Wewe Paskali una shida sana, wewe unafikiri kuwa kila mtu anawaona ni mabeberu hao wanaotusaidia. Wewe baki na theory zako za kijinga jinga. Mambo ya mabeberu yamekwenda, yamekwisha na yameondoka na Magufuli.
Achana na mambo ya Magufuli, huyu ameshakufa siku nyingi, acha tujenge diplomasia na nchi za nje.
You are better than that Paskali.
Jingine ni ule waraka wa TLS kumtaka rais mpya Samia kulivunja Baraza la mawaziri la JK na kuunda lake la Awamu ya Sita. Rais Samia kaamua kuanza Awamu yake ya 6, na wachache wapya, na wengi ni mawaziri viporo wa Awamu ya Tano, kwa hoja kuwa kile kiapo chao kwa utii kwa JPM, kinahuishwiwa kwake, kwa hoja kuwa kiapo ni kwa Taasisi ya Urais wa JMT na sio kwa mtu. Kwa maoni yangu, kwa executive appointees, hata rais akibadilika, wao wanaendelea, lakini kwa political appointees wote ilibidi wale kiapo kimya kwa Rais Samia na sio kiapo cha utii kwa JPM, lakini kumtumikia Samia, ndio maana tukamshauri PM Majaliwa ange step down kumpa mama space to start a fresh, na kama bado anamuhitaji PM Majaliwa, ange m reappoint.
Paskali TLS na wewe mmeanza na mguu mbaya kwa kushindwa kutofautisha rais mteule (anayetokana na uchaguzi) na kaimu rais (anayetokana na sababu zingine isipikuwa uchaguzi)
SSH alikuwa kaimu rais mpaka alipoapa - anarithi urais anapoapa na toka japo anaendeleza pale mwendazake alipoishia.
maneno muhimu ni rais mteule na kaimu rais ukikosea hapo unapotea
Eti mabeberu
Acha ajitahidi labda Mama atamuwona ooops amesema ana pesa nyingiiiiiiii Hana shida ya kuwa RC ama DC hahahahhh labda anataka Ukurugenzi
Uandishi kama Uandishi tuendelee
Si hapo wala hapa panahitaji msaada wa P. au nani. Unajua hata kwenye mfumo wa chama kimoja bado kuna executive na political appointees. Wanajulikana kabisa. Wako tofauti sana. Kwenye mfumo wa vyama vingi ndio kabisa tofauti inakuwa kubwa zaidi. Mapenzi kwa chama kimojawapo inakaribia dhambi! Kama yapo ni kwa kificho sana. Na sio uchama katika kazi za umma wa vyama vingi.
Tumechizika. Kwetu ni fahari kuwa daktari wa ccm, polisi ccm, jaji ccm, jw ccm! Utaachaje wakati umeteuliwa kazi ya umma kwa kigezo cha kuwa mwanachama kindakindaki wa chama tawala? Vikao vya chama vinafanyika Ikulu! Kwa jeuri na kiburi tu. Acha aende tu. Tuache uchizi.
Hapa nachanganyikiwa kwasababu ijulikanavyo serikali haina chama, hivyo ningetegemea hao jamaa wote wakaape kwa bosi wao mpya, lakini hapa kwetu chama ndio serikali yenyewe na ndio maana wanafanyia vikao ikulu kama ulivyosema, anyway tuyaache tu.
Kama anajipendekeza kwa kuelimisha sioni tatizo hapo... Ww usiejipendekeza andika makala yako hapa kwa jukwaa tuone utofauti wa makala ya kujipendekeza na ambayo c ya kujipendekeza! Jf msingi wake ni jukwaa la great thinkers maana yake tunapaswa kubishana kwa hoja na sio vijembe! Tunakatisha watu tamaa ya kuleta habar na chambuzi zao huku ! Haya ni matokeo ya kuruhusu laymans kujiunga humu! Natamani kuwe na utaratibu wa kuremove wanaoatack individuals than the ideas!
Tulishasema humu adui wa mtanzania wa kwanza ni mtanzania hizo Habari hilo gazeti za Tanzania hupelekwa na watanzania na mmoja alidakwa Kabendera na The economist wakakiri akashughulikiwa barabara sasa huyu anayepeleka habari the Economist ni nani? Connect dots ila wazungu sio wajinga kama walivyomlipua Kabendera na huyu watamlipua
Najiuliza Why Mayala a quote gazeti lililopigwa marufuku na serikali ? copy katoa wapi wakati liko forbidden Tanzania? I smell a rotten rat somewhere
Kati ya eneo gumu sana kwenye tasnia ya habari ni eneo la uchambuzi wa habari, news analysis. Japo Tanzania tuna vyombo vingi vya habari, na waandishi wengi wa habari, ni vyombo vichache ndio vina waandishi wenye uwezo wa kufanya news analysis.
