init
Senior Member
- Mar 22, 2021
- 115
- 109
Awali ya yote nipende kuwasalimu nyote mtakao pata nafasi ya kupitia uzi huu.
Binafsi nimeshangazwa na uamuzi uliofanya na Benki ya NMB leo, kutoa Kompyuta mapaka yaani laptops kwa wamachinga. Nimepata maswali mengi sana, je wamepewa ili wauze ama ziwasaidie katika biashara zao?. Na kama ni kwaajili ya kazi pia nikajiuliza ikiwa Machinga ana mtaji chini ya laki nne, 400,000/= atawezaje kutumia kifaa chenye thamani ya zaidi ya laki sita kuendesha shughuli zake pasipo kuuza hicho kifaa? , na hata asipokiuza kitaongeza nini katika uchumi wa Wamachinga?.
Binafsi nilitegemea na ningependa kuona taasisi za kifedha kama Benki zikitizama njia bora za kuwafanya Wamachinga waweze kukopesheka kwani wengi kwa sasa wana mitaji midogo na pia hawana collateral securities za kuwawezesha kupata mikopo katika taasisi za kifedha. Matokeo yake wanategemea mikopo kutoka kwenye mashirika ya serikali na NGOs zinazotoa mikopo isiyo weza kukidhi mahitaji ya idadi iliyopo pia huja kwa misimu.
Pia Kwakuwapa mikopo hata NMB isingeli baki kihasara kwani ingenufaika na riba kwa kiasi chake na kuongeza watumiaji tofauti na donation zisizo na msingi.