Kama mwendawazimu Trump na rafiki yake Netanyahu wamechafua na kuivuruga mashariki ya kati hadi kupelekea dunia nzima kuingia kwenye shida kubwa huku haya mataifa makubwa mawili yakishindwa kufanya chochote kuokoa jahazi sasa ukubwa wao una maana gani duniani?
Ni kweli wameshindwa kutimiza malengo yao Iran.
Malengo yalikuwa ni kuuvunja utawala wa Iran na kuondoa uwezo wake wa kuitishia Marekani na kuwa na uwezo wa kuunda makundi ya kigaidi kama Hamas na Hezbollah.
Ni wazi kuwa malengo hayo ya Marekani na mshirika wake mkuu Israeli hayajafikiwa kwani Iran bado yaudhibiti mfereji wa Harmuz na yapanga kuweka tozo ili ishirikiane na Oman kuusimamia mfereji huo.
Tatizo lililopo ni kwamba endapo malengo hayo hayajafikiwa hadi leo basi hitmisho ndo alolitoa raisi Trump jana kwamba Iran itaangamizwa hadi kurud enzi ya mawe (Stone Age).
Maana yake ni kwamba mpango wa Gaza ndo itabidi utumiwe na Marekani na Israeli kuivunjavunja Iran ibakie mji wa mawe.
Lakini hayo yote yakiendelea kufanywa na mataifa hayo jeuri na yenye nguvu kubwa Duniani, Umoja wa mataifa na hata nchi ya Hispania wamesema hii ni "Illegal War" na sheria za kimataofa zimevunjwa.
Hali ya uchumi Duniani imekuwa mbaya na si mafuta tu bali mbolea na bidhaa zingine muhimu kama nafaka zitapanda bei.
Sasa sidhani kama hapo pana suluhisho sahihi na lenye busara kutoka kwa raisi Trump na Benjamin Netanyahu zaidi ya kuitumbukiza Dunia katika shida ingine ya "The Great Depression".
Nnachotabiri ni kwamba kwa hasira Marekani watapiga mabomu mengi katika sehemu zilizo na vinu vya nyuklia ili kufukia kila kitu na baada ya hapo watajitangaza washindi na kwamba Iran imepigwa.
Lakini hiyo haitatosha kuzuia mashambulizi zaidi endapo Iran watajaribu kwenda sehemu za vinu hivyo kujaribu kuchimba kuitafuta ile Urani kwa sababu Marekani watakuwa wakipiga doria za Satelites kuona kinoendelea.