TV Mpya vs. Mtumba: Ipi ni Bora kwa Bajeti ya Milioni 1.5

TV Mpya vs. Mtumba: Ipi ni Bora kwa Bajeti ya Milioni 1.5

Wataalamu wa mambo naomba msaada wenu katika uamuzi huu. Nina bajeti ya milioni 1.5 kwa ajili ya kununua TV, na leo nimezunguka madukani kutafuta chaguo bora.

Katika maduka ya bidhaa mpya, nimepata TV mbili zinazovutia:

  1. Hisense 65A6K/N – UHD Smart 4K
  2. TCL UHD Smart 4K
Zote zinauzwa kwa milioni 1.5, na zinakuja na zawadi za HDMI cable, Wall bracket, na delivery ya bure. Pia, zinakuwa na warranty ya mwaka mmoja.

Baada ya hapo, niliamua kutembelea maduka ya bidhaa za mtumba. Huko, nilipata chaguo mbili za kuvutia zaidi:

  1. Sony Bravia 65XE7002 – UHD Smart 4K, Made in Japan (2017)
  2. AVA FFalcon 65UF1 – UHD Smart 4K, Made in Australia
TV hizi za mtumba zinauzwa kwa milioni 1.4, lakini hazina miguu (stand), remote, wall bracket, HDMI cable, wala delivery ya bure. Pia, warranty inayotolewa ni ya miezi 6 pekee.

Sasa, nimebaki nikitafakari kama nichukue TV mpya za Kichina (Hisense ama TCL) ambazo zinakuja na warrant ndefu na vifaa vya ziada, au nichukue Sony ya mtumba, ambayo ni brand kubwa na inajulikana kwa kudumu muda mrefu, licha ya kuwa na warranty fupi.

Kwa kuzingatia ubora wa picha, uimara wa TV, na faida za kila chaguo, je, wadau mnanishauri nichague ipi? Nipo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wenye uzoefu wa vifaa hivi.

Asanteni sana!
Chagua kuoasingle mother au bikra
 
Back
Top Bottom