"ualimu ni kupoteza muda"

"ualimu ni kupoteza muda"

mi nliacha kwa sababu nliona napoteza muda na naelekea kuzeeka masikini. NI KWELI KABISA

pole sana,utajiri wa mtu hutokana na CREATIVITY ya mtu na siyo fani uliyosomea!wangapi ni madaktari lakin bado ni masikini?Tatizo macho yako mawili yalikodolea kamshahara ka mwisho wa mwezi.
 
Ualimu ni kazi kama kazi nyingine.
Mimi nilianza certificate nikapiga vizuri nikapangwa shule mazoezi, mwaka huu nimepiga paper la form six result imekuja vema niko chuo kikuu mwaka wa kwanza na M/Mungu akinijalia nina matumaini ya kufika mbali zaidi.

Ualimu mtamu na siuachi, ukifundisha watu wote kimya wanakusikiliza wewe tu unatema chakula cha ubongo.Mi naona fahari kuwapa watu maarifa ambayo hawakuwa nayo kabla sijawafundisha.

safi sanaaaaaaaaa saluti mkuu.
 
ualimu ni lazima kwa sababu ni lazima pia watu waelimishwe. huwezi kuwa na elimu bila walimu sawa na kuwa na magari bila madereva n.k. utajiri au umasikini si sabababu ya kuwepo au kutokuwepo kwa walimu. kama unaupenda ualimu kaa huko huupendi hujalazimishwa katafute hela kwingineko. muhimmu ni kutafuta njia ya kuweka heshima ya kazi hii tukufu.
 
kazi hiyo haina seminas, wala overtime. Huko ndugu yangu utakua umejiunga rasmi na chama cha watu maskini duniani. Mtaani jina lako litafutika na utaitwa ticha kwa kejeli tu. Yaani hutaweza hata kutoa michango ya harusi. Achiliambali kua shoe shiner ili kupata fedha za kujikimu zaidi.
 
kweli ni kupoteza muda., kulingana na system zilizopo sasa. Walimu wataendelea kubaki jinsi walivyo na akili zao... heshima yao na utajiri mkubwa walionao ni SHIKAMOO.
 
kweli ni kupoteza muda., kulingana na system zilizopo sasa. Walimu wataendelea kubaki jinsi walivyo na akili zao... heshima yao na utajiri mkubwa walionao ni SHIKAMOO.

Think before..! Aaarrrrrggggg
 
Saint Augustine said " You as a TEACHER don't expect wealth from TEACHING field" so changanua akili yako
 
Kazi Mbaya unayo, Subirini kuanzia 2016 zikitoka nafasi za Ualimu kama 10 kule Ukerewe halafu Usaili unasimamiwa na Tume ya Ajira mkianza kukimbizana na vibahasha Applicants 2,000 ndio mtaona umuhimu wake, Leo kwa kuwa mnapata Ajira Direct mnaleta Nyodo, Ukitaka kujua Thamani ya kazi yenu andika barua ya Resignation halafu kaa kijiweni Mwaka mmoja!
 
Ndio maana nasema follow excelence and succesfully will follow you.

Umekosea mdau kwenye sentensi yako. Sio successfully, neno sahihi ni success. Kiingereza kina wenyewe.
 
ualimu(primary&secondary) eti una uhusiano na heading hapo juu..............nionapo hizo thread/post huwa nakata tamaa........ni maneno ya rafiki yangu ambaye yupo third year DUCE pale.....eti wadau kuna ukweli wowote kuhusu hili? N.B.Toa Sababu ambazo ni reasoning
sababu ambazo reasoning ndo nini? kwa style hiyo hata ualimu wa chuo haukufai maana ..... duh...! sijui ndo hujui maana ya reason ...! au maana ya sababu...!
 
Ninaiheshimu fani ya ualimu!!!! Nitazidi kuiheshimu!!!!
Yesu aliitwa MWALIMU MWEMA!!
....Ole wake alaaniye walimu, hajui anamlaani nani.....
 
Kwa kawaida kila kiumbe Mwenyezi Mungu amekiandikia riziki yake,vile vile neema huwezi kuiona umuhimu wake mpaka itakapo ondoka!,swala la utajir ni mipangilio ya mtu mwenyewe.Mi ninaye Mwl wangu,anafundisha Primary lakin ana nyumba 3 za maana na amepangisha na ana mashamba ya michungwa na gari kifupi anawazidi hata hao wanaojiita wamesoma vyuo kwa kipato na amekataa kabisa kwenda kujiendeleza kwani amejitosheleza.Je huyu utasema anafanya kazi TRA?,huyo anayekwambia UALIMU ni kupoteza muda ya huko DUCE anafundishwa na MAZOMBI?,mwambie aende WIZARA akaone watu wanavyobembeleza kupata nafasi,hatuwezi dunia nzima kusoma DUCE.Mungu ameweka mgawanyo huu kila mtu asikufuru kuish bila kazi!,haya vip wale wanaoshinda mitaani kama we unasema kaul hyo?,kwel huyo anafaa kuwa hata Balozi wa mtaa?.Ahsante
 
pole sana,utajiri wa mtu hutokana na CREATIVITY ya mtu na siyo fani uliyosomea!wangapi ni madaktari lakin bado ni masikini?Tatizo macho yako mawili yalikodolea kamshahara ka mwisho wa mwezi.

uko sawa kabisa lakini si sahihi. Ila ingekuwa ni Serikali sikivu ingewathamini sana hawa watu. tatizo mazingira ya kazi ni magumu. ukifanya mishe zako kidogo tu inaonekana km uko bze na mambo yako. Niliacha kwa sababu ya fitina za kuanzia Mwl Mkuu hadi DEO. nikajikita 100% kwenye mambo yangu. saiv naenjoy hata kakitambi kametoka
KWELI HAKUNA MTU MWEMBAMBA NI SHIDA TU HakiyaMungu
 
uko sawa kabisa lakini si sahihi. Ila ingekuwa ni Serikali sikivu ingewathamini sana hawa watu. tatizo mazingira ya kazi ni magumu. ukifanya mishe zako kidogo tu inaonekana km uko bze na mambo yako. Niliacha kwa sababu ya fitina za kuanzia Mwl Mkuu hadi DEO. nikajikita 100% kwenye mambo yangu. saiv naenjoy hata kakitambi kametoka
KWELI HAKUNA MTU MWEMBAMBA NI SHIDA TU HakiyaMungu

Kama kuwa na kitambi cha safura baada ya kuacha ualimu ni sifa basi ni kweli kabisa ualimu ni kupoteza muda. Sifa za kijinga!
 
Kiwito sawa ila kiuchumi...ualimu lazima ufulie

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
dah namkumbuka mwalimu wangu wa primary dah zamb n huruma xna
 
Back
Top Bottom