Mnavyopenda matusi sasa. Hamuwezi kupangua hoja kabisa.Watu wenye Degree Nne ndio huleta uzi kama ulioleta wewe.Halafu ukiambiwa unakwepa kwepa ukweli wako juu ya chuki mbaya kabisa uliyo nayo rohoni.Imekuuma sana Tyson kuwa overrated.
Jitahidi na wewe uzidi pia kuwa Overrated ni kazi nyepesi sana.
Hahaha bob mbona umeshikilia swala la kurudiana hivi unajua tumeanza wapi hadi kufika hapo?wewe ndo usome vizuri anzisha mapambano yako ya mabondia wanaorudia mpambano nakupigana tena ndo uapprove ubondia wao...baada ya kuwa....under rate
Kwa jibu kama hili, naomba niishie hapa kufuatilia uzi wako.Yupo hapo kwa ajili ya records. Je ni anastahili? Kama unafuatlia mpira, Zidane akisemwa ni kocha bora zaidi ya Wenger kwakua ana UEFA itakuingia akilini?
Evander alimpiga vichwa Tyson huyo mtoe, Lennox Lewis ndio mkali, Tyson kawapiga Riddick Bowe, Frank Bruno, Oliver McCall, etcTukisema bondia ni mzuri ni kwakua amepambana na mabondia karibia wote wa kizazi chake na amewapiga.
Mfano Muhammad Ali, bondia aliyeogopwa mno Sonny Liston alikaa kwa Ali. Kama hujui ukali na ubabe wa Liston ni kwamba msemaji wa Patterson aliulizwa kama wataufuata mkanda kwa Liston akajibu "Huyo hatutaki hata kukutana naye, ikitokea akawa anakuja njia yetu na njia yenyewe tutabadilish
Holmes, Spinks na Berbick waliopigwa na Tyson ni kizazi cha Muhammad Ali, alipokutana na kizazi chake wakina Evander ndiyo vile vipigo tulivyoviona.
Kama kati yenu kuna anayeweza kutaja mabondia wakubwa watatu wa kizazi cha Tyson na aliwapiga awataje.
Kwani ile gemu ya Evander vs Tyson iliisha ? Ile gemu kairibu kwa kumpiga vichwa Tyson mpaka akampasua juu ya jicho, Tyson naye akaamua kumng'ata, hivyo pambano kuvunjikaMike Tyson being "evandered" by Evander Hollyfield. Tatizo kubwa la Tyson ni kwamba alikuwa amezoea mapambano ya kuwapiga watu raundi ya 1 au ya 2, mwisho na hakuwa na pumzi ya kupigana zaidi ya raundi hizo. Hii ilimaanisha kuwa hakuwa na pumzi pamoja na uzoefu wa kupigana zaidi ya ya 1 au ya 2, sana sana ya tatu. Mimi siku ya pambano lao la kwanza nilipomuona Evander niliwaambia watu pale pale kuwa LEO TYSON ANAPIGWA.
Sababu kubwa iliyonifanya niseme hivyo ni kuwa figure ya Hollyfield ilikuwa inaonyesha ni mtu ambaye ni wa kupigwa kuanzia round ya 8 au zaidi na si vinginevyo, round ambazo Tyson hakuwa na uwezo nazo. Yeye alikuwa na uwezo wa raundi ya 1 na ya pili tu! Ni kweli kabisa Tyson alikuwa anakuwa over-rated, tena sana!
Sawa ila kama unataka burudani ulingoni kwa Tyson ulikua unapotea kamcheki Dwight Muhammadi Qawi, Sugar Ray, Muhammad Ali, Chris Eubank (Baba), Chris Eubank jr (mtoto) na Drunken master.
Utaenjoy mno.
[/QUO hao karibu wote nimewaona kasoro huyo chriss eubank mtoto, kwa kuwa siku hizi siangalia ngumi , eubank mkubwa alikuwa na mbwembwe nyingi ulingoni pamoja na maringo, binafsi mabondia wangu bora M.Alli , lennox lewis , iron tyson
Eubank nilikuwa nampenda zile mbwembwe zake, anakupiga then anageua huyo, ila nassikia jamaa amefirisikaKuna pambano la Eubank Sr na Big Bad Ben kabla ya pambano Eubank akawa anahojiwa akasema "...yeyote aliyeweka dau kunipinga ajue anakosea, haijalishi kama nitashindwa ila atakua amekosea" hapo yeye ni underdog na Ben ni fan favourite.
Kilichotokea bwana Ben na ngumi akastaafu
Castr, Mkuu mchezo wa ngumi pesa zaidi, ya nini kila siku upigane na mtu huna uhakika, wilder na joshua wanakimbiana, mayweathe na man pac walikuwa wanakwepana kwepana.
Awe overrated ama lah!!
Kikubwa mie namuona bondia wa kiwango cha juu, kwa burudani alizokuwa ananipa ulingoni, jinsi anavyoshambulia, kujilinda, wepesi wake burudani ya boxing ilikiwa inapatikana kwake.
Mike Tyson being "evandered" by Evander Hollyfield. Tatizo kubwa la Tyson ni kwamba alikuwa amezoea mapambano ya kuwapiga watu raundi ya 1 au ya 2, mwisho na hakuwa na pumzi ya kupigana zaidi ya raundi hizo. Hii ilimaanisha kuwa hakuwa na pumzi pamoja na uzoefu wa kupigana zaidi ya ya 1 au ya 2, sana sana ya tatu. Mimi siku ya pambano lao la kwanza nilipomuona Evander niliwaambia watu pale pale kuwa LEO TYSON ANAPIGWA.
Sababu kubwa iliyonifanya niseme hivyo ni kuwa figure ya Hollyfield ilikuwa inaonyesha ni mtu ambaye ni wa kupigwa kuanzia round ya 8 au zaidi na si vinginevyo, round ambazo Tyson hakuwa na uwezo nazo. Yeye alikuwa na uwezo wa raundi ya 1 na ya pili tu! Ni kweli kabisa Tyson alikuwa anakuwa over-rated, tena sana!
Nilitaka ujue kuwa nimekushangaa sana kwa kitendo chako cha kubishia world records.Kausha, ungeweza kuishia bila kuandika
Hebu lete hiyo sehemu ambayo mimi nimetafsiri.Umeamua Kugoogle ukatafsiri kwa Kiswahili then unajitapa kuwa umejenga hoja?
Bahati mbaya mimi si mshabiki wa Ndondi lakini hoja zako ni dhaifu mno.
Umeenda kusoma Makala za Haters na ukazibandika hapa.
Sikia mzee, hizi stori za world records ndiyo zikasababisha nimtaje Zidane na makombe ya UEFA wewe ukaingilia kati huku hujui ilikuaje.Nilitaka ujue kuwa nimekushangaa sana kwa kitendo chako cha kubishia world records.
Naomba nisiseme zaidi.