Tweets za January Makamba na Zitto kuhusu Hotuba ya Warioba

Tweets za January Makamba na Zitto kuhusu Hotuba ya Warioba

Status
Not open for further replies.
Huyu January badala ya kutoa solution analeta maneno ya kanga halafu eti anataka kuwa RAIS shame on him anadhani Tume ilikurupuka kufikia uamuzi huo pia anatakiwa ajue Ndoa ya muke na mume si sawa na Ndoa ya kuunganisha sehemu mbili kimantiki kuwa na serikali tatu haifanani na kuongeza mke wa tatu .....SHAME ON YOU JANUARY.

MKUU kwani kuna ndoa hapo ndoa ni muunganiko wa watu/pande mbili 1 inaonekana tunaitaka hii nyingine ndio ndoa iboreshwe??
Tanganyika yetu IPO wapi jamani??
 
Kwa mtu mwenye akili timamu tuu ndie anayeweza kutambuwa kuwa kuwa na Serikali tatu ni kupelekea kivunjika kwa muungano, kwanza historia ya muungano huu na umri wake sasa umekuwa na umri mkubwa miaka zaidi ya hamsini , muunganiko au muingiliano wa jamii zetu yaani makabila pia Vyama vya siasa ambavyo viko bara na visiwani ni ushahidi tosha kbs kuwa Muungano huu unapaaswa kilindwa kwa ghalama yeyote ile, Muundo wa serikali tatu 3 siyo kwamba tunakataa lkn safari yake itakapo anza itapelekea Mambo mengi ki utekelezaji yakianza kuhojiwa na yakikosa majibu haraka suluhisho litakuwa ni kuvuja muungano ki rahisi sana kuliko wakati wowote ulivyo sasa, sasa pamoJa na Mapendekezo yoote aliyoyatoa mh warioba na tume yake lkn mtambuwe kuwa sasa muungano hakuna siku Si nyingi, Hivyo cc tunaoona kuwa Muungano uko katika hatari ya kuvunjika tuta tetea kwa ghalama yeyote kuulinda.
 
Zitto umeniangusha kwa hili. sikutegemea kama unaweza kuwa low kiasi hiki. serikali 3 ndo mpango mzima, kama hutaki tupishe.
 
Kwa mtu mwenye akili timamu tuu ndie anayeweza kutambuwa kuwa kuwa na Serikali tatu ni kupelekea kivunjika kwa muungano, kwanza historia ya muungano huu na umri wake sasa umekuwa na umri mkubwa miaka zaidi ya hamsini , muunganiko au muingiliano wa jamii zetu yaani makabila pia Vyama .....
we watukane tu lakini mwishoni tutaweza kupima ni nani mwenye akili timamu kati yako na wao.
Hivi anayevunja muungano ni Tume ya warioba au hao wanaompigia mizinga raisi wao ndani ya nchi nyingine!?
Kama ni hoja ya kuoleana inaweza kuwa sawa lakini ukumbuke kuwa Watanzania (watanganyika???) wameoleana pia na Msumbiji, Malawi, Zambia, Congo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na hata Comoros mbali na hizo nchi nyingine kama Oman, USA, nk!
Cha msingi sote tukumbuke kuwa uzuri wa Muungano ujikite kwenye urahisi wa kutoa maamuzi ya maendeleo na sio kila siku kulalamika tu, inapoteza muda wakati dunia nyingine ikipiga hatua. Wenye akili za ukweli ni wale wanaosema SERIKALI MOJA.

 
wanaweza kutumia uwingi wao, wao ni wachache kuliko wananchi waliowatuma. wabunge wa ccm hata kama wangekuwa alfu moja, ni wachache kuliko wananchi walio nje wanaowaangalia ambao wanaweza kuamua kama katiba mpya itengenezwe tena hata baada ya mwaka mmoja wa hii mpya kupatikana. cha muhimu ni kwamba, wananchi wengi wanajua maana ya nini lisu na warioba walikuwa wanasema, na wapinzani ninaamini kuanzia mwakani wakati wa kampeni, wataendeleza awareness kwa watu na hakika ccm wataaibika na kutupiliwa mbali kwa hoja zao za ajabu kama hiii ya makamba. watu wenye mawazo kama ya makamba ndio walioifikisha hii nchi kwenye umasikini kama huu wa leo, na ni watu ambao tz hatutakiwi kuwa nao kabisa kwenye uongozi.
 
Kwa hiyo Zitto anapingana na makala yake moja, tena ya mwaka huu, akiunga mkono serikali 3?

hiyo ni kabla hajanunuliwa kwa ajili ya katiba mpya.tutegemee nini kwa muasisi wa Aliance for Cowards ana Traitors
 
Kwenye swala la Katiba tukubali kutofautiana.Hoja kinzani husaidia kuibua madhaifu ya kila hoja.Zitto anao uhuru wa kutoa mawazo yake kama mimi na wewe ingawa wengi tungetamani Zitto awe radical kwenye issues kama hizi akiwa upande wa sera za chama chake maana yupo pale kwa mgongo wa chama hicho na serikali tatu ndio sera yake.
 
