Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Cus D'Amato alimuokota Tyson mtaani, aliona ubabe, aliona sharpness, aliona njaa, aliona vingi lakini cha muhimu zaidi ni aliona 'eye of the tiger'.

Akamchukua Tyson, akam-train, akapambana, kwa ubabe wa Tyson ulingoni akapachikwa jina la Kid Dynamite, kisha Iron halafu likaja Baddest man on the planet.

Ni kweli alistahili?

Ninasema hapana. Na hili ni jibu la wote ambao reference yao ya bondia mzuri ni Tyson.

Tyson alibebwa na journeymen, alibebwa na vikongwe, alibebwa na media, akabebwa na promoters ndiyo akafanikiwa kumilikia hizo nicknames tatu.

George Foreman baada ya kupigwa na Jimmy Young (Nalipenda hili pambano sichoki kuangalia) na kuokoka palepale ukumbini alistaafu na kuwa mchungaji. Baada ya kurudi tena ulingoni ndiyo zikawa enzi za Tyson zimepamba moto.

Sasa siku hiyo Tyson akiwa anahojiwa akaulizwa "Unafikiria kupambana na Foreman?" Akajifanya hajasikia swali, akaelezea swala jingine alipomaliza yule mwandishi akarudia tena "Unafikiria kupambana na Foreman?" Tyson akang'aka "KWANI NI LAZIMA NIPAMBANE NAE? NENDA KAPAMBANE NAYE WEWE BASI"

Huyo ndiye Tyson sasa. Muoga na anayeogopa kusimama ulingoni na bondia aliyekamilika.

Wanaomtetea wanakwambia alichukua ubingwa akiwa mtoto. Rekodi ambayo hakuna aliyeiweka, it's true. Alichukua ubingwa kutoka kwa Trevor Berbick mwaka 1986, Trevor Berbick alichukua ubingwa kutoka kwa Pinklon Thomas mwaka 1986 huo huo.

So Trevor Berbick ametoka kupambana na Pinklon Thomas, mkali wa left jab, pambano la raundi 12 na ushindi wake aliupata kwa uamuzi wa majaji, means alizunguka raundi zote 12 bila kuacha hata moja.

Na unataka jua kivipi pambano lilikua gumu? Hakuna aliyeanguka kwenye hili pambano mpaka Berbick anatangazwa bingwa.

So mtu wa miaka 32 ametoka kupigana pambano la heavyweight la raundi 12 unampa kijana wa miaka 22 ili apigane naye kutetea ubingwa. Unategemea nini? Ndiyo nikasema mapromoter pia wanambeba.

Tafuta siku hizi ni heavyweight gani anaingia ulingoni zaidi ya mara mbili tena kwa mapambano ya umuhimu. So Berbick risked it, iwe ni madeni au vitisho vya promoter hatujui, ila ni alipanda ulingoni kumpa ushindi Tyson.

Ok akampiga Michael Spinks (ndugu wa Leon) bondia aliyekua anatafuta pambano moja tu limstaafishe akiwa tajiri, akalipata baada ya pale na ngumi akaacha. This was not a completed boxer.

Akaenda kumpiga Holmes, again, babu mwingine alikutana na bahati mbaya ya kijana ulingoni.

So promoter na kocha wake wakawa wanavizia 'has been' na journeymen ili kuikuza rekodi ya Tyson, wakisaidiana na media.

And then 'has been' na journeymen wakaisha ikabidi apambane na mabondia wakali wa kizazi chake.

Alipigwa na kila bondia. Alipigwa na Evander akang'ata (kuliko kupigana ukang'ata sa si bora ukimbie - Chid Benz) alipigwa na Lenox Lewis,

Yeye na mapromota wake wakajichanganya wakamchagua Douglas Buster kama stepping stone kwa Tyson. Douglas akamchapa huyu bwana kwa KO raundi ya kumi. Ikawa aibu. Unajiita Iron mara Baddest how do you lose to underdog? You lose kwakua promoter hakutoa maelekezo kwa Douglas kua inabidi ashindwe so hata journeyman akimkazia Tyson, Iron linakua plastiki.

