Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Mi mwenyewe huwa nasikiasikia tu ooh tyson hivi mara tyson vile.. lakini nikiangalia clip zake naona ushubwada tu
Media ndiyo zilimpa title hapa mpaka saa hii hakuna anayepinga kwa hoja huu uzi.
 
Kwenye issue ya kuwa biashara niligusia kuwa palikuwa na shifting ya power toka kwa boxer na technical team na kwenda kwa promoters/promotion companies. Mfano mara kadhaa kumekuwa na claims baada ya mapambano kadhaa kuwa boxer mmoja hakuwa 100% fit baada ya kuwa sustained kwny training siku kadhaa before fight but was forced to fight na hakukuwa na room ya kupostpone fight kwa sabab za cost za maandalizi.
Pia utaona bravery ya promoter wa Tyson. Huwezi peleka pambano la Mohammad Ally vs G. Foreman Congo ukapata the same profit kwa maana ya endorsement ya makampuni na gate collections.
This is why I consider Tyson (and his associates) to be a 'real shift'.
Pambano kua nje ya Marekani siyo jambo la ajabu. Huyu Ali na Foreman hawakwenda Congo kwa kupenda, Ali leseni yake ilizuiwa Marekani na mdhamini wa kutoa pesa nyingi alikua ni Kuku Ngbendu wa Zabanga, raisi wa Zaire.

Power shifted tangu Don King atokee kwenye boxing, its why nakwambia Tyson kila kitu alishakikuta.
 
Tukisema bondia ni mzuri ni kwakua amepambana na mabondia karibia wote wa kizazi chake na amewapiga.

Mfano Muhammad Ali, bondia aliyeogopwa mno Sonny Liston alikaa kwa Ali. Kama hujui ukali na ubabe wa Liston ni kwamba msemaji wa Patterson aliulizwa kama wataufuata mkanda kwa Liston akajibu "Huyo hatutaki hata kukutana naye, ikitokea akawa anakuja njia yetu na njia yenyewe tutabadilish

Holmes, Spinks na Berbick waliopigwa na Tyson ni kizazi cha Muhammad Ali, alipokutana na kizazi chake wakina Evander ndiyo vile vipigo tulivyoviona.

Kama kati yenu kuna anayeweza kutaja mabondia wakubwa watatu wa kizazi cha Tyson na aliwapiga awataje.
Kwani tofauti kubwa ya umri iliyopo kati ya Evender na Frank bruno ni ipi?.Vip kuhusu Bruce seldon.Unataka kusema watu waliopishana miaka 7 hawawezi kua rika kwenye ushindani.Kinachomtofautisha Tyson na hao wengine vi vipindi vyakuanza kucheza ngumi ila swala la umri sijui kizazi kuna tofauti ndogo sana kati ya hao mabondia.Mapambano ya Tyson na Kina Evender yamekuja badae sana ambako kimsingi wote walikua wanaelekea ukingoni mwa uwezo wao laiti wangekutana bado vijana tungekua na jambo zuri zaidi lakusimulia kwasababu ata Evender au Lewis wamepigana na mabondia wengi tu wamarika tofauti tofauti hadi kufika juu.Kwaiyo point yako haina mashiko.
 
Mike Tyson being "evandered" by Evander Hollyfield. Tatizo kubwa la Tyson ni kwamba alikuwa amezoea mapambano ya kuwapiga watu raundi ya 1 au ya 2, mwisho na hakuwa na pumzi ya kupigana zaidi ya raundi hizo. Hii ilimaanisha kuwa hakuwa na pumzi pamoja na uzoefu wa kupigana zaidi ya ya 1 au ya 2, sana sana ya tatu. Mimi siku ya pambano lao la kwanza nilipomuona Evander niliwaambia watu pale pale kuwa LEO TYSON ANAPIGWA.

Sababu kubwa iliyonifanya niseme hivyo ni kuwa figure ya Hollyfield ilikuwa inaonyesha ni mtu ambaye ni wa kupigwa kuanzia round ya 8 au zaidi na si vinginevyo, round ambazo Tyson hakuwa na uwezo nazo. Yeye alikuwa na uwezo wa raundi ya 1 na ya pili tu! Ni kweli kabisa Tyson alikuwa anakuwa over-rated, tena sana!
Mkuu mbona hueleweki, yani mtu anakalisha mtu kwa KO raundi ya pili alafu unasema alikua overrated? Uko serious kweli?
 
