screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ok naona hujui boxing ngoja nikueleweshe.Haaaaaahaaaaa Wilder huyu niliyemuona juzi hp? anakimbia kimbia tu na km asingebahatisha ile Ko Ortiz alikuwa anashinda kwa point maana hadi raundi ya 6 ilikuwa anaongoza!
Boss mi sina cha kusema. Hata wewe kaangalie highlights za niliowataja kisha wafananishe na Tyson.Tatizo lako wewe kutaka unachotaka wewe ndio kiwe mbona mwenzio kaheshimu mawazo yako hajakupinga? Yeye anasema akicheki mapambano ya Mike ndio anaenjoy we unamwambia eti alikuwa anapotea akamcheki nani sijui nani!
Kuna wadau wananipinga hapa ila hawana hoja hata kidogo.Naunga mkono hoja 100%, Tyson alikuwa ni lion[emoji881] kwa mabondia wa kawaida, ila akikutana na high profile boxers alikuwa hatoboi. Kwa hawa mabondia wa zamani namkubali sana Evander, Kwanza alikuwa undisputed cruiserweight, akapanda uzito ili kuwachallenge watabe wa heavyweight na akafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Nimeangalia mapambano yao mengi na loss zao zote, nimekubali kwanini Evander alikuwa anaitwa 'Real Deal', jamaa pamoja na umbile lake kuwa dogo ukilinganisha na Heavyweights wengine ila still alikuwa anapigana toe to toe, hakuna kurudi nyuma, hakuwa mwoga kabisa. Pia hata loss zake ukiziangalia nyingi ni zile za 'close fight', yaani anakuwa outpointed, sijaona pambano ambalo amepigwa akashindwa kuendelea hadi mwisho (KO/TKO), kama lipo nirekebishwe. Kwa upande wa Tyson yeye loss zake zote ni za aibu
Alikuwa na umaarufu mkubwa sana mtaani, ndio alikuwa reference ya boxing. Ila baada ya kuijua U-Tube na kuangalia mapambano ya zamani nikagundua kuna wana walikuwa wanakaza zaidi yake sema ndo hivyo 'nyota'[emoji3][emoji3]Hahaha hapana. Hata mimi wakati naanza kujua kuhusu ubondia nilijua bondia duniani ni Tyson tu
Wilder naye wanamponda kwa kuwa na reassume mbovu, wanasema kati ya mabondia 43 aliopigana nao only 2 ndio credible (Tyson Fury na Ortiz)Tyson supporters mnashindwa kujenga hoja badala yake mnatetea jinsi alivyokua muoga na mkimbia watu.
Sasa kama hoja yenu ni kwamba alikua anakimbia watu kwa ajili ya pesa mbona alipigwa na Douglas? Si angekua anawapiga hawa underdogs kirahisi?
Tukiwa hapohapo kwenye kukimbia watu, nitajieni bondia ambaye Wilder amewahi kumkimbia. Nitajieni bondia ambaye Foreman amewahi kumkimbia? Au Liston.
Mm hadi leo nasema T aliwahi pigwa na Douglas tu hawa wapuuzi wengine wote wamemvizia keshavurugwa kwa fitna na vituko alivyofanyiwa na wenye mchezo wao!Hii Point Nyepesi sana, nilichogundua wewe ni MTU wa ngumi, yaani mchezo unaujua hasa kwa maana uko detailed, mpaka kuanza kukuelewesha vitu ambavyo najua unajua aibu naona mimi,kinachonishangaza ni vile umeamua kushupaza shingo na kuanza kuongea kishabiki
Hivi wewe hujui kuwa ili kuwa bingwa kwa Mara ya kwanza huo mkanda unamnyang'anya bingwa??hivi wewe hujui kuwa mkanda huwa unautetea against highest ranking boxers wa wakati huo??Nakuomba uwe na heshima kwa mabondia waliopigwa na Tyson, ndio walikuwa bora kwa nyakati hizo mkuu.
