Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Haaaaaahaaaaa Wilder huyu niliyemuona juzi hp? anakimbia kimbia tu na km asingebahatisha ile Ko Ortiz alikuwa anashinda kwa point maana hadi raundi ya 6 ilikuwa anaongoza!
Ok naona hujui boxing ngoja nikueleweshe.

Boxer mfupi akitakiwa kupambana na boxer mrefu kwakua ngumi zinakua hazifiki kutokea mbali anakua anatakiwa aingie (awe in boxer) ili aingie hapo atakutana na jabs za kumzuia asiingie so atahitaji stronger chin ili aweze kuingia na kurusha ngumi zenye madhara.

Sasa Wilder ana ngumi nzito mno (Spoiler nickname Bronze Bomber) ili uingie ni ukubali kupokea vitasa. Tyson ana weak chin so actually ili aingie ni lazima ajikute kapokea knock downs nyingi na hatimaye KO au TKO.

So mimi kusena Wilder atashinda nipo sahihi mno. Lete hoja yako ya kwanini atashinda yeye.
 
Tatizo lako wewe kutaka unachotaka wewe ndio kiwe mbona mwenzio kaheshimu mawazo yako hajakupinga? Yeye anasema akicheki mapambano ya Mike ndio anaenjoy we unamwambia eti alikuwa anapotea akamcheki nani sijui nani!
Boss mi sina cha kusema. Hata wewe kaangalie highlights za niliowataja kisha wafananishe na Tyson.
 
Kuna wadau wananipinga hapa ila hawana hoja hata kidogo.
 
Acha dharau ...

''Tyson won his first 19 professional fights by knockout, 12 of them in the first round. He won the WBC title in 1986 after stopping Trevor Berbick in the second round, and added the WBA and IBF titles after defeating James Smith and Tony Tucker in 1987. This made Tyson the first heavyweight boxer to simultaneously hold the WBA, WBC and IBF titles, and the only heavyweight to successively unify them''

Naona unajisahaulisha kuwa at the peak kabla Tyson hajapigana na hao unaowasifu kina Evandar na Lennox, alihukumiwa jela miaka 6 na kukaa gerezani miaka 3. Lennox alimkuta Tyson akiwa na miaka 35

Tyson ni miongoni mwa ma legend wa Heavyweight taka usitake na wapenda masumbwi wote tunamheshimu
 
Hahaha hapana. Hata mimi wakati naanza kujua kuhusu ubondia nilijua bondia duniani ni Tyson tu
Alikuwa na umaarufu mkubwa sana mtaani, ndio alikuwa reference ya boxing. Ila baada ya kuijua U-Tube na kuangalia mapambano ya zamani nikagundua kuna wana walikuwa wanakaza zaidi yake sema ndo hivyo 'nyota'[emoji3][emoji3]
 
Wilder naye wanamponda kwa kuwa na reassume mbovu, wanasema kati ya mabondia 43 aliopigana nao only 2 ndio credible (Tyson Fury na Ortiz)
 
Mm hadi leo nasema T aliwahi pigwa na Douglas tu hawa wapuuzi wengine wote wamemvizia keshavurugwa kwa fitna na vituko alivyofanyiwa na wenye mchezo wao!
 
Castr, Umechambua vyema, naomba nikuulize swali, unadhani Tyson kwenye ubora wake angepigana na Wilder nani angeibuka mshindi?
Kwa mtazamo wangu yeyote angeweza kumpiga mwenzake kwa KO maana wote ni 'KO artist', sasa hapo inategemea nani kaanza kupata upenyo wa kurusha KO punch (aliyemuotea mwenzake). Hilo pambano lisingeenda round nyingi ni KO vs KO
 
