Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,734
- 140,476
Ndugu yetu huyu amekuja na tamko la kumkosoa Gwajima juu ya masikitiko yake na ushauri alioutoa kwa serikali kuhusu utekaji unaoendelea.
Pasco ni mwanasheria, mtu ambaye anapaswa kuheshimu katiba na sheria. Kwa uanasheria wake tulitegemea amuunge mkono Gwajima kwa sababu licha tu ya kutumia haki ya kikatiba na kisheria kutoa maoni yake na kushauri serikali bali pia Gwajima ameonyesha masikitiko yake juu ya Haki ya Kuishi ambayo ni haki ya kikatiba na haki ya binadamu. Yaani mwanasheria anampinga mtu anayetetea haki ya kuishi?! Inasikitisha sana.
Pasco pia ni mwanahabari, mtu ambaye ulitegemea apaze sauti zetu na sauti ya Gwajima na kuhoji, lakini ndio kwaaanza.
Unajiuliza uanasheria wake una msaada gani kwa jamii?