Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Tyson alikuwa anabebwa, overrated

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
tyson.jpg

Cus D'Amato alimuokota Tyson mtaani, aliona ubabe, aliona sharpness, aliona njaa, aliona vingi lakini cha muhimu zaidi ni aliona 'eye of the tiger'.

Akamchukua Tyson, akam-train, akapambana, kwa ubabe wa Tyson ulingoni akapachikwa jina la Kid Dynamite, kisha Iron halafu likaja Baddest man on the planet.

Ni kweli alistahili?

Ninasema hapana. Na hili ni jibu la wote ambao reference yao ya bondia mzuri ni Tyson.

Tyson alibebwa na journeymen, alibebwa na vikongwe, alibebwa na media, akabebwa na promoters ndiyo akafanikiwa kumilikia hizo nicknames tatu.

George Foreman baada ya kupigwa na Jimmy Young (Nalipenda hili pambano sichoki kuangalia) na kuokoka palepale ukumbini alistaafu na kuwa mchungaji. Baada ya kurudi tena ulingoni ndiyo zikawa enzi za Tyson zimepamba moto.

Sasa siku hiyo Tyson akiwa anahojiwa akaulizwa "Unafikiria kupambana na Foreman?" Akajifanya hajasikia swali, akaelezea swala jingine alipomaliza yule mwandishi akarudia tena "Unafikiria kupambana na Foreman?" Tyson akang'aka "Kwani ni lazima nipambane nae? Nenda kapambane naye wewe basi!"

Huyo ndiye Tyson sasa. Muoga na anayeogopa kusimama ulingoni na bondia aliyekamilika.

Wanaomtetea wanakwambia alichukua ubingwa akiwa mtoto. Rekodi ambayo hakuna aliyeiweka, it's true. Alichukua ubingwa kutoka kwa Trevor Berbick mwaka 1986, Trevor Berbick alichukua ubingwa kutoka kwa Pinklon Thomas mwaka 1986 huo huo.

So Trevor Berbick ametoka kupambana na Pinklon Thomas, mkali wa left jab, pambano la raundi 12 na ushindi wake aliupata kwa uamuzi wa majaji, means alizunguka raundi zote 12 bila kuacha hata moja.

Na unataka jua kivipi pambano lilikua gumu? Hakuna aliyeanguka kwenye hili pambano mpaka Berbick anatangazwa bingwa.

So, mtu wa miaka 32 ametoka kupigana pambano la heavyweight la raundi 12 unampa kijana wa miaka 22 ili apigane naye kutetea ubingwa. Unategemea nini? Ndiyo nikasema mapromoter pia wanambeba.

Tafuta siku hizi ni heavyweight gani anaingia ulingoni zaidi ya mara mbili tena kwa mapambano ya umuhimu. So Berbick risked it, iwe ni madeni au vitisho vya promoter hatujui, ila ni alipanda ulingoni kumpa ushindi Tyson.

Ok akampiga Michael Spinks (ndugu wa Leon) bondia aliyekua anatafuta pambano moja tu limstaafishe akiwa tajiri, akalipata baada ya pale na ngumi akaacha. This was not a completed boxer.

Akaenda kumpiga Holmes, again, babu mwingine alikutana na bahati mbaya ya kijana ulingoni.

So promoter na kocha wake wakawa wanavizia 'has been' na journeymen ili kuikuza rekodi ya Tyson, wakisaidiana na media.

And then 'has been' na journeymen wakaisha ikabidi apambane na mabondia wakali wa kizazi chake.

Alipigwa na kila bondia. Alipigwa na Evander akang'ata (kuliko kupigana ukang'ata sa si bora ukimbie - Chid Benz) alipigwa na Lenox Lewis.

Yeye na mapromota wake wakajichanganya wakamchagua Douglas Buster kama stepping stone kwa Tyson. Douglas akamchapa huyu bwana kwa KO raundi ya kumi. Ikawa aibu. Unajiita 'Iron' mara 'Baddest' how do you lose to underdog? You lose kwakua promoter hakutoa maelekezo kwa Douglas kua inabidi ashindwe so hata journeyman akimkazia Tyson, Iron linakua plastiki.

Anyway akaanza safari ya kutaka kurudisha mkanda toka kwa Douglas, Bwana Douglas akaenda kuuacha mkanda kwa Evander, Tyson akapangiwa apigane na Evander ili arudishe mkanda wake. Bwana Tyson akaona isiwe kesi akalikimbia pambano.

