mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Nilimaliza sheria 2012 , then nilisota mtaani hadi mwaka 2015 nilipopata ajira za ualimu wa serikali,sikuona umuhimu wa kwenda law school kwa sababu sikuwa na connection na watu mjini, nilibahatika kuajiriwa kwetu(wilaya niliyozaliwa), soon baada ya kuajiriwa , nilijibana sana nikanununua kiwanja na kujenga kinyumba kidogo chumba na sebule, huku nikijifunza kilimo na ufugaji ,
(Hapa nilikuwa natumia ardhi ya nyumbani tu ) baadaye niligundua kuwa na ardhi tu bila fedha kilimo hakiendi , thanks God mwaka juzi 2020 nilichukua mkopo milioni kumi na kuutupa wote kwenye pembejeo na kununua mifugo ( ngombe na nguruwe) , kiufupi salary yangu take home ni laki tatu tu, ila ninachokipata shambani ni zaidi ya hizo laki tatu kwa mwezi , sasa najenga, nina usafiri , namiliki viwanja kadhaa mjini, nimeongeza mashamba ya parachichi na kahawa na huku nikiendelea kulima viazi mviringo, nikienda bank wahudumu wa bank siku hizi wananifahamu na wale wakina dada wa bank wananichekea , kifupi nimeanza kupumzika na kuziona njia za hela kubwa , nimeandika haya kuwakumbusha walimu tu kuwa uwalimu sio umaskini Bali walimu wengi ni maskini, uwalimu kama kazi hauji kukupa hela zaidi ya kukopa na tumia vyema mikopo , salary ya mwalimu ni ndogo sana hivo hakuna means ya kupata hela kupitia salary,kopa ila ujue unakopea nini na una udhoefu wa kiasi gani na
Hicho kitu unachokopea, sijafanikiwa ila naziona hatua na viashiria vizuri na sijisifu sababu najua shit can happen