Anyway akaanza safari ya kutaka kurudisha mkanda toka kwa Douglas, bwana Douglas akaenda kuuacha mkanda kwa Evander, Tyson akapangiwa apigane na Evander ili arudishe mkanda wake. Bwana Tyson akaona isiwe kesi akalikimbia pambano.

Manina, akadai ati amepata jeraha la mbavu hivyo hawezi kuingia ulingoni na Evander. Plan yao ni atokee bondia mlaini amkalishe Evander kisha wao ndiyo wamkurupukie huyo bondia mlaini.

Akajichanganya akamvagaa Evander hivyo hivyo, kufika raundi ya 11 Tyson akabutuliwa kwa KO. Akajifanya anataka kurudiana naye, walivyorudiana akaona balaa limezidi akamng'ata Evander.

Akajichanganya akaenda kwa Lennox Lewis. Huyu anaye akamtoboa toboa Tyson hadi aibu.

Huyu sasa ndiyo Tyson. Ambaye watu wanamsifia huku hawajui kua jamaa alikua ni mwoga, mtegemea journeymen kama stepping stone na media.

Overrated nigga

Update:

Kuna watu wanadai sasa kwanini apigane na Foreman wakati Foreman alishajichokea. Lakini mbona hawajiulizi inakuwaje mtu huyu huyu akapigana na Holmes na Berbick ambao ni watu wa kizazi cha Foreman?

Wanadai eti anajulikana dunia nzima. Nimewajibu mbona uzi una majibu ya kwanini anajulikana? Si nimeandika Media zilitengeneza hype au?

Wanasema ni mkali yupo top 5 ya greatest heavyweight boxers. Ni kweli ila hiyo ni kwakua amepelekwa pale na rekodi ambazo kazivuna kwa journeymen na has been.

Yaani watu wanajenga hoja ambazo tayari uzi umejibu. Kwa mwingine anayetaka kujenga hoja tafadhali aangalie kama uzi umeshajibu swala analotaka kuleta.

Update 2:

Mpaka saa hii hakuna ambaye ameweza kupangua hoja za huu uzi. Wengi wametukana au kusema tu walienjoy kumuangalia Tyson.

Bado hakuna aliyeijibu challenge hii - atajwe bondia ambaye alikua wa moto na Tyson wa moto kisha walipokutana Tyson akashinda.

Kuna mtu katoa hoja kua kupigwa kupo ndiyo maana Ali alipigwa pia. Nikajibu ni kweli ila mtaje bondia ambaye alimpiga Ali halafu walivyorudiana akampiga tena Ali. Kisha atajwe bondia aliyempiga Tyson na walivyorudiana Tyson akampiga huyo bondia.
Waweza kuwa sawa, kuna ka story fulani kuhusu "Iron Mike" kudundwa akiwa jela, sijajuwa kama kana ukweli...

Hichi kitu,hata Mimi nilikiona,evander aliluwa mtu kumshika iron muda wote,real fighter alikuwa Tyson baba
Mi nakubaliana na wewe wala sibishi, ila kama dunia nzima wamemkubali Tyson alikuwa mwamba wewe mla mihogo ya kukaanga ukagundua ni overrated unastahili kabisa kupewa uprofesa. Kuhusu pambano la Evenderhollyfield nadhani benchi la ufundi lilifanya kazi ya ziada kugundua udhaifu wa Mike. Ukiangalia kuanzia raundi ya kwanza hadi ya sita Evander hakuwa anapigana, alichokifanya ni kumkumbatia tu Tyson. Hii stahili ya kumkumbatia ilimtia hasira Tyson na kumuongezea muda wa mapigani. Kama Evender angekuwa anapiga toka round ya kwanza bila kukumbatia kumbatia hati raundi ya pili asingefika.
 
Castr,

Ungejifunza kuwa analytical zaidi kuliko kuweka records ambazo hazijachakatwa vizuri, Tyson msikie tu ukiwa huko huko uliko ila kwa waliokutana nae ulingoni wanatoaga ushuhuda mpaka nyumba za ibada. Ila tunaheshimu uhuru wa kutoa mawazo.
 
