Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Hawa wenzetu lazima wapige kazi... Mifumo Yao ipo Bora sana... Sasa angalia mtu unaenda kazini nyumbani hapaeleweki, mishahara tiatia maji. Mtoto akiumwa unapandwa na kizunguzungu, bima huduma hazieleweki. Ulaya ni Ulaya tu, huduma za kijamii, mishahara bonus plus fairness acha tu. Lazima upige kazi
 
Hao viongozi wabovu waliopo Afrika wametoka wapi???
Ukiona kuna viongozi wabovu ujue kwamba pia kuna wananchi wabovu.
'Daima mtoto wa nyoka ni nyoka.'
 
Muafrika ana error kwenye gene yake. Kupenda starehe kuliko kazi. Wakati wenzetu wanaluwa drived na kazi then starehe. Is why wanapiga hatua sisi tukibakia kulalamika?
Kitu lingine nilichojifunza kwa hawa wenzetu wazungu wanavyokuja Afrika ni watu wanaozingatia bajeti sana hata awe na pesa nyingi huwezi kukuta anafanya matumizi ya hivyo au kumpa ofa mtu bila sababu za msingi

Sisi huku kunatabia ya ujamaa mtu wapo vijana wanapata pesa lakini inaishia kuwanyeshwa wana pombe ata akiamka hana kitu yeye anaona sawa tu
 
Usifananishe kubeba zege na kunyanyua mabox kwa forklift ni mbingu na ardhi
 
Coffee kaka..mchawi coffee..mim siwez ingia shift huku bila coffee..siwez toboa
Nalipwa euro 13 kwa saa,..napiga 12hours
 
Hii sio sababu, watu wanalipwa 5M hii bongo na bado kazi tia maji tia maji tu
 
tatizo ni aina ya viongozi tulio nawo wanawaza miaka 5 wakaibe kur basi,
wezetu wamejiwekea mazingira mazuri hata ya kufanya hizo kazi,
wewe upo kazini ujitume huku bosi wako anawaza madili haiwezekani kuwa hari ya kujituma nawe utawaza wizi tu!
 
Turudi nyuma twende mbele, au twende nyuma tu.
 
Mkuu!

Hawa wenzetu wamefanya sehemu ya kazi iwe haina tofauti na nyumbani! Yani mtu akiwa kazini anajihisi raha kama yuko nyumbani tu, huku mpunga wa maana Ukingia!

Huku kwetu mahala pa kazi ni kama jehanamu, uchawi, majungu, wivu, umbeya n.k.
 
Mkuu hata mimi hapa hapa Afrika nilipo tunafanya kazi masaa 12 ila baadhi tuna likizo ya mwezi mmoja kazi miezi miwili, hapa hapa kuna wenye likizo ya wiki 1 kazi wiki 2 huku wengine wakiwa na likizo ya wiki 3 kazi wiki 6. Hao unao waongelea ndo wanafanya kazi masaa nane ila likizo ni moja kwa mwaka.
 
Kina mangi hawapo huko?
 
Mdau umeongea ukweli wote.

Ila ndio hivyo malipo yetu pia ni kiduchu ujue
 
Na hawachagui sana..huku kukuta mtoto maisha mazur home..anapiga kaz ya kibarua supermaket ni kawaida .yaan level ya kuona noma hawana hawa watu..kila mtu na maisha yake
Upo ulaya nchi gani mkuu
 
Mbunge analipwa mafao kila baada ya miaka 5 na si 10.Hapo kwa walimu , hiyo 500k ni secondary lakini primary wanakula hadi 350k.
Unafikiri huyo mwalimu afanye kazi mpk siku za jumamosi hadi jumapili na afundishe mpk saa 1 usiku na wanafunzi wote wapate dvn 1.
Unafikiri huyo mwalimu wa 350k atakuja kumzidi maendeleo mbunge kwa miaka 5? Issue siyo kufanya kazi kwa bidii bali ni mshahara mnono. Ukilipwa vizuri, utanunua trekta, utalima hekta nyingi kwa muda mfupi na utatumia kilimo cha umwagiliaji.
 
Mdau umeongea ukweli wote.

Ila ndio hivyo malipo yetu pia ni kiduchu ujue
Maisha lazima ule bata. Angalia mifano ya matajiri wanavyoishi kila wikiend wanatoka na familia kula bata. Angalia matumizi yao kwa siku.
Unafanya kazi ili upate pesa uzifanyie nini? Unaingia kiwandani tena cha wahindi, kazi ngumu unafanya kazi saa 1 asubuhi mpk saa 1 usiku halafu unalipwa 7,000. Kuna mjinga anasema watu hawafanyi kazi😁😁😁😁😁
 
Tatizo malipo mkuu.
Hata mm natamani sana kuchapa kazi day & night ila shida kazi haiendani na malipo, utajiumiza mwisho hiyo akiba kiduchu uitumie kujitibu.

Hao wenzetu washaseti mifumo mizuri ya kumwezesha mfanyakazi kutopata shida ndogondogo hasa akiwa mchapakazi.
 
Ndio aisee, huko mtu kupiga kazi masaa 15 kwa siku kawaida, na wanajituma haswaaaa
Sasa kwa saa analipwa let say dollar 50 kwanini usikomae masaa 15 utakua umechota dollars ngapi

Njoo huku saa 1
 
Akiumia kazini analipwa
Akiugua kazini analipwa
Akipata tatizo kazini analipwa
Akijikwaa kazini analipwa
Akianguka kazini analipwa

Njoo wewe huku ugua tu kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…