinao wasanii kama chrisbrown, justin Bieber, nick minaj wakizipigia kelele tuzo hadi za grammy alafu uje ushangae kwa kiba kama sio unafki ni nini, wiz kafuta hadi tuzo za mama kwakuwa kajishtukia kuwa ataonekana ata hizo hajashinda kihalali so mtvmama wamemdharirisha wizkid pia wamejidharirisha wao pia
 
my gbedu is final, wizzy baby baba nla won My girl wear designer, everytin wey I give am final eh r eh I no like wahala, oh wizzybaby baba nla won Say my gbedu is final, wen me drops everybody no dey tire eh e eh
 
Aisee hata kama kiba alistahili ile ni too much! Yale matusi ya fans wake kule kwenye page ya wizkid aisee!
Nafikiri kiba angetumia busara flani kuliko hivyo........
 
Seriously??? [emoji15]

Ndio kiba aone balaa aliloanzisha..

Mkubwa acha kupanic.
Naomba uthibitishe kwamba Alikiba aliwaambia mashabiki wake wakalalamike kwenye page ya MTV.
Pili kama Alikiba kuuliza vigezo then wampe tuzo kwasababu ya kulalamika sidhani kama ni rahisi hivyo ukilalamika tu unapewa hatakama hukustaili.

Hizi timu ni za hovyo hovyo sana huna tofauti na hao Timu Kiba walioenda kumtukana Wiz.wewe unakesha hapa kujaribu kupotosha watu kua Kiba na Management yake wamekosea.

Acheni Hizo.huyo Eddy alipolalamika alipewa?

Inakera sana kupotosha jambo ili kumfanya mtu aonekane hana Maana
 
Aisee hata kama kiba alistahili ile ni too much! Yale matusi ya fans wake kule kwenye page ya wizkid aisee!
Nafikiri kiba angetumia busara flani kuliko hivyo........

Mkuu kwani kiba Amefanyaje?

Mie nasema hizi tim ni za Hovyo sana.Unafikiri kiba anaweza kucontrol tem Kiba??
 
Don't settle for less while you deserve the best!
Wizkid hajawahi kushinda MTVEMA BEST AFRICAN ACT! Ingia weekpedia
Kiba kaweka Historia! He deserve it! Na kosa halipo kwake wala kwa Wizkid!
Kuna Nafasi hazijirudii Once for All! Mziki unacompetition, unashangaa next year hata nomination hayupo hata kama asingepata hii na kuacha kufuatilia.
Binafsi Nampongeza Jamaa! Kapata Zali, It is enough!
 
Tunzo Ndio mkatukane kama wehu kweli wabongo kwenye mitandao tunatia aibu sana tubadilike ili tuweze kupata network na mataifa Mengine mtu ambaye hajaelimika hujidai kwa matusi na aloyeelimika hujidai kwa hoja,.......
 
Jeh niyakwel ayoh?
 
Hii tuzo kila mwaka watakaowanominated wabongo itabaki bongo tu maana hakuna nchi Africa ambayo watu wake wanapiga kura kwa wingi kama bongo
 
fact
 
Asante
 
Mkuu kwani kiba Amefanyaje?

Mie nasema hizi tim ni za Hovyo sana.Unafikiri kiba anaweza kucontrol tem Kiba??
kiba anaweza asiwe na tatizo ila njia aliyotumia kulalamika kuhusu tuzo! na kama ulisikiliza xxl walikuwa kama wanapambisha mashabiki kwenda kulalamika kwenye page ya mtv!
Sasa mashabiki wake wamejikita kwenye page ya wizkid kumtukana!
Nafikiri hii inamharibia image pande ya kule,angelishughulikia hilo swala kimyakimya kwasababu yeye anawaelewa wabongo kwenye mitandao walivyo wehu!
angekuja kuwapostia baadae......sasa kule kunachimbika wabongo Vs waniger
 
Tunzo Ndio mkatukane kama wehu kweli wabongo kwenye mitandao tunatia aibu sana tubadilike ili tuweze kupata network na mataifa Mengine mtu ambaye hajaelimika hujidai kwa matusi na aloyeelimika hujidai kwa hoja,.......
Si Bora wametukana!
Marekani wanakushoot kabisa!
Watanzania Tumepewa Upole sana, Kuna Kipindi Lazima Tuwe Wakali ili Mambo yaende!
Nakwambia ukweli ukitaka kufanikiwa siyo lazima uwe na watu wote, wengine achana nao~
 
ushabiki wake kwa Diamond,, yaani huyu 'bold'kakomalia hili swala alikiba,, ameshindwa kabisa kuficha chuki aliyonayo kwa alikiba
Tangu hii issue ya tuzo ianze kutrend haha jamaa wamejitahidi kuonesha ni jinsi gani wanaona kuwa kiba hafai kupata tuzo kubwa,, uzuri hawakuficha hisia zao, hamna jema wanaloweza kusema juu ya alikiba, zaidi Sana watajifanya wanabishana kwa hoja huku wakipotosha Hali halisi
Mimi kwa kujua kuwa hawatafurahia Ali kushinda nikasema kuwa haters watakuja na Mada potofu kama
1.kiba kalilia tuzo
2.wizkid atamuelewa vbaya alikiba
3.ali hatanominatiwa tena kisa kadai haki yake.
Na bado wataleta post nyingi wakijitia busara busara kibao!!,, !!
 
Whatever it is!
Me naamini No body can block your blessings as long as they are coming from God!
Usiogope, Huu ndiyo Mziki!
Apate Collabo au asipate Collabo, as long as he lives, Muda ukifika atatoboa!
Take it from me, you can only control yourself but not others!
Mashabiki huumia sana kuliko wahusika 100%!
Unakumbuka shabiki yule wa Yanga alikuwa analia kabisa???
Huwezi kukontrol hisia za mashabiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…