The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Kwa mujibu wa utafiti wa TWAWEZA asilimia 67% ya watanzania wako tayari Kulipa tozo kwa sababu wanatambua ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Kwa matokeo haya ni wazi Waziri Mwigulu na serikali inazidi kuwaumbua CHADEMA ambao kila siku ni kudandia hoja na kupotosha 😂😂.
CHADEMA kazi mnayo, tafuteni hoja za kwenda nazo kwenye uchaguzi 👇
=============
Maoni ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya pesa kwa njia ya simu yanatofautiana. Wananchi walio wengi wanakubali kwamba tozo hizo ni njia muhimu ya serikali kupata mapato (asilimia 67) na kwamba inahakikisha kuwa kila mtu anachangia maendeleo ya taifa (63%). Hata hivyo, wachache wanakubali kwamba tozo hizo zitapunguza utegemezi kwa wafadhili (46%) au kwamba kodi kwenye miamala ya pesa kupitia simu ni jambo zuri (43%).
Wananchi wanaonesha dalili kwamba wangeunga mkono zaidi tozo hizo iwapo wangekuwa na taarifa kamili za namna mapato yanayopatikana yanavyotumika. Wengi (63%) wanasema wangekuwa tayari zaidi kulipa ushuru kama wangefuatilia jinsi fedha zinavyotumika. Wachache wanasema wanajua jinsi fedha hizo zinavyotumika (39%) au wanaweza kujua kwa urahisi kutoka serikalini matumizi ya fedha zilizokusanywa (44%).
Walio wengi pia walikubaliana na pendekezo kwamba tozo yenyewe siyo tatizo bali gharama za miamala zinazotozwa na watoa huduma (66%) na kwamba tozo hiyo inapaswa kutumika tu kwa miamala mikubwa (52%). Miongoni mwa wale wanaokubali kwamba tozo hiyo ni njia muhimu ya kuongeza mapato kwa serikali wanasema viwango vya kodi hiyo ni kubwa (26%) kuliko wale ambao hawakubali (11%).