Mimi nilikuwa mwalimu. Na nasema kwa dhati na mnielewe hii ni kazi nzuri sana kama mtu ana malengo hutakiwi kurithika kwa kazi ya aina yeyote ile.
Ukiwa mwalimu waweza kufanya biashara maana walimu wana muda mwingi, ktk mwaka wana miezi 3 ambayo hawaendi kazini yaani wapo likizo pindi shule zinapofungwa. Muda wa kukaa kazini ni mchache ukilinganisha na kazi nyingine hivyo mambo yako mengine yanaendelea kama una malengo.
Mwalimu ana nafasi kubwa ya kujiendeleza kielimu na akaweza badilisha kazi kama atadhani kuna umuhimu wa kufanya hivyo, maisha ya Tanzania kupata kazi ni ngumu sana lkn walimu wanaajili moja kwa moja serikalini hivyo ukishapata ajira yako na kama hupendi nenda kasomee kitu kingine unachokipenda ukiwa tayari mwajiliwa wa serikali na ukimaliza omba kubadilishiwa kada ya utumishi (categorization) kwa course mpya uliyosomea, kisheria unatakiwa kubadilishiwa.
Kuna watu wengi wajanja sasa wanafanya hivyo. Akishapata ualimu wake, kuna wanaoenda kusoma uasibu, social work, procurement, sheria, human resourse na kozi tofauti hadi udaktari na baada ya kuhitimu anaomba kubadilishiwa kada na kiuraini anapata ajira yake safi ya bila jasho ndani ya halmashauri yake tena bila interview. Na hapo sasa anaweza kupata uhamisho na kuhamia popote serikalini mf. Wizarani n.k
Amkeni wabongo acheni kudharau kazi. Kwa maisha ya leo Tz. Hakuna kazi bomba kama ualimu ni kutokujua tu.
Mke mwalimu ndo mke bora ndugu zangu. Anajua saikolojia ya mtoto hivyo atamlea mwanao ktk mazingira mazuri, atakuwa na muda mwingi wa kukaa na mwanao anajua tabia mbalimbali za watoto hivyo itakuwa rahisi kwake kumshape mwanao.
Oooh! Nimechoka kuandika, kwa ufupi kuna faida nyingi za kuwa mwalimu.
Ualimi ulivyoniweke nilivyosasa aise nauheshimu mnoooo. Kikubwa usiridhike, Ualimuuuu juuuuuuu!.