Uamuzi kuifungia CHADEMA kufanya siasa kutolewa Agosti 28

Uamuzi kuifungia CHADEMA kufanya siasa kutolewa Agosti 28

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252


Mahakama Kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam inatarajia kutoa uamuzi wa maombi madogo ya zuio la kufanya shughuli za kisiasa kwa CHADEMA Agosti 28, 2026 saa tisa alasiri.

Maombi hayo yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Said Issa Mohammed na Ahmed Rashid baada ya kesi waliyokuwa wameifungua awali, kutupiliwa mbali na Mahakama ya Rufani Mei 27, 2026.

Maombi hayo yametolewa na wadai hao katika kesi ya msingi ya mgawanyo wa rasilimali iliyofunguliwa na Said na mwenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho.

Uamuzi wa maombi hayo ulipangwa kutolewa Agosti 5, 2026 na Jaji Mbagwa baada ya kukamilika kwa majibizano ya hoja kwa mawakili wa pande zote, lakini Wakili anayeiwakilisha CHADEMA, Rugemeleza Nshala aliieleza mahakama kuwa hakuweza kukamilisha kuwasilisha majibu ya hoja za waleta maombi kutokana na kuwa na msiba wa kaka yake.

Soma: Kesi ya Mgawanyo wa Mali CHADEMA kuendelea Agosti 5, 2026
 
Kila step wanayo chukua wanaharibu zaidi
 
Back
Top Bottom