Uchaguzi 2020 TV na Redio hazitangazi ujio wa Lissu, lakini mbona watu ni wengi?

Uchaguzi 2020 TV na Redio hazitangazi ujio wa Lissu, lakini mbona watu ni wengi?

Naanza kuogopa na kuwashangaa wanaobeza mitandao ya kijamii na nguvu yake.

Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla imezibiwa kutangazwa na TV na Redio za nchi hii kueleza kwa ufasaha ratiba na Sera za CHADEMA, lakini jambo LA ajabu mwitikio kila mahali aendapo ni mkubwa mno.

Tena tunaweza kusema mkubwa kuliko wa Rais aliye madarakani kwani yeye kuna vigezo vya mahudhurio yake;
1. Wasanii wanakundikwa.
2. Watu wanabebwa na malori.
3. Wafanyakazi wanalazimishwa kuwepo.
4. Wanafunzi wanavuliwa uniform na kujazwa viwanjani.
5. Ushawishi maslahi unafanywa. Yaani chakula, vinywaji na tisheti.

Sasa hawa wa Lissu wanapashanaje habari kuwa bingwa kesho au kesho kutwa tunaye? CCM wanapaswa kujua mpango huo wa kuwanyima haki ya kutangazwa wamefeli mazima.
Tunatumia redio za mabeberu
 
Ukisubiri umeliwa. Hakuna alieamini kuna wa kumpeleka puta Magu 2020. Kila mtu alijua utakuwa mteremko. Hiyo generation change haiji tu automatic. Inachochewa. Tundu Lissu anatengeneza momentum kila uchao. Hiki ni kibarua cha kila uchaguzi. Hata kama Magufuli atakuwa rais tena, sidhani ataendeleza mwendo uleule.

Ccm watakuwa wamejifunza kwamba Magufulinomics na Magufulism hazilipi

Hata Ile hamu ya kuongeza mda ili atawale milele kwa Moto huu hamu hana
 
Ili ikae sawa, ungesema hivi, kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza........

Hiyo ndiyo hali halisi ilivyo hivi sasa kati ya washindani hao wakuu wawili ambao ni CCM VS CHADEMA

Chadema ndiyo inayojiuza na CCM ndiyo inayojitembeza kwa nguvu ili ipendwe!
Kwann ccm isiwatumie polisi iwalazimishe watz kuipenda
 
Naanza kuogopa na kuwashangaa wanaobeza mitandao ya kijamii na nguvu yake.

Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla imezibiwa kutangazwa na TV na Redio za nchi hii kueleza kwa ufasaha ratiba na Sera za CHADEMA, lakini jambo LA ajabu mwitikio kila mahali aendapo ni mkubwa mno.

Tena tunaweza kusema mkubwa kuliko wa Rais aliye madarakani kwani yeye kuna vigezo vya mahudhurio yake;
1. Wasanii wanakundikwa.
2. Watu wanabebwa na malori.
3. Wafanyakazi wanalazimishwa kuwepo.
4. Wanafunzi wanavuliwa uniform na kujazwa viwanjani.
5. Ushawishi maslahi unafanywa. Yaani chakula, vinywaji na tisheti.

Sasa hawa wa Lissu wanapashanaje habari kuwa bingwa kesho au kesho kutwa tunaye? CCM wanapaswa kujua mpango huo wa kuwanyima haki ya kutangazwa wamefeli mazima.
Wanatangza wao wenyewe mitaani halafu wanasema wananchi wamekuja wenyewe bila kutangaziwa...wakati mwingine tunajidanganya sana. Wanakesha wiki mzima kutangazia watu Ohio wa viongozi wao
 
Back
Top Bottom