Kwani tofauti kubwa ya umri iliyopo kati ya Evender na Frank bruno ni ipi?.Vip kuhusu Bruce seldon.Unataka kusema watu waliopishana miaka 7 hawawezi kua rika kwenye ushindani.Kinachomtofautisha Tyson na hao wengine vi vipindi vyakuanza kucheza ngumi ila swala la umri sijui kizazi kuna tofauti ndogo sana kati ya hao mabondia.Mapambano ya Tyson na Kina Evender yamekuja badae sana ambako kimsingi wote walikua wanaelekea ukingoni mwa uwezo wao laiti wangekutana bado vijana tungekua na jambo zuri zaidi lakusimulia kwasababu ata Evender au Lewis wamepigana na mabondia wengi tu wamarika tofauti tofauti hadi kufika juu.Kwaiyo point yako haina mashiko.

Jibu lako liko hapa...

.....

Wakina Holmes ni kizazi cha Ali, kwanini Tyson hakuwahi kumface Ali? Holmes ni kizazi cha Foreman kwanini Tyson hakumface Foreman?

Hata kwa Frazier asingeweza kujipeleka.

Ndiyo maana nakwambia alitegemea kupigana na 'has been' akawa anakwepa mabondia wa kizazi chake. Ikitokea anadeal na bondia wa kizazi chake basi ujue ni journeyman.

Ndiyo maana hautapata siyo majina 3 bali hata 1 la accomplished boxer ambaye alipigana na Tyson halafu Tyson akashinda. Weak chin, protected by promoters, coach na hype ya media.
 
Mkuu sasa unaandika kitabu halafu unajikandia si utakua wa ajabu.

Haji kutokea kama Tyson?

AJ na Wilder unawajua lakini?

Alichokifanya Tyson chooote isipokua kua bingwa na miaka 22 watu walishakifanya. Na wanafanya.

Sababu ya yeye utoto kumkuta ulingo wa heavyweight ni hakupitia wenzake walipopitia mfano utakuta mabondia wengi umri huo bado wapo kwenye mashindano ya olympic au bado mapromota wanamzungusha.
Nakazia, alichokinya Tyson hakuna atakae kuja kukifanya leo wala kesho... Tyson hapigan ..hayuko ulingon miaka tu.. Ila bado ana jina kuliko hao AJ na huyo mwenzie.. Ukitoka nje ya watu wanaofuatilia masumbwi.....hakuna mtu atakutajia wala anaejua kuna mtu anaitwa AJ.. ila Tyson wanajua kuna huyu kiumbe anewah kuwepo.
 
Tukisema bondia ni mzuri ni kwakua amepambana na mabondia karibia wote wa kizazi chake na amewapiga.

Mfano Muhammad Ali, bondia aliyeogopwa mno Sonny Liston alikaa kwa Ali. Kama hujui ukali na ubabe wa Liston ni kwamba msemaji wa Patterson aliulizwa kama wataufuata mkanda kwa Liston akajibu "Huyo hatutaki hata kukutana naye, ikitokea akawa anakuja njia yetu na njia yenyewe tutabadilish

Holmes, Spinks na Berbick waliopigwa na Tyson ni kizazi cha Muhammad Ali, alipokutana na kizazi chake wakina Evander ndiyo vile vipigo tulivyoviona.

Kama kati yenu kuna anayeweza kutaja mabondia wakubwa watatu wa kizazi cha Tyson na aliwapiga awataje.
Umeandika mambo mengi kinachokucost ni ujuaji.
Jifunze kubishana na rekodi kama hizi
Mike Tyson turns 50
Ukipata mda kaa chini soma vizuri historia ya Tyson.

mike tyson.jpg
 
Angalau unajenga hoja. Hii itafanya iwe rahisi kukuelewesha.

Ukisoma uzi utaona uzi umesema Tyson alichukua mkanda toka kwa Berbick, lakini Berbick alikua ametoka kuuchukua kwa nani? Pinklon. Hii hoja yako inajibiwa na uzi pale mwanzoni tu.

Wakina Holmes ni kizazi cha Ali, kwanini Tyson hakuwahi kumface Ali? Holmes ni kizazi cha Foreman kwanini Tyson hakumface Foreman?