January Makamba ‏@JMakamba 10m Kilichofanyika Bungeni leo ni kuorodhesha matatizo ya ndoa (ambayo ni ya kweli) halafu kisha kusema kwamba kuongeza mke ndio jawabu lake.

Tumwulize JMakamba: Kwa serikali 2 nani amemuoa mwenzake? January anaendeleza yaleyale aliyoyasema Jaji Warioba kuwa wanadhani Tanzania bara ndio serikali ya muungano. Au pia wanafaidika kisiasa na mfumowa Tanganyika kuvaa koti la mungano.
Jaji Warioba ameweka wazi msingi wa uraia. Maana yake km Marekani ilivyo, utaifa utabakia kuwa mmoja. Maana yake ni pasipoti moja tu ya Tanzania. Kwa kifupi na nilivyomwelewa Jaji, nchi itabakia moja yenue serkali 3.
 
Last edited by a moderator:
Huyu ndo eti naye anataka kuwa Rais; hoja kaishiwa anataka kutumia wingi wao....rubbish
 
hakuna hotuba nzuri kama ya warioba leo, na yenye kueleweka, hata mbumbumbu angeelewa. huyu mzee ni noma.
 
Kulazimisha mifano ya ndoa katika suala muhimu namna hii ni jaribio la kudunisha mjadala juu ya muundo wa Muungano kama unavyojitokeza katika Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.
Mifano ya aina hii inayalenga,pamoja na mambo mengine,kuwapa faraja ya kitambo kidogo wahusika ambao badala ya kutumia akili katika suala hili wanatumia hisia na ulaghai.
 
Naye ndio anataka kuwa rais wa JMT?nchi hii haishi vituko
 
Hawa wanaotaka serikali tatu ni mahututi kiakili zanzibara wapende wasipende watakuwa ndani ya serikali mbili
 
This guys is coward and kwa kweli amenikera sana, iinaonekana sasa ni shabiki wala hajui hata umhimu wa tafiti zinazofanywa; nilitegemea a comparison analysis of live and dying union government, ni dhahiri zitto anafaidiaka na mfumo huu wa ccm; ni dhahiri ana mgao wa kutosha kutoka katika mfumo huu batili kabisa katika jamii yoyote duniani; zitto anatweety. Akili za aina hii sijui hatawanapataje bahati kupata hata nfasi za ubunge, zitto mtu hovyo kabisa, nilitegemea aeleze hoja then atoe uchambuzi wa kitafiti kupingana na hoja za warioba; by th way already rasmu tunayo tayari uda mrefu alitegemea wanakuja kutoa tofauti?

Maelezo ya warioba kiukweli ni opportunity kubwa sana tena yenye suluhisho

Zitto: "Tujidae kisakolojaia kuvunjika kwa muungano"

Hivi kuna anayeweza kuniambia kwa dhati ya moyo wake madhara makubwa wanayoweza kuyapata watanzania wa kawaida kule Nanyumbu, Liwale, Mkuranga, Ulanga na kwingineko kama huu muungano utavunjika hata leo hii?? Ukiondoa wanasiasa nini hasa mtanzania huyu amefaidika nacho kwa dhahiri kabisa na huu muungano?? Kama umemsikiliza Mhe Warioba vizuri leo utabaini kwamba huo unaoitwa muungano (kwa maana ya nchi moja yenye dola mbili kama ilivyokusudiwa awali) ulishavunjika zamani mbona?? sasa uvunjike mara ngapi?? Kilichopo sasa nilivyomuelewa Warioba kwa maelezo yake ya kina ni kiini macho tu cha muungano.
 
Mipasho imeanza, wanamfungulia njia baba Ritzmoko hiyo Ijumaa, halohaloooooo!
Ushauri wa bure: baba Ritzmoko amuige jaji namna ya kuongea kama msomi, taratibu, kwa kujiamini na "gestures" za ki-stateman sio zile zake za kukurupuka, kujichekeshachekesha, mifano ya kipuuzi kama huo wa Makamba etc
Washauri wake mnafanya kazi gani?!
 
Kabila yangu wanafanya kama mfano wa Januari unavyoeleza. Kwetu hakuna kuacha mke. Unaoa mwingine. Matokeo yake mara nyingi mume kufa mapema tu. Wajane kwenye kabila yetu ni wengi sana.


Tujadili hoja ya January badala ya kumjadili yeye na Babayake.
 
Anajibu hoja za mzee kwa maneno mepesi na ya kipuuzi kabisa, huyu naye anataka Urais..!!??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom