Hii Point Nyepesi sana, nilichogundua wewe ni MTU wa ngumi, yaani mchezo unaujua hasa kwa maana uko detailed, mpaka kuanza kukuelewesha vitu ambavyo najua unajua aibu naona mimi,kinachonishangaza ni vile umeamua kushupaza shingo na kuanza kuongea kishabiki
Hivi wewe hujui kuwa ili kuwa bingwa kwa Mara ya kwanza huo mkanda unamnyang'anya bingwa??hivi wewe hujui kuwa mkanda huwa unautetea against highest ranking boxers wa wakati huo? Nakuomba uwe na heshima kwa mabondia waliopigwa na Tyson, ndio walikuwa bora kwa nyakati hizo mkuu.
Tyson Kachukua Ubingwa toka kwa Bingwa Berbick unawezaje kumu underrate Berbick kwa vihoja vyako dhaifu? Tyson Kamkalisha Frank Bruno, unamjua Frank Bruno wa Nyakati Hizo? Tyson kamkalisha
Unamjua Donovan Ruddock wa nyakati za Tyson aliyechapwa Mara 2 mfululizo? angepangiwa na nani nyakati hizo kama Ruddock?
Larry Holmes, Tony Tucker, Michael Spinks,Tony Tubbs na Tyrell Biggs ni majina makubwa ya Nyakati zake ulitaka apambane na kina nani nyakati zile??kuwa na heshima kwa hao mabondia, unadhani umemponda Tyson ila kwa sisi werevu tunaona umewakosea heshima mabondia waliopambana na Tyson
Zaidi katika mapambano ya Tyson utagundua ameanza kupoteza jioni sana mengi akipoteza baada ya kutoka Jela.Tyson ktk Ubora wake alipigwa Na Douglas Buster tu katika usiku wa Mshangazo kwa Dunia.
MPE Heshima anayostahili Tyson