TWAWEZA: Asilimia 67 ya watanzania wanakubali kwamba tozo ni njia muhimu ya serikali kupata mapato

TWAWEZA: Asilimia 67 ya watanzania wanakubali kwamba tozo ni njia muhimu ya serikali kupata mapato

Utafiti huo ni fake,sisi Watanzania 99.9% tunakubaliana na tozo kwa maendeleo ya Nchi.
Tena iongezwe kwa asilimia mia tano kabisa ili viongozi wetu na wateule wa Rais waishi kama malaika na sisi tuishi kama vibwengo
 
Kuna utafiti pia uliwwahi kusema, katika watanzania idadi kadhaa kuna machizi kadhaa, ni vyema wakatueleza hawa 67% wapo upande.
 
Wacheni upumbavu wenu, Serikali na Bunge lenu wenyewe mkiyakoroga lazima muitaje Chadema. Mnaleta tafiti zenu za mchongo mnafikiri ndiyo zitatoa hasira ya wananchi? Chadema wanahusika nini kwenye maujinga yenu? Mtanyooka tu, ili mradi mshaanza kutengeneza tafiti fake tayari maumivu mnayo.
Hawa jamaa wajinga sana, washanyooka tayari. Wanahangaika kutengeneza fakes wakati wananajua original results zipo kwenye tovuti ya Twaweza.

Wapuuzi tu hawa.
 
Unahoji ccm tu alafu unakuja ujinga hapa jf , hivi Janvi hili mnafikili Kuna vilaza ,? Jf imejaa watu Makin ,wenye busara na kitu, hamjiulizi why ina watu laki tano au sita? Ni KWa sababu wengi wanaliogopa jukwaa hili, utaandika ujinga insta,facebook, sijui wapi, ila sio jf, Kama ni mgeni kaa chini na tafakari upya hii ni jf
 
Watanzania gani hao waliohojiwa wakatoa majibu hayo?
Uhalisia wa wananchi juu hizi tozo uko wazi kabisa yakwamba hatuzitaki.
 
Tozo ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu!
 
Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, hence Wananchi.
 
Wamekosea

Labda Kama asilimia HIZO ni wale tunataka katiba MPYA!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba mpya"!
 
IMG-20180405-WA0006.jpg
 
Kwa mujibu wa utafiti wa TWAWEZA asilimia 67% ya watanzania wako tayari Kulipa tozo kwa sababu wanatambua ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Kwa matokeo haya ni wazi Waziri Mwigulu na serikali inazidi kuwaumbua CHADEMA ambao kila siku ni kudandia hoja na kupotosha 😂😂.

CHADEMA kazi mnayo, tafuteni hoja za kwenda nazo kwenye uchaguzi 👇

=============

Maoni ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya pesa kwa njia ya simu yanatofautiana. Wananchi walio wengi wanakubali kwamba tozo hizo ni njia muhimu ya serikali kupata mapato (asilimia 67) na kwamba inahakikisha kuwa kila mtu anachangia maendeleo ya taifa (63%). Hata hivyo, wachache wanakubali kwamba tozo hizo zitapunguza utegemezi kwa wafadhili (46%) au kwamba kodi kwenye miamala ya pesa kupitia simu ni jambo zuri (43%).

Wananchi wanaonesha dalili kwamba wangeunga mkono zaidi tozo hizo iwapo wangekuwa na taarifa kamili za namna mapato yanayopatikana yanavyotumika. Wengi (63%) wanasema wangekuwa tayari zaidi kulipa ushuru kama wangefuatilia jinsi fedha zinavyotumika. Wachache wanasema wanajua jinsi fedha hizo zinavyotumika (39%) au wanaweza kujua kwa urahisi kutoka serikalini matumizi ya fedha zilizokusanywa (44%).

Walio wengi pia walikubaliana na pendekezo kwamba tozo yenyewe siyo tatizo bali gharama za miamala zinazotozwa na watoa huduma (66%) na kwamba tozo hiyo inapaswa kutumika tu kwa miamala mikubwa (52%). Miongoni mwa wale wanaokubali kwamba tozo hiyo ni njia muhimu ya kuongeza mapato kwa serikali wanasema viwango vya kodi hiyo ni kubwa (26%) kuliko wale ambao hawakubali (11%).

Wanajitekenya halafu wanacheka wenyewe. Nonsense
 
Back
Top Bottom