Hata kwa Frazier asingeweza kujipeleka.

Ndiyo maana nakwambia alitegemea kupigana na 'has been' akawa anakwepa mabondia wa kizazi chake. Ikitokea anadeal na bondia wa kizazi chake basi ujue ni journeyman.

Ndiyo maana hautapata siyo majina 3 bali hata 1 la accomplished boxer ambaye alipigana na Tyson halafu Tyson akashinda. Weak chin, protected by promoters, coach na hype ya media.
Nasisitiza tena na tena kuwa na heshima kwa mabondia waliopigwa na Tyson, ndio waliokuwa mabondia bora nyakati hizo!!Nimekutajia list ndefu zaidi ya hao watatu uliotaka, halafu kapigana na kizazi cha nyuma yake mabondia wa 3 ulitaka apigane na mabondia wote wa kizazi kilichopita??nani awewahi kufanya hivyo!!Nakupa rejea tena, Bondia wa kizazi chake aliyempiga akiwa ktk ubora wake ni Douglas Buster tu.Evander Mwenyewe wamekutana jioni, Evander kampiga Tyson aliyekuwa frustrated si Tyson wa Ubora wake.
 
Nakazia , alichokinya Tyson hakuna atakae kuja kukifanya leo wala kesho... Tyson hapigan ..hayuko ulingon miaka tu.. Ila bado ana jina kuliko hao AJ na huyo mwenzie.. Ukitoka nje ya watu wanaofuatilia masumbwi.....hakuna mtu atakutajia wala anaejua kuna mtu anaitwa AJ.. ila Tyson wanajua kuna huyu kiumbe anewah kuwepo
Kwa hii hoja yako ni inamaanisha media zilifaulu pia kumtangaza jamaa.

Kama nilivyoandika mwanzo.
 
Najua halikwenda kule kibiashara ni sababu ya Mobutu ambaye alilipa dau nono pengine above expectations.
Pambano kua nje ya Marekani siyo jambo la ajabu. Huyu Ali na Foreman hawakwenda Congo kwa kupenda, Ali leseni yake ilizuiwa Marekani na mdhamini wa kutoa pesa nyingi alikua ni Kuku Ngbendu wa Zabanga, raisi wa Zaire.

Power shifted tangu Don King atokee kwenye boxing, its why nakwambia Tyson kila kitu alishakikuta.
 
Wilder angekua mshindi.

Kimo kinampa advantage Wilder.

Pumzi ya Wilder ni kubwa kuliko ya Tyson.

Wilder ana ngumi nzito.

Wilder ana stronger chin.
Haaaaaahaaaaa Wilder huyu niliyemuona juzi hp? anakimbia kimbia tu na km asingebahatisha ile Ko Ortiz alikuwa anashinda kwa point maana hadi raundi ya 6 ilikuwa anaongoza!
 
Sawa ila kama unataka burudani ulingoni kwa Tyson ulikua unapotea kamcheki Dwight Muhammadi Qawi, Sugar Ray, Muhammad Ali, Chris Eubank (Baba), Chris Eubank jr (mtoto) na Kung Fu master.

Utaenjoy mno.
Tatizo lako wewe kutaka unachotaka wewe ndio kiwe mbona mwenzio kaheshimu mawazo yako hajakupinga? Yeye anasema akicheki mapambano ya Mike ndio anaenjoy we unamwambia eti alikuwa anapotea akamcheki nani sijui nani!
 
Angalau unajenga hoja. Hii itafanya iwe rahisi kukuelewesha.

Ukisoma uzi utaona uzi umesema Tyson alichukua mkanda toka kwa Berbick, lakini Berbick alikua ametoka kuuchukua kwa nani? Pinklon. Hii hoja yako inajibiwa na uzi pale mwanzoni tu.

Wakina Holmes ni kizazi cha Ali, kwanini Tyson hakuwahi kumface Ali? Holmes ni kizazi cha Foreman kwanini Tyson hakumface Foreman?

Hata kwa Frazier asingeweza kujipeleka.

Ndiyo maana nakwambia alitegemea kupigana na 'has been' akawa anakwepa mabondia wa kizazi chake. Ikitokea anadeal na bondia wa kizazi chake basi ujue ni journeyman.

