Uamuzi wa Bibi: Kazi au Familia Kwanza?

Uamuzi wa Bibi: Kazi au Familia Kwanza?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Kuna siku nilikaa na bibi yangu tukizungumza kuhusu maisha yake ya zamani.

Nilimuuliza swali ambalo lilinifanya nisikie simulizi ambayo hata baadhi ya wajukuu zake hawakuwa wamewahi kuisikia.

Niligundua kuwa zamani alikuwa amesomea na kufanya kazi ya uuguzi, lakini baadaye akaja kuwa mwalimu.

Nikamuuliza, "Bibi, ilikuwaje ukafanya kazi mbili tofauti?"

Simulizi yake ilianza Wakati huo alikuwa muuguzi mkoani Musoma, huku babu akiwa meneja wa kampuni kubwa mkoani Mwanza.

Siku moja bibi alipokea barua ya uhamisho wa kikazi kwenda Kisiwa cha Ukerewe. Uhamisho huo ulimaanisha kuishi mbali na mume na familia yake.

Alimweleza babu kuhusu taarifa hiyo.
Babu akamuuliza, "Kuna jambo lolote unalokosa kutoka kwangu au kwenye familia yetu?", Bibi akajibu, "Hapana."

Ndipo babu akamwambia, "Kama ni hivyo, acha kazi hiyo. Familia yetu ni muhimu kuliko nafasi hiyo ya kazi."

Haikuwa uamuzi mwepesi. Lakini bibi aliamua kuisikiliza familia kwanza. Akaandika barua ya kuacha kazi na kuwasilisha ofisini.

Baadaye alipata nafasi ya kuwa mwalimu katika shule iliyokuwa karibu na nyumbani, jambo lililomwezesha kuendelea kufanya kazi huku akiwa karibu na familia yake.

Alipomaliza simulizi lake akasema "Sio kwamba nilichukia taaluma yangu ya uuguzi, bali nilifanya uamuzi ambao wakati huo niliona ungeijenga familia yangu."
 
Hata bibi alikuaga binti...🤣
20260605_163436.jpg
 
Mkuu Bule, bless on ,asante sana kwa bandiko hili,very inspiring, Thanks
P
 
Back
Top Bottom