Kwenye print media wanajitahidi kwenye editorial, lakini kwenye electronics main stream media, ukiondoa TBC ile segment ya Shabani Kisu, na Jicho Letu Ndani ya Habari cha Star TV, chini ya Mkongwe Dotto Bulendu, naweza kusema, Tanzania hatuna any serious news analysis na news analysts.
Hivyo kufuatia uzoefu wangu kwenye media wa miaka 30, sasa baada ya kustaafu, naendelea kuwatumikia Watanzania kwa kujitolea, kila nipatapo muda, nitakuwa nawapatia kitu kinachoitwa trends & analysis za mambo mbalimbali kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Tukio la kifo cha ghafla cha Rais Magufuli, ni jambo ambalo halikuwahi kutokea, matokeo yake bado kuna trials na errors nyingi zitafanyika na serikali ya Samia hapa mwanzo mwanzo, ambazo nyingine zitakwenda kinyume cha katiba, lakini kwa vile tukio hilo ni kama force majeure kwenye mikataba, tutavumiliana tuu.
Mfano kwa mujibu wa katiba, baada ya Ripoti ya CAG kukabidhiwa kwa rais, within the first 7 days, ilipaswa itue mezani kwa Spika. This is the most important report, katiba haikuweka mazingira yoyote ya ripoti hii kushindwa kuwasilishwa mezani kwa Spika within the prescribed time frame. Ila kiutu uzima tuu, ripoti hii ilibidi iwasilishwe jana saa 3 asubuhi. Very unfortunately jana hiyo Waziri wa Fedha alikuwa hajaapishwa hivyo hawawezi kuipokea. Natumaini itatinga Bungeni kati ya Jumanne na Alhamisi Ijayo.
Jingine ni ule waraka wa TLS kumtaka rais mpya Samia kulivunja Baraza la mawaziri la JK na kuunda lake la Awamu ya Sita. Rais Samia kaamua kuanza Awamu yake ya 6, na wachache wapya, na wengi ni mawaziri viporo wa Awamu ya Tano, kwa hoja kuwa kile kiapo chao kwa utii kwa JPM, kinahuishwiwa kwake, kwa hoja kuwa kiapo ni kwa Taasisi ya Urais wa JMT na sio kwa mtu. Kwa maoni yangu, kwa executive appointees, hata rais akibadilika, wao wanaendelea, lakini kwa political appointees wote ilibidi wale kiapo kimya kwa Rais Samia na sio kiapo cha utii kwa JPM, lakini kumtumikia Samia, ndio maana tukamshauri PM Majaliwa ange step down kumpa mama space to start a fresh, na kama bado anamuhitaji PM Majaliwa, ange m reappoint.
Hayo tuyaache yangu ya leo ni haya..
Baada ya kuisoma ile makala ya Jarida la Mabeberu la The Economist na hoja zake kumhusu Presidaa Samia, Nimekuja na hoja 30 kwa waliyasema kuhusu Samia. Kati ya hoja hizo, kuna za hoja za kweli, ni muhimu kutozipuuzia, Luna hoja za uongo na uzushi ni za kuzipuuza, lakini mabeberu hawa walivyo na akili, kuna hoja ambazo ni za kutaka kumpangia kazi kiana, rais wetu ili afanye au atende kile mabeberu hawa wanacho kitaka.
Nilisisitiza humu, kwa vile JPM hakupenda kupangiwa, na hatukumpangia, vivyo hivyo kwa Samia, tusimpangie, lakini kumshauri na kumweleza jinsi mabeberu hawa wanavyo muona ni silaha muhimu sana ya kujiimarisha dhidi ya hila zozote za mabeberu hawa.
Ili uweze kulifaidi bandiko hili, anza na bandiko hili
Wanabodi, Kwa vile hili ndio bandiko langu la kwanza kwa mwaka huu, kwanza tutakiane heri ya mwaka mpya. Pili tupeana pole sana kwa msiba mkubwa wa kumpoteza JPM. Tatu, nitoe pongezi kwa President Samia kuwa rais wa JMT, kuongoza awamu ya Sita, hongera sana Mama Samia, umeanza vizuri kwa...
www.jamiiforums.com
Ukiona mabeberu wanaanza anza kuwasifu viongozi wazalendo wa bara la Afrika, ujue, wana lao jambo!.
Karibu kwenye hoja zangu... Hitimisho.
Swali ni Jee President Samia, atakubali kupangiwa kazi na mabeberu?.
Jibu ni only time will tell.
Bashiru, kama wanasiasa au wanadamu wengine, anayo nafasi ya kuibuka mbele kwa style nyingine. watu wa aina yake sio rahisi kusahaulika. Trust me he will bounce back even more strong than he was.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.