Tyson Kachukua Ubingwa toka kwa Bingwa Berbick unawezaje kumu underrate Berbick kwa vihoja vyako dhaifu?Tyson Kamkalisha Frank Bruno, unamjua Frank Bruno wa Nyakati Hizo??Tyson kamkalisha
Unamjua Donovan Ruddock wa nyakati za Tyson aliyechapwa Mara 2 mfululizo??angepangiwa na nani nyakati hizo kama Ruddock??
Larry Holmes, Tony Tucker, Michael Spinks,Tony Tubbs na Tyrell Biggs ni majina makubwa ya Nyakati zake ulitaka apambane na kina nani nyakati zile??kuwa na heshima kwa hao mabondia, unadhani umemponda Tyson ila kwa sisi werevu tunaona umewakosea heshima mabondia waliopambana na Tyson
Zaidi katika mapambano ya Tyson utagundua ameanza kupoteza jioni sana mengi akipoteza baada ya kutoka Jela.Tyson ktk Ubora wake alipigwa Na Douglas Buster tu katika usiku wa Mshangazo kwa Dunia.
MPE Heshima anayostahili Tyson
Kwa mtazamo wangu yeyote angeweza kumpiga mwenzake kwa KO maana wote ni 'KO artist', sasa hapo inategemea nani kaanza kupata upenyo wa kurusha KO punch (aliyemuotea mwenzake). Hilo pambano lisingeenda round nyingi ni KO vs KOCastr, Umechambua vyema, naomba nikuulize swali, unadhani Tyson kwenye ubora wake angepigana na Wilder nani angeibuka mshindi?
Hata hueleweki sasa unasema kwa Frazier asingeweza jipeleka kwani Frazier,Foreman ni kizazi chake? na angecheza nao akawashinda ungesema kapigana na vizee huyo Holyfield wako mbona alipigana na Foreman alishinda kwa point tena Foreman katoka kukaa miaka 10 nje ya ring mbona hiyo husemi? Nani asiejua michezo michafu ya Holyfield headbutts na lowblow? Mara ngapi mabondia wenzie walimlalamikia hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa? rejea pambano lake vs Rahman vs Lewis yote mawili vs Tyson pia yote mawili ushindi wake ulikuwa wa kihuni sana mbona husemi? acha chuki zako kila mmoja ana ubora na udhaifu wake ila we umeponda tu mwanzo mwisho hajatokea bondia rafu km Holyfield duniani!Angalau unajenga hoja. Hii itafanya iwe rahisi kukuelewesha.
Ukisoma uzi utaona uzi umesema Tyson alichukua mkanda toka kwa Berbick, lakini Berbick alikua ametoka kuuchukua kwa nani? Pinklon. Hii hoja yako inajibiwa na uzi pale mwanzoni tu.
Wakina Holmes ni kizazi cha Ali, kwanini Tyson hakuwahi kumface Ali? Holmes ni kizazi cha Foreman kwanini Tyson hakumface Foreman?
Hata kwa Frazier asingeweza kujipeleka.
Ndiyo maana nakwambia alitegemea kupigana na 'has been' akawa anakwepa mabondia wa kizazi chake. Ikitokea anadeal na bondia wa kizazi chake basi ujue ni journeyman.
Ndiyo maana hautapata siyo majina 3 bali hata 1 la accomplished boxer ambaye alipigana na Tyson halafu Tyson akashinda. Weak chin, protected by promoters, coach na hype ya media.
Ni overrated kwavile kama hufatilii boxing kiundani unaweza ukazani ana rekodi ya pekee sana kushinda wenzake wa wakati huo, maana ndio jina lililopenya sana mtaani kutokana na tulivyoaminishwa na medias. Lewis na Evander wamewapiga wakali wengi wa wakati huo (wana rekodi bora zaidi) still majina yao hayakuimbwa sana kama Mike TysonYah! Sipo kukupinga, wewe ukisema overrated ni sawa ni mawazo yako,ie sijali opponents wake, mie nasema nilikuwa naenjoy vile alivyokuwa anapigana ni moja kati ya wachezaji ndondi bora niliopata kuwatizama, kujilinda, kushambulia n.k n.k
Na ndio maana comment yangu ya kwanza sikuanza kumpinga mleta mada, alivyoongea vingine vina ukweli ndani yake, kiuchezaji kwangu alikuwa bondia bora.
