Pichani ni ndugu yetu/rafiki yetu anayefahamika kwa jina la TYSON NDUNGURU maarufu mtandaoni kama Tyzee SwahiliHood.
Ndugu yetu tokea alivyotoka nyumbani kwake siku ya ijumaa ya tarehe 26/05/2023 hajarudi wala kuonekana nyumbani kwake hadi dakika hii tunapoandika tangazo hili.
Muda wote huo juhudi za kumtafuta zimekua zikiendelea lakini bado hatujafanikiwa kupata taarifa yoyote inayomhusu mpaka sasa maana hata simu zake za mkononi zote hazipatikani.
Mkewe na familia yake inamtafuta. Wafanyakazi wenzake nao wanamtafuta na sisi marafiki zake tunamtafuta.
Tunaomba ushirikiano kwako wewe unayesoma ujumbe huu wa hali na mali ili tuweze kumpata mwenzetu akiwa salama. Taarifa zimeshatolewa kwenye mamlaka husika. Juhudi zimefanyika na zinaendelea kufanyika tumekuja kuomba juhudi za pamoja zaidi.
Tafadhali tusaidie kusambaza taarifa hizi. Ukipata taarifa yeyote tafadhal piga namba hizi.
Mawasiliano
0694644530
0625634902
0655642321