Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Tatizo waafrika hasa watanzania wamesharidhika na umaskini wao.

Wala hawana muda wa kupigania haki zao za msingi.

Juzi kati hapa madaktari wa Kenya wamekinukisha kushinikiza serikali iwaongezee na kuboresha maslahi yao.

Watanzania ni kusifia kila kitu mama anaupiga mwingii.
Hata ungekuwa wewe usingeweza kuandamana. Ilishatokea madaktari wakaandamana ila mkuu wao, alitekwa na watu wasiojulikana na mpk leo hakuna kesi ya kutekwa. Ilikuwa kipindi cha Kikwete
 
hakika,huko watu wakiwa kazini akuna story akuna simu ni kazikazi.

mfano huku kwetu bank kuna madirisha sita tellers,ila dirisha linalohudumia ni moja tu msululu wa watu na bado huyo muhudumu dakika moja simu dakika moja anahudumia.
Sababu hawalipwi kwa saa ajitume asijitume mwisho wa mwezi atapokea yote.
Kule ukichezea simu mfumo unakutoa nje pia usipojituma unajiibia mwenyewe
 
Mfano.
Idadi kubwa ya watanzania wanategemea kilimo cha mvua. Kibaya zaidi wanalima kwa kutegemea jembe la mkono na mbegu wanatumia za kizamani.
Hayo mazao wanapata faida ya kubadilisha yao?
Watu wanafanya kazi sana ila shida ni teknolojia na mishahara duni huku gharama za maisha zikiwa juu
Huku uhakika wa kesho haupo thus watu wanapiga ukiwa na pesa upo juu ya Sheria kufungwa ni kupenda kwako
 
Bila kusahau na kodi wanalipa, njoo kwetu huku........ kukwepa kodi ndio ujanja.
 
Sababu hawalipwi kwa saa ajitume asijitume mwisho wa mwezi atapokea yote.
Kule ukichezea simu mfumo unakutoa nje pia usipojituma unajiibia mwenyewe
hapana iyo sio sababu,hali hiyo kwa hapa bongo niliyotolea mfano huwa inatokea sana kwenye bank au taasisi za umma,taasisi,bank au biashara binafsi uwezi kuta iyo hali na awalipwi kwa masaa.
 
Hii kaulimbiu yako ya twende mbele turudi nyuma ndo imefanya nyumba nyingi zimeishia kwenye renta.
Kama tunaenda mbele twende tu kama tunarudi nyuma tirudi.
mambo ya kwenda mbele na kurudi nyuma at the same time HAPANA.
 
Sawa mimi ni mediocrity
wewe umefanya nini cha maana huku duniani
Cha maana ni nini?

Kila mtu ana vitu vyake anavyoona vya maana hapa duniani na wengine hakuna cha maana kwao hapa duniani

Kuna watu hata uhai hauna maana kwao, wanataka wafe tu. Kifo ndio cha maana kwao.

Kwa hiyo "cha maana" depends upon your frame of reference.
 
Mwafrika hasa mtanzania anataka apige kazi masaa nane tena hayo bado anaona ni mengi,

Awahi kutoka kazini apitie baa amwagilie moyo na nyama choma huku akibishana simba na yanga.

Wanawake wanataka wawahi kutoka kazini wapitie saluni wakajirembe huku wakipiga soga na umbea.

Halafu jumapili wakajazane makanisani wakipayuka kama mbayuwayu kumuomba Mungu wapate mafanikio.

Hawa ndio waafrika..!!d
Daaah hakika sisi weusi ni sawa na bure
 
Tanzania inakabiliwa na changamoto moja tu mfumo wa elimu ya juu haujakaa vizr coz watu wengi saivu wamesomea mambo ambayo hayapo kwenye maisha ya kweli na kama yapo basi ni kidogo sana kulinganisha na idadi ya watu walio somea kitu hicho.

Mfano; vyuo Vinavyo toa program za managers, supervisor, HRM vina idadi mubwa ya wanafunzi ukilinganisha na Vyuo vya ufundi.

Pia maeneo ya kuajiliwa ni machache sana kulinganisha na idadi ya wahitimu.

Fursa zipo na ideas juu ya maendeleo zipo ila wakuzisapot wapo bize kujenga shule.
 
Hata ungekuwa wewe usingeweza kuandamana. Ilishatokea madaktari wakaandamana ila mkuu wao, alitekwa na watu wasiojulikana na mpk leo hakuna kesi ya kutekwa. Ilikuwa kipindi cha Kikwete
Huweziacha kudai mfumo mzuri wa maisha yako na vizazi vyako kisa mwenzio katekwa ama kuuwawa. Hizi ni kauli za kioga , ujinga na umaskini na ndo tabia ya watanzania. Kudai mfumo bora ni vita na mnatakiwa kuwa na mbinu mbalimbali na si kukariri kuandamana tu.
 
  • Mbunge amekaa bungeni analipwa 200k km posho hapo bado mshahara ila mwalimu analipwa 500k kwa mwezi
  • Mafao analipwa akimaliza ubunge miaka 10 ila wengine wasubiri wafikishe miaka 50 halafu kuna kikokotoo
  • Huduma za afya ni changamoto
  • Elimu yenyewe unajifunza theory.
Tuna matatizo mengi sana kuliko watu wanavyofikiria na wala suala siyo kufanya kazi.
Mbunge analipwa mafao kila baada ya miaka 5 na si 10.Hapo kwa walimu , hiyo 500k ni secondary lakini primary wanakula hadi 350k.
 
