omujubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 4,326
- 2,506
Huyu jamaa ni mtata na sasa anaumbuka, ni suala la muda tu. Hebu angalia hapa alipoandika baada ya kutoka kwenye kikao alichokuwa mwenyekiti (PAC). Yaani anaandika utafikiri yeye sio Mtanzania na hayo mambo hayamhusu, kwa maana tulitegemea kwa nafasi yake kama mbunge angesaidia kuamsha hisia ili wananchi wa kawaida tuamke kuipinga IPTL.Zitto Kabwe: Watanzania watakapoamka watakuta hili saga la #IPTL limegharimu Taifa takribani dola nusu bilioni. #TegetaEscrow
Kwa hakika ameisaliti cdm iliyomkuza na wengi hawakujua kuwa kwa kufanya hivyo amewasaliti wananchi kama ccm na sasa eti anapimana ubavu na mwandishi wa Katiba ya mwaka 1977 Mzee Warioba kana kwamba yeye anaelewa na ni mzalendo zaidi yake!
Na huyu mtu anafanya PhD!