Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Mahakama kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, imeahirisha kutolewa kwa uamuzi wa maombi ya zuio katika kesi inayowahusisha Said Issa Mohamed na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mahakama imesema uamuzi huo umesogezwa mbele hadi tarehe 22 Oktoba 2026, saa 8 mchana, kutokana na Jaji aliyetarajiwa kutoa uamuzi huo kuwa na majukumu mengine nje ya kituo cha kazi.
Kesi hiyo ya Maombi Madogo Namba 14864 ya 2026, inatokana na mgogoro wa ndani ya CHADEMA ulioanza mwaka 2025, ambapo Said Issa Mohamed, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, pamoja na Ahmed Rashid Khamis na marehemu Maulidah Anna Komu, walifungua kesi dhidi ya viongozi wa Chama hicho wakiwadai ubaguzi wa usambazaji wa rasilimali za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Mwezi Aprili 2026, Mahakama ya Rufaa ilifuta uamuzi wa Mahakama Kuu uliokuwa umekataza shughuli za siasa za CHADEMA kwa siku 309, na kurudisha haki ya Chama hicho kuendelea na shughuli zake za kisiasa.
Mei 28, 2026, Mahakama Kuu iliitupa kesi hiyo kuu (Namba 8323 ya 2025) kutokana na kasoro za kisheria katika maandishi ya malalamiko, hasa kutotaja tarehe husika za madai.
Kufuatia hatua hiyo, Juni 6, 2026, CHADEMA ilimuondoa Said Issa Mohamed kutoka Chama hicho, ikidai alikiuka katiba na kanuni za chama kwa kuchukua hatua ya kisheria dhidi ya viongozi wake