Kiongozi nadhani hujamuelewa Zitto Kabwe, na umefanya vibaya sana kuanzisha thread ambayo inamshambulia na kuwafanya wasomaji wawe biased na kumshambulia serious. Zitto anakubaliana na hoja za Warioba siku nyingi, Zitto Kabwe ameunga mkono hoja ya serikali 3 wazi wazi, nilichoelewa kwenye tweet yake ni kwamba anaona kuwa solution ya Muungano ni serikali Tatu lakini wajumbe wengi wa bunge la Katiba hawapo tayari kuchukua solution iliyopendekezwa na Jaji Warioba. Kwa hiyo kama wajumbe wa Bunge la katiba hawatapokea na kupitisha rasimu ya katiba kama ilivyopendekezwa na Tume ya warioba maana yake Muundo wowote wa serikali/Muungano utapelekea kufa kwa Muungano. Hivyo kama tutatoka na serikali mbili kama CCM wanavyotaka au Moja kama ambavyo wachache walipendekeza Basi anachokiona Zitto Kabwe ni kuwa Muungano utavunjika, hivyo anachotuambia ni kuwa tujiandae kisaikolojia kuona Muungano unavunjika, Sasa kashfa zote anazopewa zinatokana na nini Kiongozi???? nadhani Hukuuruhusu ubongo wako ujishughurishe zaidi ya kujenga conclusion kutoka na imani zako za nyuma, SIO VIZURI HIVYO mkuu tujitahidi wakati fulani kureason in professional way