Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 199


Masiku kadhaa ulipita mjadala juu ya mchakato wa ajira ndani ya JWTZ,mchakato ambao umeonekana kugubikwa sana na walakini kutokana na ulivyoendesha.
Tangazo la ajira lilitolewa,ila baada ya watu kuomba hakukuwa na taarifa yeyote kuhusiana na waliochaguliwa.Zaidi tu tulipata taarifa kwamba waliochaguliwa walipigiwa simu za mkononi kujulishwa kuwa wamechaguliwa na nini cha kufanya.
Tulipohoji,wahafidhina wa mfumo wakatuambia kwamba JWTZ ni jeshi na lina siri,kwa hiyo mambo ya kutangaza waliochaguliwa kwenda kwenye usaili ni jambo nyeti ndio maana likafanywa kwa mfumo huo.
Jana jeshi la polisi wametoa tangazo na orodha ya watu waliochaguliwa kwenda kufanya mafunzo ya polisi moshi.
Ninachohoji mm binafsi ni kweli Jeshi la Polisi wao hawana siri??
Ni kweli jeshi la polisi wao ndio wana mambo ya kiraia na kuleta siasa ndani ya jeshi hilo la Polisi??
Naomba mazingatio!!