Mkuu naomba unipe jina la kitabu na picha yke utojari...
IMG_20191126_065532.jpg
 
Ungejifunza kuwa analytical zaidi kuliko kuweka records ambazo hazijachakatwa vizuri, Tyson msikie tu ukiwa huko huko uliko ila kwa waliokutana nae ulingoni wanatoaga ushuhuda mpaka nyumba za ibada. Ila tunaheshimu uhuru wa kutoa mawazo.
Ushuhuda wa nani na nani?

Onyesha rekodi yoyote unayoona 'haijachakatwa vizuri' na nimeaiandika hapo
 
Jamaa kachambua vizuri,ukiangalia ni kweli kuwa ni nani Tyson alirudiana na alimpiga awali na kushinda kama ilivyo kwa Muhammad Ali? Kasoro pambano lake la mwisho na Larry Homes.
Castr, Hujui unchokiandika juu ya Mike Tyson wewe.
 
Kwa jinsi tu nilivyoona mapambano machache ya Tyson mlima Mjani maarufu kwa sasa.
Na vile alipigwa na ndugu zetu wale miaka hii ya Tisini mwishoni na 2000s😁😁😁

Hakuna pambano lolote la ndondi liliniamsha usiku na kukesha zaidi ya huyo Bwana..

Vyovyote tutakavyoonesha chuki na comments za ajabu ajabu juu yake...
Kijana wa watu alijitahidi sana na alibebeka sana pale alipobebwa...sisi tuendelee na chambuzi zetu za kuhusu past events kama zinafaida zizidi kutuongezea mabondia hapa Bongo😀😀😀😀😀😀😀

Mtoa mada toa na wewe kijana wako awe overrated abebwe na media kama unaoa rahisi kihivyo...
Tupunguze chuki waafrika ndio maana hatupigi hatua....
Wazungu wakiamua kubebana mnakuja tena kulia lia humu ...oooh..eee kwanini wao tu.
Walimbeba Tyson ona sasa mambo yetu..eee oooh....

Genk wamembeba Samata duuh sikia comments zetu na roho pana tulizo nazo juu yake.

Uzeeni msije kulia lia mkisikia watoto wenu wakisemwa vibaya maana chimbuko la chuki na wivu usio na maana.

Ndio maana watabaki kina Ronadinho,Zidane (Alijiamulia akimbile France huko)...Ronaldo na Messi na woote weupe kwa vijiroho kama hivyo.

1574752766269.png

Kula maisha bro..kuna watu huku wanajadili ulivyobebwa.Wanaumia kweli mioyo yao..wanatamani hata turudi nyuma uporwe mafanikio yako.

Ndio maana tunakufa mapema ngozi nyeusi mambo kama hayo.
 
Mkuu, sijasema naandika kitabu. Nina kitabu nilichonunua.
Baada ya Cassius Clay, ndiyo Tyson. Na kabla ya Clay walikuwepo akina Sunny Liston na wengine.
Unamfahamu Jack Johnson? Enzi zao walikuwa wanapigana mpaka raundi 45 nje (bila kiyoyozi) kwenye nyuzi joto 38C.
 
Kwa jinsi tu nilivyoona mapambano machache ya Tyson mlima Mjani maarufu kwa sasa.
Na vile alipigwa na ndugu zetu wale miaka hii ya Tisini mwishoni na 2000s😁😁😁

Hakuna pambano lolote la ndondi liliniamsha usiku na kukesha zaidi ya huyo Bwana..

Vyovyote tutakavyoonesha chuki na comments za ajabu ajabu juu yake...
Kijana wa watu alijitahidi sana na alibebeka sana pale alipobebwa...sisi tuendelee na chambuzi zetu za kuhusu past events kama zinafaida zizidi kutuongezea mabondia hapa Bongo😀😀😀😀😀😀😀

Mtoa mada toa na wewe kijana wako awe overrated abebwe na media kama unaoa rahisi kihivyo...
Tupunguze chuki waafrika ndio maana hatupigi hatua....
Wazungu wakiamua kubebana mnakuja tena kulia lia humu ...oooh..eee kwanini wao tu.
Walimbeba Tyson ona sasa mambo yetu..eee oooh....

