Mbona unatudanganya mchana kweupe mkubwa?
Bure kivipi wakati kila mwenye king'amuzi hicho cha Startimes;
Kwanza havigawiwi bure, ni sharti ukanunue
Pili ni lazima ulipe fundi ili akufungie na;
Tatu, lazima ulipie moja ya vifurushi vya king'amuzi hicho!!
Sasa, niambie ubure hapo uko wapi aisee?
Na kwa faida yako tu, kununua haki za kurusha matangazo ya mpira ya moja kwa moja (live) ya ligi mbili kubwa duniani EPL (England) na La Liga (Spain) ni very expensive to the extent that ili upate kuona mechi zote ni sharti uchomoke hasa!!
Ndo kusema kuwa, hapa mnavutwa mtoroke kwa wingi ili jamaa wauze ving'amuzi vyao kwa kwa lengo na idadi wanayotaka huku kweli mkioneshwa kwa siku flani flani mechi za EPL pengine bure kweli na baada ya hapo mnakuwa mmebanwa engo na kulazimika kulipia!!