Tyson akadai ati amepata jeraha la mbavu hivyo hawezi kuingia ulingoni na Evander. Plan yao ni atokee bondia mlaini amkalishe Evander kisha wao ndiyo wamkurupukie huyo bondia mlaini.

Akajichanganya akamvagaa Evander hivyohivyo, kufika raundi ya 11, Tyson akabutuliwa kwa KO. Akajifanya anataka kurudiana naye, walivyorudiana akaona balaa limezidi akamng'ata Evander.

Akajichanganya akaenda kwa Lennox Lewis. Huyu anaye akamtoboa toboa Tyson hadi aibu.

Huyu sasa ndiyo Tyson. Ambaye watu wanamsifia huku hawajui kuwa jamaa alikuwa ni mwoga, mtegemea journeymen kama stepping stone na media.

Overrated nigga

Update:

Kuna watu wanadai sasa kwanini apigane na Foreman wakati Foreman alishajichokea. Lakini mbona hawajiulizi inakuwaje mtu huyu huyu akapigana na Holmes na Berbick ambao ni watu wa kizazi cha Foreman?

Wanadai eti anajulikana dunia nzima. Nimewajibu mbona uzi una majibu ya kwanini anajulikana? Si nimeandika Media zilitengeneza hype au?

Wanasema ni mkali yupo top 5 ya greatest heavyweight boxers. Ni kweli ila hiyo ni kwakuwa amepelekwa pale na rekodi ambazo kazivuna kwa journeymen na has been.

Yaani watu wanajenga hoja ambazo tayari uzi umejibu. Kwa mwingine anayetaka kujenga hoja tafadhali aangalie kama uzi umeshajibu swala analotaka kuleta.

Update 2:

Mpaka saa hii hakuna ambaye ameweza kupangua hoja za huu uzi. Wengi wametukana au kusema tu walienjoy kumuangalia Tyson.

Bado hakuna aliyeijibu challenge hii - atajwe bondia ambaye alikuwa wa moto na Tyson wa moto kisha walipokutana Tyson akashinda.

Kuna mtu katoa hoja kua kupigwa kupo ndiyo maana Ali alipigwa pia. Nikajibu ni kweli ila mtaje bondia ambaye alimpiga Ali halafu walivyorudiana akampiga tena Ali. Kisha atajwe bondia aliyempiga Tyson na walivyorudiana Tyson akampiga huyo bondia.

Update 3:

Wazee siyo lazima uandike. Unabisha, ukiulizwa swali unasema hata hivyo hufuatilii ngumi. Ilikua ya nini kujileta hapa? Unauliza vitu ambavyo wenzako walishauliza au uzi una majibu, haina maana.

Unaniambia 'Hoja zako dhaifu' nakukubalia nakwambia sawa zilete 'Hoja imara' unadai ngumi hufuatilii au unaleta deals zishajibiwa. Surprisingly, hakuna anayekuja kujibu uzi.

Please kama huna cha kuandika, acha.

Update 4:

Uzi ushavamiwa huu, nilipigwa ban narudi nakuta urembo na quoted contents za baadhi ya member ambazo mimi sikuzifanya.

Am out.
.
images.jpeg


.
images (1).jpeg

Castr, Mkuu mchezo wa ngumi pesa zaidi, ya nini kila siku upigane na mtu huna uhakika, Wilder na Joshua wanakimbiana, Mayweather na Man Pac walikuwa wanakwepana kwepana.

Awe overrated ama lah!!
Kikubwa mie namuona bondia wa kiwango cha juu, kwa burudani alizokuwa ananipa ulingoni, jinsi anavyoshambulia, kujilinda, wepesi wake burudani ya boxing ilikiwa inapatikana kwake.

Mkuu nimesoma hoja na baadhi ya comments zako, na maoni yangu ni haya:

1. Kipindi cha kina Tyson, kilikuwa ni shifting era toka kwenye boxing kama burudani (more of an entertainment) kuja kwenye biashara (more of a business). Ukifatilia vizuri kwenye hizi zama mbili, utagundua kuwa kwny era ya kwanza boxing iliongozwa/endeshwa na passions,techniques na legacy (political/social) wakati kwenye era ya pili economic factors zilikuwa most influencial na hivyo kufifiza passions na techniques ambazo zilileta real fights in the boxing ring.

2. Kutokana na sababu hiyo hapo juu, Promoters na Promotion companies zilikuwa na sauti zaidi ya bondia na technical team yake. Hivyo issue kama kupigana na opponent gani, kwa wakati gani na kwa gharama gani vilikuwa chini ya wadhamini na si bondia.