Hata hueleweki sasa unasema kwa Frazier asingeweza jipeleka kwani Frazier,Foreman ni kizazi chake? na angecheza nao akawashinda ungesema kapigana na vizee huyo Holyfield wako mbona alipigana na Foreman alishinda kwa point tena Foreman katoka kukaa miaka 10 nje ya ring mbona hiyo husemi? Nani asiejua michezo michafu ya Holyfield headbutts na lowblow? Mara ngapi mabondia wenzie walimlalamikia hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa? rejea pambano lake vs Rahman vs Lewis yote mawili vs Tyson pia yote mawili ushindi wake ulikuwa wa kihuni sana mbona husemi? acha chuki zako kila mmoja ana ubora na udhaifu wake ila we umeponda tu mwanzo mwisho hajatokea bondia rafu km Holyfield duniani!
 
Mi nakubaliana na wewe wala sibishi, ila kama dunia nzima wamemkubali Tyson alikuwa mwamba wewe mla mihogo ya kukaanga ukagundua ni overrated unastahili kabisa kupewa uprofesa. Kuhusu pambano la Evenderhollyfield nadhani benchi la ufundi lilifanya kazi ya ziada kugundua udhaifu wa Mike. Ukiangalia kuanzia raundi ya kwanza hadi ya sita Evander hakuwa anapigana, alichokifanya ni kumkumbatia tu Tyson. Hii stahili ya kumkumbatia ilimtia hasira Tyson na kumuongezea muda wa mapigani. Kama Evender angekuwa anapiga toka round ya kwanza bila kukumbatia kumbatia hati raundi ya pili asingefika.
 
Ni overrated kwavile kama hufatilii boxing kiundani unaweza ukazani ana rekodi ya pekee sana kushinda wenzake wa wakati huo, maana ndio jina lililopenya sana mtaani kutokana na tulivyoaminishwa na medias. Lewis na Evander wamewapiga wakali wengi wa wakati huo (wana rekodi bora zaidi) still majina yao hayakuimbwa sana kama Mike Tyson
 
Haaaaaahaaaaa huna hoja Douglas alikataa kurudiana Holyfield waliporudiana nadhani unajua kilichotokea usiniambie hujui kilichofanya T amng'ate Holyfield na kabla ya pambano Mike alimtahadharisha Real Deal "ukirudia kufanya ulichonifanyia mara ya kwanza utalipa" mbona clip zipo? na wote walishahojiwa? Usijifanye hujui michezo aliyofanyiwa Mike ili kumuangusha katika prime yake Mike hakuna mbwa yeyote wa kutia mguu
 
Haka kajamaa kana ushabiki sana yeye anamuona Mike tu Evander alipelekewa moto kishenzi na babu Foreman tena baada ya kukaa nje ya ring kwa miaka kumi hiyo hawezi sema!
 
Binafsi nafikiri kwa Tanzania huyu ni bondia maarufu kuliko wote, pengie hata kuliko wa nchini kwetu. So hatujawahi kutaka kujua upande mwingine wa Tyson
Ndiye bondia maarufu zaidi kupata kutokea duniani (kama sio Ali), ila umaarufu wake umechangiwa na kuwa overrated kupita kiasi
 
Mkuu unayo softcopy ya kitabu cha huyu mbabe walau ufanye kutuwekea hapa ikikupendeza.
 
Haaaaaahaaaaa kuna kale kaimbaji kanaitwa Nandy na kenyewe kanamjua kuna wimbo niliusikia kamuimba sasa haoni ajabu mtu km yule ambae si mfuatiliaji anamjua Tyson,Khadija kopa kawahi kumuimba wasanii kibao humuimba Mike bibi yangu juzi hp ananiambia "Usijifanye Tyson hapa" yaani mleta mada inamuuma kishenzi watu kumtukuza Mike hata saa hz pita YouTube na mitandao mingine utakuta khabari za Mike hao wengine wamestaafu wamesahaulika Mike km bado yupo ulingoni ana mvuto wa kipekee sana!
 
Mtoa mada unazungumzia zama hizi au zama zile? Zama zile kulikuwa na ngumi haswa ila sio ktk zama hizi USANII mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…