Nadhani maswali yako mengi nimeyajibu kwenye vipengele vinavyofuata na mtoa mada nilimpa tu food for thought.., Hard Work does not Necessarily pay kwahio angeweza kuongelea efficiency na effectiveness lakini sio necessarily hassling... nadhani ndio maana nikasema ni vema tukaangalia uhusiano kati ya uvivu na umasikini

Suala la kupindua meza au kwanini tupo katika hii predicament nachoweza kukwambia ni Kwamba Necessity is the Mother of all Invention.... hao western tunaowasifia leo wala civilisation haikuanzia kwao na mengi wanayofanya either waliyaiga au kuwa-subjugate wengine (miji kama liverpool imejengwa na kujengeka sababu ya Utumwa) Nchi kama Belgium imejengwa kwa jasho la Congo) - Great Britain ni Kisiwa ilibidi watoke huku na kule kwenda kutafuta colonies ili waweze kuishi...; Egypt vitu kama irrigation vilianzia huko....,

Africa ingawa ukiangalia historically vitu kama pottery na ufuaji vyuma tulikuwa navyo lakini maisha ya huku mtu angeweza kuishi bila kujituma (kwanini uhitaji fridge wakati una mtungi, kwanini uhitaji AC wakati ukilala nje unapigwa Natural AC)

Kwahio huku tunapoelekea when the push comes to shove na maisha yanazidi kuwa magumu for better or for worse mambo yatabadilika (watu lazima tutapigana na kuchukiana) kwanini you might ask..., Sababu hatuna viongozi bora, tuna viongozi ambao ni walafi wanajenga kesho yetu ya matabaka na watu wenye nothing to loose..., kwahio ikifikia hapo All Hell will Break Loose.....

Hapo kwenye bold…

Hao viongozi wanatokana na sisi wananchi wenyewe, hawatoki kuzimu.

Kinachowajenga na kuwapa nguvu kuwa hivyo walivyo sasa ni jamii yetu. Wao ni zao letu, ni watu miongoni mwetu na matokeo ya mienendo ya jamii yetu.

Bado kuna jambo lipo linalosababisha hii tofauti kati yetu kuwepo.

Kama sisi tulikua bora zamani na hao wenzetu wameiga kwetu basi ni kwanini tunashindwa kurudi katika ubora wetu? Kikwazo haswa ni kipi?

Kwamba tumeshindwa kabisa hata kuanza upya basi? What really happened to us??

Hii hali ukiifikiria kwa umakini unaona kabisa it goes beyond colonialism.

Walitufanya nini mpaka tuko hapa leo hii na kila juhudi ya kunyanyuka tena inapotea kila ikichipua?
 
Nakumbuka wakati nipo ugaibuni nilikuwa nalala almost kama masaa matatu tu basi out of 24 hours.

I remember nilikuwa naweza kuingiza hela ya kibongo by then like 4 million Tsh na hapo nimeshakatwa Kodi Yao 36%.
Yaani unapiga box huku unasoma. Kuna muda unajiuliza hivi nimekuja huku kusoma au kupiga box?

Namshukuru Mungu niliyofanya kwa umri wangu nisingeweza kufanya hata kama after retirement still nisingekuwa na uwezo kufanya.
Tukipata fursa ya kwenda ugaibuni Ili ufanikiwe inatakiwa ujitume na kuwekwa show off pembeni.
Kwa Sasa nawinda Green Card ya Mmarekani ili nikapotelee huko and I will come back after achieving my goal!
Tuendelee kupambana na maisha na kupunguza kuhonga hawa kausha damu wasio na shukrani
Dah nilitaka nilale muda huu, ila kwa hii comment imenipa challenge.. ngoja niendelee kukomaa ase.
 
Nakubali wao wanafanya kazi sana kwasababu hizo kazi pia wanazo. Hapa kwetu kazi hakuna tufanye nini?Watu wengi kila mahala unapopita masaa yote kwasababu kazi hakuna.

Mtuletee kazi tutafanya, Msituambie twende kulima, wengine tumezaliwa mijini hatujawahi kulima na hatuna mashamba.
 
Yaani tusijidanganye hata siku moja.

Watu weusi tunajisemaga tuko na maguvu etc..

Ila kwa jinsi hawa wenzetu ngozi nyeupe wanavyopiga kazi speed yao kama umekaa kibwegebwege utakuwa unalia kila siku

Hawa jamaa ni nuksi jamani, yaani huku kufanya kazi saa 12 + ni jambo la kawaida sana.

Halafu wako speed kama legelege lazima utapike dagaa.

Watu weusi tuko polepole sana hata kazi nchini kwetu infact ukisema u rate kwenye scale ya 10
Hawa wenzetu wako 9/10 sis tuko 1/10

Yaani hakuna kitu wakuu, nadhani hii ndio siri kubwa ya wao kutupiga gap la maana achana na kelele za ohh walikuja kuiba malighafi Afrika hizo ni kelele za kujitetea tu hawa jamaa ni watafutaji yaani wana ile spirit ya kichaga na kikinga mara 100

Ni hayo tu wadau, tupambane. sana

Na haijalishi ni me au ke hawa watu ni hatari na wanaanza michakato wadogo kabisa yaani 18yrs mtu anapiga kazi
Uko sahihi mia mia
Halafu wanajali sana muda na pia kwenye kazi na huduma ni wa KWELI hawana ubabaishaji.
 
Sasa huku kwetu watu kama TID na Ray kigosi kwa umri wao bado wanaishi na kula kwao,what do you expect?
 
Nakubali wao wanafanya kazi sana kwasababu hizo kazi pia wanazo. Hapa kwetu kazi hakuna tufanye nini?Watu wengi kila mahala unapopita masaa yote kwasababu kazi hakuna.

Mtuletee kazi tutafanya, Msituambie twende kulima, wengine tumezaliwa mijini hatujawahi kulima na hatuna mashamba.
Kazi zipo nyingi tu,ajira ndio hakuna
 
Back
Top Bottom