3. Sababu ya 1 na ya 2, zikapelekea changes in boxers' mindset (Tyson in particular) from entertainment to business as well.

4. Mabondia wengine (pamoja na uliowaorodhesha) kwa zama hizo walipambana na target fights zao zilikuwa kupata match against Tyson ambaye alikuwa the most rated boxer hivyo ukipata pambano na Tyson hata ukipigwa unaweka mpunga mrefu mfukoni (hii ni domino effect ya sababu ya 1 hapo juu) kuwa 'pigana upate pesa'.

5. Ukiwa kwenye situation namba 4 hapo juu with plenty of options around, hata kama ni wewe utachagua pambano linaloguarantee ushindi(kwa nn uchanganye pilau yako na mlenda?). Hata CCM jana walichagua kupambana na TLP na UDP et all na sio CHADEMA.

5. Kuhusu issue ya hofu, hiyo ni kawaida unapokuwa ume-invest kwny jambo fulani lazima uwe na fear. Tyson na promoter wake walikuwa sahihi. Hii hata Mayweather Jr ameitumia sana ingawa tofauti na Tyson, Mayweather Jr alihakikisha anakuwa na muda mzuri wa kujiandaa na kumsoma mpinzani ambayeni tishio kabla ya kumvaa. Naye pia alikataa mapambano mengi ya wababe na alipigana when he felt the time was right for him.

6. Kwa kumtaza Tyson akipigana,nikiri kuwa the talent was there, he had the passion to fight and he was a natural warrior.

Angeweza kuwa-defeat hao uliowataja kama angetumia technique ya Mayweather, huyu jamaa ni genius wa mipango. Pamoja na watu kumtuhumu kubebwa baadhi ya mapambano kwny points, hakuna bondia aliyewahi kuondoa huo utata kwa kumpiga kwa KO/TKO, I think this was what Tyson lacked in his days.
 
Acha tu niheshimu maamuzi yako, hizo ndio fikra zako mkuu.
Tyson akishinda kapigana na mzee, underdog au Bingwa aliyecheza mapambano mengi kwa kipindi kifupi.

Akipigwa anabebwa, overrated n.k
Hujui unchokiandika juu ya Mike Iron ....wewe
Underdog ni timu/mtu ambae hategemewi kushinda katika hilo pambano.
Mf.real madrid na sheffield..sheffield ni underdog
hivi nini maana ya underdog?
Wachambuzi wetu hawa
Tukisema bondia ni mzuri ni kwakua amepambana na mabondia karibia wote wa kizazi chake na amewapiga.

Mfano Muhammad Ali, bondia aliyeogopwa mno Sonny Liston alikaa kwa Ali. Kama hujui ukali na ubabe wa Liston ni kwamba msemaji wa Patterson aliulizwa kama wataufuata mkanda kwa Liston akajibu "Huyo hatutaki hata kukutana naye, ikitokea akawa anakuja njia yetu na njia yenyewe tutabadilish

Holmes, Spinks na Berbick waliopigwa na Tyson ni kizazi cha Muhammad Ali, alipokutana na kizazi chake wakina Evander ndiyo vile vipigo tulivyoviona.

Kama kati yenu kuna anayeweza kutaja mabondia wakubwa watatu wa kizazi cha Tyson na aliwapiga awataje.
 
Mchezo wa ngumi ni kwa ajili ya kutafuta pesa sasa kama sponsor aliwekeza kwa Tyson ana haki ya kuangalia namna nzuri ya kurudisha pesa na alifanikiwa. Tusiwe kama wale wanahiphop njaa wa miaka Ile kule chuga kwamba mziki kwake ni bangi, ubabe na kuogopeka mtaani hata kama haumpi kipato. Kuna sababu gani kwenda kupigana wakati unajua utashindwa na thamani ya uwekezaji wako kwenye ndondi itashuka?
 
Mchezo wa ngumi ni kwa ajili ya kutafuta pesa sasa kama sponsor aliwekeza kwa Tyson ana haki ya kuangalia namna nzuri ya kurudisha pesa na alifanikiwa. Tusiwe kama wale wanahiphop njaa wa miaka Ile kule chuga kwamba mziki kwake ni bangi, ubabe na kuogopeka mtaani hata kama haumpi kipato. Kuna sababu gani kwenda kupigana wakati unajua utashindwa na thamani ya uwekezaji wako kwenye ndondi itashuka?
Naunga mkono maoni yako. Na kiukweli hii ni kwa mabondia wengi.
 