Genk wamembeba Samata duuh sikia comments zetu na roho pana tulizo nazo juu yake.

Uzeeni msije kulia lia mkisikia watoto wenu wakisemwa vibaya maana chimbuko la chuki na wivu usio na maana.

Ndio maana watabaki kina Ronadinho,Zidane (Alijiamulia akimbile France huko)...Ronaldo na Messi na woote weupe kwa vijiroho kama hivyo.
View attachment 1272962

Kula maisha bro..kuna watu huku wanajadili ulivyobebwa.Wanaumia kweli mioyo yao..wanatamani hata turudi nyuma upolwe mafanikio yako.
Ndio maana tunakufa mapema ngozi nyeusi mambo kama hayo...
Hii mipasho unayoandika hapa unadhani ndiyo itapindua ukweli?
 
Wakina Holmes ni kizazi cha Ali, kwanini Tyson hakuwahi kumface Ali? Holmes ni kizazi cha Foreman kwanini Tyson hakumface Foreman?
Screenshot_2019-11-26 george foreman on mike tyson - Google Search.png

Muhammad Ali mwenyewe aliwahi kusema ,"I'm scared of him" kwenye Arsenio show (1990).
 
Hii mipasho unayoandika hapa unadhani ndiyo itapindua ukweli?
Soma vizuri ulichoandika..ni mpasho wa kukwepa kwepa uhalisia wa Tyson..uliobebwa na ukweli ambao wewe unahisi ni ukweli kwa mtazamo wako.Ndio maana umehisi nilichoandika ni mipasho.
 
Unamfahamu Jack Johnson? Enzi zao walikuwa wanapigana mpaka raundi 45 nje (bila kiyoyozi) kwenye nyuzi joto 38C.
Ulivyoandika juu ya Jack Johnson nikadhani unajua boxing angalau historia.

Ali alipigana na Liston.

Tuanze na Liston.

Unajua ni mabondia wangapi wamemkwepa huyu jamaa? Ali akiwa anatokea kifungoni anapambana arudishe heshima anakuta mkanda upo kwa Liston na hakuna heavyweight aliyetaka kumface Liston, Ali akaufuata mkanda kwa Liston akauchukua.

Tuje kwa Tyson.

Ni mabondia wangapi wamemkwepa Tyson? Ni lini umewahi sikia eti mtu kaogopa kuufuata mkanda kwa Tyson?

So mtu aliyemface Liston, mara mbili na akampiga mara zote kwa KO, akisema anamuogopa Tyson, utachukulia serious?

Na wewe uwe serious siku nyingine.
 
Soma vizuri ulichoandika..ni mpasho wa kukwepa kwepa uhalisia wa Tyson..uliobebwa na ukweli ambao wewe unahisi ni ukweli kwa mtazamo wako.Ndio maana umehisi nilichoandika ni mipasho.
Pinga nilichoandika.

Sema kua Berbick hakutoka kupigana na Pink, na hakua na umri huo. Taja mabondia niliosema ni journeymen na prove kua sio journeymen.

Taja bondia aliyewahi mpiga Tyson kisha walivyorudiana Tyson akalipa kisasi.
 
Ulivyoandika juu ya Jack Johnson nikadhani unajua boxing angalau historia.

Ali alipigana na Liston.

Tuanze na Liston.

Unajua ni mabondia wangapi wamemkwepa huyu jamaa? Ali akiwa anatokea kifungoni anapambana arudishe heshima anakuta mkanda upo kwa Liston na hakuna heavyweight aliyetaka kumface Liston, Ali akaufuata mkanda kwa Liston akauchukua.

Tuje kwa Tyson.

Ni mabondia wangapi wamemkwepa Tyson? Ni lini umewahi sikia eti mtu kaogopa kuufuata mkanda kwa Tyson?

So mtu aliyemface Liston, mara mbili na akampiga mara zote kwa KO, akisema anamuogopa Tyson, utachukulia serious?

Na wewe uwe serious siku nyingine.
Sasa unabishana na Ali mwenyewe? kumbuka hayo aliyasema wakati wa "prime" ya Tyson wakati rekodi yake ilikuwa safi.
 
Back
Top Bottom