Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Mi mwenyewe huwa nasikiasikia tu ooh tyson hivi mara tyson vile.. lakini nikiangalia clip zake naona ushubwada tu
Media ndiyo zilimpa title hapa mpaka saa hii hakuna anayepinga kwa hoja huu uzi.
 
Pambano kua nje ya Marekani siyo jambo la ajabu. Huyu Ali na Foreman hawakwenda Congo kwa kupenda, Ali leseni yake ilizuiwa Marekani na mdhamini wa kutoa pesa nyingi alikua ni Kuku Ngbendu wa Zabanga, raisi wa Zaire.

Power shifted tangu Don King atokee kwenye boxing, its why nakwambia Tyson kila kitu alishakikuta.
 
Kwani tofauti kubwa ya umri iliyopo kati ya Evender na Frank bruno ni ipi?.Vip kuhusu Bruce seldon.Unataka kusema watu waliopishana miaka 7 hawawezi kua rika kwenye ushindani.Kinachomtofautisha Tyson na hao wengine vi vipindi vyakuanza kucheza ngumi ila swala la umri sijui kizazi kuna tofauti ndogo sana kati ya hao mabondia.Mapambano ya Tyson na Kina Evender yamekuja badae sana ambako kimsingi wote walikua wanaelekea ukingoni mwa uwezo wao laiti wangekutana bado vijana tungekua na jambo zuri zaidi lakusimulia kwasababu ata Evender au Lewis wamepigana na mabondia wengi tu wamarika tofauti tofauti hadi kufika juu.Kwaiyo point yako haina mashiko.
 
Mkuu mbona hueleweki, yani mtu anakalisha mtu kwa KO raundi ya pili alafu unasema alikua overrated? Uko serious kweli?
 

Jibu lako liko hapa...

 
Nakazia, alichokinya Tyson hakuna atakae kuja kukifanya leo wala kesho... Tyson hapigan ..hayuko ulingon miaka tu.. Ila bado ana jina kuliko hao AJ na huyo mwenzie.. Ukitoka nje ya watu wanaofuatilia masumbwi.....hakuna mtu atakutajia wala anaejua kuna mtu anaitwa AJ.. ila Tyson wanajua kuna huyu kiumbe anewah kuwepo.
 
Umeandika mambo mengi kinachokucost ni ujuaji.
Jifunze kubishana na rekodi kama hizi
Mike Tyson turns 50
Ukipata mda kaa chini soma vizuri historia ya Tyson.

 
Nasisitiza tena na tena kuwa na heshima kwa mabondia waliopigwa na Tyson, ndio waliokuwa mabondia bora nyakati hizo!!Nimekutajia list ndefu zaidi ya hao watatu uliotaka, halafu kapigana na kizazi cha nyuma yake mabondia wa 3 ulitaka apigane na mabondia wote wa kizazi kilichopita??nani awewahi kufanya hivyo!!Nakupa rejea tena, Bondia wa kizazi chake aliyempiga akiwa ktk ubora wake ni Douglas Buster tu.Evander Mwenyewe wamekutana jioni, Evander kampiga Tyson aliyekuwa frustrated si Tyson wa Ubora wake.
 
Kwa hii hoja yako ni inamaanisha media zilifaulu pia kumtangaza jamaa.

Kama nilivyoandika mwanzo.
 
Najua halikwenda kule kibiashara ni sababu ya Mobutu ambaye alilipa dau nono pengine above expectations.
 
Wilder angekua mshindi.

Kimo kinampa advantage Wilder.

Pumzi ya Wilder ni kubwa kuliko ya Tyson.

Wilder ana ngumi nzito.

Wilder ana stronger chin.
Haaaaaahaaaaa Wilder huyu niliyemuona juzi hp? anakimbia kimbia tu na km asingebahatisha ile Ko Ortiz alikuwa anashinda kwa point maana hadi raundi ya 6 ilikuwa anaongoza!
 
Sawa ila kama unataka burudani ulingoni kwa Tyson ulikua unapotea kamcheki Dwight Muhammadi Qawi, Sugar Ray, Muhammad Ali, Chris Eubank (Baba), Chris Eubank jr (mtoto) na Kung Fu master.

Utaenjoy mno.
Tatizo lako wewe kutaka unachotaka wewe ndio kiwe mbona mwenzio kaheshimu mawazo yako hajakupinga? Yeye anasema akicheki mapambano ya Mike ndio anaenjoy we unamwambia eti alikuwa anapotea akamcheki nani sijui nani!
 
Pia nataka Uniambie Alli na Tyson walipigana wakati mmoja??wakati Tyson anakuwa bingwa kwa Mara ya Kwanza kuanzia hapo Alli alikuwa bado anapigana mpaka utake wakutane??Pia Foreman mwenyewe alistaafu miaka na miaka, alirudi "usiku" kabisa akacheza mapambano machache akastaafu tena
 
Soma vizuri uelewe hpo kati kamuongelea Mayweather pia kwamba ingawa nae watu wanamlalamikia kuwa anabebwa lakini hakuwahi pigwa Tko au Ko so kuna vitu Mike alikosa ambavyo huyu dogo anavyo!
 
umeandika mambo mengi kinachokucost ni ujuaji...
Jifunze kubishana na rekodi kama hizi
Mike Tyson turns 50
Ukipata mda kaa chini soma vizuri historia ya Tyson

Wewe huwezi kuniambia mimi nikae chini eti nimsome Tyson. Kama unajihisi unamjua sana karibu twende kwa hoja.
 
Hahaha am making you go and do some googling. Au siyo? Sasa kama Foreman alirudi usiku si ilibidi awe easy target? Why didn't he go for it?

Nakupa siri. Tangu Foreman arudi kwa mara ya pili ulingoni mpaka anastaafu hakuwahi kupigwa akaanguka. Now usijiulize sana kwanini Tyson hakutaka kukutana na huyu mtu.

Unauliza kama Ali alikua kizazi cha Tyson. Safi sana je Holmes ni kizazi cha Tyson? Mbona hao alipigana nao? Holmes ni kizazi cha Ali.

Ndiyo maana nasema alipigana na mababu na has beens. Kua muelewa.
 
Castr,

Naunga mkono hoja 100%, Tyson alikuwa ni lion[emoji881] kwa mabondia wa kawaida, ila akikutana na high profile boxers alikuwa hatoboi. Kwa hawa mabondia wa zamani namkubali sana Evander, Kwanza alikuwa undisputed cruiserweight, akapanda uzito ili kuwachallenge watabe wa heavyweight na akafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Nimeangalia mapambano yao mengi na loss zao zote, nimekubali kwanini Evander alikuwa anaitwa 'Real Deal', jamaa pamoja na umbile lake kuwa dogo ukilinganisha na Heavyweights wengine ila still alikuwa anapigana toe to toe, hakuna kurudi nyuma, hakuwa mwoga kabisa. Pia hata loss zake ukiziangalia nyingi ni zile za 'close fight', yaani anakuwa outpointed, sijaona pambano ambalo amepigwa akashindwa kuendelea hadi mwisho (KO/TKO), kama lipo nirekebishwe. Kwa upande wa Tyson yeye loss zake zote ni za aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…