Castr, Mkuu mchezo wa ngumi pesa zaidi, ya nini kila siku upigane na mtu huna uhakika, Wilder na Joshua wanakimbiana, Mayweather na Man Pac walikuwa wanakwepana kwepana.

Awe overrated ama lah!!
Kikubwa mie namuona bondia wa kiwango cha juu, kwa burudani alizokuwa ananipa ulingoni, jinsi anavyoshambulia, kujilinda, wepesi wake burudani ya boxing ilikiwa inapatikana kwake.
 
Upo sahihi kabisa. Sahivi mapambano heavyweight ya kichovu kinoma. Watu wanaviziana viziana na kukumbatiana tu ,hakuna burudani yoyote, unaona tu pambano limeisha.

Iron alikua anafata kama nyuki. Hata kama kapigwa bado utaona raha ya pambano.
Mkuu mchezo wa ngumi pesa zaidi, ya nini kila siku upigane na mtu huna uhakika, wilder na joshua wanakimbiana, mayweathe na man pac walikuwa wanakwepana kwepana.

Awe overrated ama lah!!
Kikubwa mie namuona bondia wa kiwango cha juu, kwa burudani alizokuwa ananipa ulingoni, jinsi anavyoshambulia, kujilinda, wepesi wake burudani ya boxing ilikiwa inapatikana kwake.
 
Mike Tyson being "evandered" by Evander Hollyfield. Tatizo kubwa la Tyson ni kwamba alikuwa amezoea mapambano ya kuwapiga watu raundi ya 1 au ya 2, mwisho na hakuwa na pumzi ya kupigana zaidi ya raundi hizo. Hii ilimaanisha kuwa hakuwa na pumzi pamoja na uzoefu wa kupigana zaidi ya ya 1 au ya 2, sana sana ya tatu. Mimi siku ya pambano lao la kwanza nilipomuona Evander niliwaambia watu pale pale kuwa LEO TYSON ANAPIGWA.

Sababu kubwa iliyonifanya niseme hivyo ni kuwa figure ya Hollyfield ilikuwa inaonyesha ni mtu ambaye ni wa kupigwa kuanzia round ya 8 au zaidi na si vinginevyo, round ambazo Tyson hakuwa na uwezo nazo. Yeye alikuwa na uwezo wa raundi ya 1 na ya pili tu! Ni kweli kabisa Tyson alikuwa anakuwa over-rated, tena sana!
 
Mkuu mchezo wa ngumi pesa zaidi, ya nini kila siku upigane na mtu huna uhakika, wilder na joshua wanakimbiana, mayweathe na man pac walikuwa wanakwepana kwepana.

Awe overrated ama lah!!
Kikubwa mie namuona bondia wa kiwango cha juu, kwa burudani alizokuwa ananipa ulingoni, jinsi anavyoshambulia, kujilinda, wepesi wake burudani ya boxing ilikiwa inapatikana kwake.
Naona umesapoti nilichoandika.
 
Mkuu mchezo wa ngumi pesa zaidi, ya nini kila siku upigane na mtu huna uhakika, wilder na joshua wanakimbiana, mayweathe na man pac walikuwa wanakwepana kwepana.

Awe overrated ama lah!!
Kikubwa mie namuona bondia wa kiwango cha juu, kwa burudani alizokuwa ananipa ulingoni, jinsi anavyoshambulia, kujilinda, wepesi wake burudani ya boxing ilikiwa inapatikana kwake.
Bandiko limejaa chuki za wazi dhidi ya iron Mike Tyson.
Upo sahihi kabisa. Sahivi mapambano heavyweight ya kichovu kinoma. Watu wanaviziana viziana na kukumbatiana tu,hakuna burudani yoyote, unaona tu pambano limeisha.

Iron alikua anafata kama nyuki. Hata kama kapigwa bado utaona raha ya pambano.
Tyson supporters mnashindwa kujenga hoja badala yake mnatetea jinsi alivyokua muoga na mkimbia watu.

Sasa kama hoja yenu ni kwamba alikua anakimbia watu kwa ajili ya pesa mbona alipigwa na Douglas? Si angekua anawapiga hawa underdogs kirahisi?

Tukiwa hapohapo kwenye kukimbia watu, nitajieni bondia ambaye Wilder amewahi kumkimbia. Nitajieni bondia ambaye Foreman amewahi kumkimbia? Au Liston.
 
Back
Top Bottom