Haaaaaahaaaaa huna hoja Douglas alikataa kurudiana Holyfield waliporudiana nadhani unajua kilichotokea usiniambie hujui kilichofanya T amng'ate Holyfield na kabla ya pambano Mike alimtahadharisha Real Deal "ukirudia kufanya ulichonifanyia mara ya kwanza utalipa" mbona clip zipo? na wote walishahojiwa? Usijifanye hujui michezo aliyofanyiwa Mike ili kumuangusha katika prime yake Mike hakuna mbwa yeyote wa kutia mguuHebu mtaje bondia mmoja tu ambaye alimpiga Ali halafu walivyorudiana akarudia kumpiga tena Ali.
Nenda kagoogle nakusubiri.
Kisha taja mabondia ambao walipigana na Tyson wakampiga halafu walivyorudiana Tyson akawapiga.
Mtu kuitwa Greatest si mchezo aisee.
Haka kajamaa kana ushabiki sana yeye anamuona Mike tu Evander alipelekewa moto kishenzi na babu Foreman tena baada ya kukaa nje ya ring kwa miaka kumi hiyo hawezi sema!Kwani tofauti kubwa ya umri iliyopo kati ya Evender na Frank bruno ni ipi?.Vip kuhusu Bruce seldon.Unataka kusema watu waliopishana miaka 7 hawawezi kua rika kwenye ushindani.Kinachomtofautisha Tyson na hao wengine vi vipindi vyakuanza kucheza ngumi ila swala la umri sijui kizazi kuna tofauti ndogo sana kati ya hao mabondia.Mapambano ya Tyson na Kina Evender yamekuja badae sana ambako kimsingi wote walikua wanaelekea ukingoni mwa uwezo wao laiti wangekutana bado vijana tungekua na jambo zuri zaidi lakusimulia kwasababu ata Evender au Lewis wamepigana na mabondia wengi tu wamarika tofauti tofauti hadi kufika juu.Kwaiyo point yako haina mashiko.
Ndiye bondia maarufu zaidi kupata kutokea duniani (kama sio Ali), ila umaarufu wake umechangiwa na kuwa overrated kupita kiasiBinafsi nafikiri kwa Tanzania huyu ni bondia maarufu kuliko wote, pengie hata kuliko wa nchini kwetu. So hatujawahi kutaka kujua upande mwingine wa Tyson
Mkuu unayo softcopy ya kitabu cha huyu mbabe walau ufanye kutuwekea hapa ikikupendeza.Castr,
Natamani nikuazime kitabu cha Mike Iron Tyson ili ujue ukweli.
Cus D'Amato hakumuokota Tyson mitaani. Alipelekwa kwake na mtu mwingine aliyemwona Tyson kwenye gereza la watoto na akaona talent yake.
Kwenye hicho kitabu anaeleza vizuri jinsi alivyopigwa Japan.
Kifupi kama Tyson haji kutokea kirahisi.
Haaaaaahaaaaa kuna kale kaimbaji kanaitwa Nandy na kenyewe kanamjua kuna wimbo niliusikia kamuimba sasa haoni ajabu mtu km yule ambae si mfuatiliaji anamjua Tyson,Khadija kopa kawahi kumuimba wasanii kibao humuimba Mike bibi yangu juzi hp ananiambia "Usijifanye Tyson hapa" yaani mleta mada inamuuma kishenzi watu kumtukuza Mike hata saa hz pita YouTube na mitandao mingine utakuta khabari za Mike hao wengine wamestaafu wamesahaulika Mike km bado yupo ulingoni ana mvuto wa kipekee sana!Nakazia , alichokinya Tyson hakuna atakae kuja kukifanya leo wala kesho... Tyson hapigan ..hayuko ulingon miaka tu.. Ila bado ana jina kuliko hao AJ na huyo mwenzie.. Ukitoka nje ya watu wanaofuatilia masumbwi.....hakuna mtu atakutajia wala anaejua kuna mtu anaitwa AJ.. ila Tyson wanajua kuna huyu kiumbe anewah kuwepo