"ualimu ni kupoteza muda"

"ualimu ni kupoteza muda"

Wakati nasoma elimu yangu ya juu nilifundishwa rational and reasonable thinking katika phillosoph, all i know ni kwamba elimu mchango wake ni mdogo sana ..kukupa maharifa,ila kufanikiwa kwako kunategemeana sana na akili yako binafsi (nature) uliyoumbwa nayo
 
Unajua ufinyu wa mawazo ndio unafanya watu kama wewe wakisikia neno Mwalimu wanajua ni primary na sekondari tu! Kumbuka hata lecturer na Proffesor ni Walimu na hutasikia malalamiko kutoka kwao.

Mwambie mwenzako akaze buti mafanikio hayaletwi na taarabu kama hizi.

hakika wewe wasema
 
Mimi nilikuwa mwalimu. Na nasema kwa dhati na mnielewe hii ni kazi nzuri sana kama mtu ana malengo hutakiwi kurithika kwa kazi ya aina yeyote ile.
Ukiwa mwalimu waweza kufanya biashara maana walimu wana muda mwingi, ktk mwaka wana miezi 3 ambayo hawaendi kazini yaani wapo likizo pindi shule zinapofungwa. Muda wa kukaa kazini ni mchache ukilinganisha na kazi nyingine hivyo mambo yako mengine yanaendelea kama una malengo.
Mwalimu ana nafasi kubwa ya kujiendeleza kielimu na akaweza badilisha kazi kama atadhani kuna umuhimu wa kufanya hivyo, maisha ya Tanzania kupata kazi ni ngumu sana lkn walimu wanaajili moja kwa moja serikalini hivyo ukishapata ajira yako na kama hupendi nenda kasomee kitu kingine unachokipenda ukiwa tayari mwajiliwa wa serikali na ukimaliza omba kubadilishiwa kada ya utumishi (categorization) kwa course mpya uliyosomea, kisheria unatakiwa kubadilishiwa.
Kuna watu wengi wajanja sasa wanafanya hivyo. Akishapata ualimu wake, kuna wanaoenda kusoma uasibu, social work, procurement, sheria, human resourse na kozi tofauti hadi udaktari na baada ya kuhitimu anaomba kubadilishiwa kada na kiuraini anapata ajira yake safi ya bila jasho ndani ya halmashauri yake tena bila interview. Na hapo sasa anaweza kupata uhamisho na kuhamia popote serikalini mf. Wizarani n.k
Amkeni wabongo acheni kudharau kazi. Kwa maisha ya leo Tz. Hakuna kazi bomba kama ualimu ni kutokujua tu.
Mke mwalimu ndo mke bora ndugu zangu. Anajua saikolojia ya mtoto hivyo atamlea mwanao ktk mazingira mazuri, atakuwa na muda mwingi wa kukaa na mwanao anajua tabia mbalimbali za watoto hivyo itakuwa rahisi kwake kumshape mwanao.
Oooh! Nimechoka kuandika, kwa ufupi kuna faida nyingi za kuwa mwalimu.
Ualimi ulivyoniweke nilivyosasa aise nauheshimu mnoooo. Kikubwa usiridhike, Ualimuuuu juuuuuuu!.

Kumbe wewe ni GREAT THINKER NAMNA HII?
 
kAZI YA UALIMU NI KAZI NZURI NA YA HESHIMA KAMA KAZI NYINGINE TATIZO NI SIASA ZA NCHI HII,NAKUSHAURI KWA HALI TULIYONAYO YA AJIRA SASA KAMA HAUTAKI KUTEMBEA NA BAHARA MPAKA KIATU KIISHE SORE SOMA UALIMU BAADA YA HAPO ZITAFUTE NDOTO ZAKO MAANA BADO UTAKUWA NA MUDA NA MKONO UMESHIKA KITU KURIKO KUITAFUTA 2 WAKATI HATA 1 HAUNA.
 
kazi hiyo haina seminas, wala overtime. Huko ndugu yangu utakua umejiunga rasmi na chama cha watu maskini duniani. Mtaani jina lako litafutika na utaitwa ticha kwa kejeli tu. Yaani hutaweza hat
a kutoa michango ya harusi. Achiliambali kua shoe shiner ili kupata fedha za kujikimu zaidi.

Nakubaliana na wewe ualimu ni sawa na chama cha masikini. Walimu wanaofanikiwa kiuchumi ni wale wenye juhudi binafsi(wakati huo wanakuwa watoro kazini), wanaobahatika kuwa maafisa elimu wilaya au mkoa, wakuu wa shule(kwa kuiba) na maafisa wa juu serikalini. Waliobaki ni masikini
 
Ndiyo hivyo,hakuna overtime kwenye ualimu,teaching allowance ziliondolewa kitambo,unakatwa CWT,PAYE,LAPF/PSPF n.k,National income,NHIF bado ulipe kodi ya nyumba na usafiri,si unajua shule nyingi siku hizi hazina nyumba za walimu!
Ili ufanikiwe lazima ukomae la sivyo utajaza madeni dukani!
 
Ualimu ni kazi kama kazi nyingine.
Mimi nilianza certificate nikapiga vizuri nikapangwa shule mazoezi, mwaka huu nimepiga paper la form six result imekuja vema niko chuo kikuu mwaka wa kwanza na M/Mungu akinijalia nina matumaini ya kufika mbali zaidi.

Ualimu mtamu na siuachi, ukifundisha watu wote kimya wanakusikiliza wewe tu unatema chakula cha ubongo.Mi naona fahari kuwapa watu maarifa ambayo hawakuwa nayo kabla sijawafundisha.

Excellent! We need people like you. It does not matter what you do in life, what matters is how you do it. Ni kweli utafika mbali.
 
kazi hiyo haina seminas, wala overtime. Huko ndugu yangu utakua umejiunga rasmi na chama cha watu maskini duniani. Mtaani jina lako litafutika na utaitwa ticha kwa kejeli tu. Yaani hutaweza hata kutoa michango ya harusi. Achiliambali kua shoe shiner ili kupata fedha za kujikimu zaidi.

Na watu wote wangukuwa na upeo kama wa kwako hata haya maandishi usingeweza kuyalambaza humu.
 
Nyakageni
kama unafundisha na wote wako kimya, hiyo ni ROTE LEARNING! Darasa lazima lichangamke. Participatory approach is the best

Mkuu, wanafunzi wa namna hii siyo "potential" kwa "participatory approach", aidha hawajui kusoma wala kuandika watazipataje nondo za kutumia kwenye "participation"?
 
Na watu wote wangukuwa na upeo kama wa kwako hata haya maandishi usingeweza kuyalambaza humu.

Kilio changu sio kua naidharau hiyo kazi. Sasa hivi kila mtoto afundishwe na bibi yake. Maswala ya mwalimu kumfundisha Mwanafunzi mpka mjukuu wa mwanafunzi yake, huku wakija na magari shuleni huku mwalimu huyo alie wafundisha hata shati la kubadili hana, ni kejeli kubwa kwa taaluma Hiyo.
 
kazi ya ualimu ni kazi nzuri sana kuanzia kozi za ualimu hadi kazi yenyewe...ukiwa mwalimu mwenye mipango mizuri utafanikiwa sana na kufanya mambo mengi katika jamii..cha muhimu ili usipoteze Muda kuwa na malengo na hakikisha yanafanikiwa pia penda unachokifanya na kuwa na changamko...tumia fursa zote unazokutanana
 
Back
Top Bottom