TV1 Kurusha Live ligi kuu ya Uingereza(EPL)

Bora tu aisee! Nami nifaidi epl bhana kila siku niwe naskiliza kwa radio tu
 
Kituo cha Televisheni nchini, TV1 leo hii kimezindua kampeni yake inayokwenda kwa jina la Toroka Uje ambayo inawaletea watazamaji wake matangazo ya bure ya mechi zote za ligi kuu ya Uingereza maarufu kama English Premier League zitakazoanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 13 mwaka huu.

Akizungumzia kampeni hiyo Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Sayi alisema kuwa watanzania kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuangalia ligi hiyo maarufu duniani lakini kupitia TV1 ambayo inapatikana kwenye king’amuzi cha Startimes, watanzania watakuwa wakitazama mechi hizo bure bila gharama yoyote.


Naye Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu aliongeza kuwa mbali na watazamaji wa TV1 kufurahia mechi hizo ambazo zitarushwa kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho wa ligi, pia wamejiandaa kukutana na watazamaji wa TV1 kupitia michezo mbalimbali, matamasha na mashindano yatakayokuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo vifurushi vya king’amuzi cha Startimes na nyingine kibao.

Akizungumzia kuhusu kampeni hiyo ya Toroka Uje, Mkuu wa Uzalishaji vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo, alisema kuwa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tarehe 10 mwezi huu kitakuwa katika siku tatu ambapo kutakuwa na mijadala ya kandanda, mpira laivu na uchambuzi kuhusu mechi zijazo ambapo uchambuzi huo utaongozwa na wachambuzi wakubwa akiwemo Dr Leaky Abdallah na Ally Kashushu.

Aidha Meneja Masoko wa Startimes, Damien Li aliwahakikisha Watanzania kuwa Startimes haitaongeza bei ya vifurushi wala kutoza chochote kwa watazamaji wa Ligi hiyo kupitia TV1 kwa kuwa ni bure kabisa.
 
Mkuu TV1 inapatikana pia kwenye king'amuzi cha Azam, je tutaona live kupitia huku pia? Au TV1 ya startimes na TV1 ya Azam ni tofauti?

Ufafanuzi tafadhali.
 
Kwenye kunitangaza wanasema watarusha zote labda na marudio sijui, ila ukweli utajulikana ligi ikianza.
 
Hii nchi wanamichezo tunapata shida sana.Heri tungekuwa walevi wa kitu kingine
 
Umeeleweka
Hakuna jipya km CRTV ya Cameroon tu
 
bora itupunguzie adha ya kwenda vibandaumiza na bukubuku zetu kwa sie tusio na DSTV.
 
Hawawezi kuonesha mechi zote,wakat mwingne huchezwa pamoja
 
Wasidanganye mechi zote kwani nyingine zinachezwa muda mmoja pili chaneli hyo itakuwa ya EPL tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…