Ndiyo maana hautapata siyo majina 3 bali hata 1 la accomplished boxer ambaye alipigana na Tyson halafu Tyson akashinda. Weak chin, protected by promoters, coach na hype ya media.
Pia nataka Uniambie Alli na Tyson walipigana wakati mmoja??wakati Tyson anakuwa bingwa kwa Mara ya Kwanza kuanzia hapo Alli alikuwa bado anapigana mpaka utake wakutane??Pia Foreman mwenyewe alistaafu miaka na miaka, alirudi "usiku" kabisa akacheza mapambano machache akastaafu tena
 
Unasema Tyson hajawahi kupigwa kwa KO/ TKO? Mbona nimeeleza kwenye uzi mapambano aliyopigwa kwa KO?

Talent was there? So are journeymen. Si yeye aliyekua na talent pekee its why Douglas proved them (him) otherwise.

Mkuu zama za boxing kua business mpaka Tyson anafika kuhama kulishamalizika. Wakina Marciano wenyewe walikua tayari wapo kwenye business. Kipindi ambacho boxing haikua business ni kipindi cha raundi 50 kwa pambano (if you didn't know now you know) na hata kipindi kile wakina Dempsey walishakua matajiri kupitia boxing.

Kusema kua walipambana ili wakapigane na Tyson hauoni unajipinga mwenyewe? Umesema kua promoters wanaamua nani apambane na nani. At the same time unasema boxers fought their way to face Tyson, kivipi sasa?
Soma vizuri uelewe hpo kati kamuongelea Mayweather pia kwamba ingawa nae watu wanamlalamikia kuwa anabebwa lakini hakuwahi pigwa Tko au Ko so kuna vitu Mike alikosa ambavyo huyu dogo anavyo!
 
umeandika mambo mengi kinachokucost ni ujuaji...
Jifunze kubishana na rekodi kama hizi
Mike Tyson turns 50
Ukipata mda kaa chini soma vizuri historia ya Tyson

Wewe huwezi kuniambia mimi nikae chini eti nimsome Tyson. Kama unajihisi unamjua sana karibu twende kwa hoja.
 
Pia nataka Uniambie Alli na Tyson walipigana wakati mmoja??wakati Tyson anakuwa bingwa kwa Mara ya Kwanza kuanzia hapo Alli alikuwa bado anapigana mpaka utake wakutane??Pia Foreman mwenyewe alistaafu miaka na miaka, alirudi "usiku" kabisa akacheza mapambano machache akastaafu tena
Hahaha am making you go and do some googling. Au siyo? Sasa kama Foreman alirudi usiku si ilibidi awe easy target? Why didn't he go for it?

Nakupa siri. Tangu Foreman arudi kwa mara ya pili ulingoni mpaka anastaafu hakuwahi kupigwa akaanguka. Now usijiulize sana kwanini Tyson hakutaka kukutana na huyu mtu.

Unauliza kama Ali alikua kizazi cha Tyson. Safi sana je Holmes ni kizazi cha Tyson? Mbona hao alipigana nao? Holmes ni kizazi cha Ali.

Ndiyo maana nasema alipigana na mababu na has beens. Kua muelewa.
 
Castr,

Naunga mkono hoja 100%, Tyson alikuwa ni lion[emoji881] kwa mabondia wa kawaida, ila akikutana na high profile boxers alikuwa hatoboi. Kwa hawa mabondia wa zamani namkubali sana Evander, Kwanza alikuwa undisputed cruiserweight, akapanda uzito ili kuwachallenge watabe wa heavyweight na akafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Nimeangalia mapambano yao mengi na loss zao zote, nimekubali kwanini Evander alikuwa anaitwa 'Real Deal', jamaa pamoja na umbile lake kuwa dogo ukilinganisha na Heavyweights wengine ila still alikuwa anapigana toe to toe, hakuna kurudi nyuma, hakuwa mwoga kabisa. Pia hata loss zake ukiziangalia nyingi ni zile za 'close fight', yaani anakuwa outpointed, sijaona pambano ambalo amepigwa akashindwa kuendelea hadi mwisho (KO/TKO), kama lipo nirekebishwe. Kwa upande wa Tyson yeye loss zake zote ni za aibu
 
Back
Top Bottom