vijana wenzangu tuwe macho sana na hawa wazee hili swala usiingie kichwakichwa matokeo ya serikali mbili au tatu yatalifaidisha kundi mojawapo ndani ya ccm na sio wewe wala ndugu yako, CCM imegawanyika mara mbili kuna wa serikali 2 na tatu kwa maslahi bnafsi. cha msingi tuconcetrate na na maswala muhimu kwenye katiba yetu kama afya, miundombinu, elimu na malazi. katiba inasema nini juu ya haya, hata wao wakiamua nchi iongozwe na jaji mkuu au spika hayo ni yao wanasiasa.
Hujatulia wewe! Unafikiri hata kama afya,elimu na mengine yakiwekwa kwenye katiba kama ccm wakiendelea kutawala haitakusaidia chochote, hata katiba ya sasa ina mambo mengi tu mazuri lakini hakuna kinachofanyika! Unadhani haki ya kupata huduma ya afya haipo. Kwenye katiba? Lakini nini kinachoendelea sasa? Ccm haitaki mabadiliko yoyote ili iendelee kutawala.