SoC03 Uanzishwaji wa Viwanda vijijini Sera mojawapo ya kupunguza idadi ya watu na vijana wasio kuwa na Ajira katika Miji mikubwa

SoC03 Uanzishwaji wa Viwanda vijijini Sera mojawapo ya kupunguza idadi ya watu na vijana wasio kuwa na Ajira katika Miji mikubwa

Stories of Change - 2023 Competition

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Kwa nchi kama Tanzania ambayo ipo katika nchi zinazoendelea duniani inahitajika jitihada kubwa kutoka kwa viongozi wetu katika kujenga uchumi wa nchi yetu hasa kupitia katika nyanja kuu ya uchumi ambayo ni kilimo Imo na viwanda . Endapo sera hii ikitumika vyema Na Serikali basi manufaa yafuatayo yatapatikana.
Jakarta_slumhome_2.jpg

UANZISHWAJI WA VIWANDA VIJIJINI.
Kutokana na kuwa uzalishaji wa mazao mengi ya chakula na biashara yanatoka vijijini kuja mijini sababu ya viwanda na Soko kubwa kuwa mijini basi ni vyema sasa nguvu kubwa ikawekwa katika kuanzisha viwanda vijijini ambavyo ingeleta ama kuchochea mambo Makubwa ya kiuchumi. Serikali ingetilia mkazo katika uwekezaji wa Viwanda vikubwa na vidogo maeneo ya vijijini yafuatayo ni faida au athari chanya ambazo zingetokana na uwekezaji wa Viwanda maeneo ya vijijini.


MAPINDUZI YA KILIMO.
Endapo Serikali itatia mkazo katika kuwekeza na kuhamasisha uanzishwaji wa Viwanda vikubwa kwa vidogo huko maeneo ya vijijini basi idadi kubwa ya vijana na watu wazima wataweka nguvu zao kubwa katika kuwekeza kwenye kilimo, hii itahusisha vijana wasomi na wasio wasomi waliolundikana huko mijini bila kuwa na kazi kuingia kwenye kilimo kutokana na kuwa na uhakika wa soko eneo husika kwa sababu ya uwepo wa viwanda

Ikumbukwe kuwa katika nchi zinazoendelea kilimo ni. Moja ya sekta muhimu sana katika ukuaji wa uchumi na pia kilimo hicho hicho ndo chanzo muhimu cha ongezeko la viwanda katika nchi pamoja ongezeko la fedha za kigeni

IDADI YA WATU KUPUNGUA MIJINI /DEPOPULATION.

Endapo serikali itatia mkazo katika uanzishwaji wa Viwanda vijijini basi idadi kubwa ya vijana na watu wengi wasiokuwa katika ajira na sekta rasmi ya ajira waliopo mijini watahamia vijijini kutokana na kuwa kutakuwa na uhakika wa ajira viwandani na hivyo basi kutoona umuhimu wa kuendelea kukaa mijini ilhali ajira za uhakika zipo huko vijijini.

HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII
Fzh-RAxWIAAIqGz.jpeg

Picha kwa hisani ya mtandao.

Huduma muhimu za kijamii kama vile ujenzi wa Hospital, shule/vyuo., maji safi na salama, huduma za Internet, maduka makubwa hivyo basi tunaona umuhimu wa uanzishwaji wa Viwanda vijijini ni kiasi gani ingeleta tija katika mambo mbalimbali yanayogusa jamii yetu haswa upande wa vijijini ambapo huduma muhimu kama hizo hapo juu ni shida.

MIUNDOMBINU

Hii ni mojawapo ya mambo muhimu sana katika nchi yoyote duniani. Miundombinu inayozungumziwa hapa ni ujenzi wa barabara katika viwango vya Lami.
Bara bara ni kiungo muhimu sana kati ya vijijini na Mijini,
Sote tunajua umuhimu wa barabara katika uharakishaji wa usafiri wa bidhaa, mazao pamoja na watu kwa haraka.
Endapo basi viwanda wakaazishwa huko vijijini itarahisisha sana upatikanaji na ukarabati wa miundombinu iliyo bora kama vile barabara za Lami, reli na hata viwanja vya ndege.

NGUVU KAZI KURUDI VIJIJINI.

Sehemu nyingi za vijijini idadi kubwa ya watu waliopo ni wazee na watu wazima na watoto,hivyo basi endapo sera ya uanzishwaji wa Viwanda vijijini itaanzishwa basi idadi kubwa na nguvu kazi iliyokimbilia mijini itarudi yenyewe vijijini kutokana na kuwa na uhakika wa ajira mambo mengine muhimu ya kijamii kama vile huduma muhimu za Hospital, upatikanaji wa chakula na lishe bora.

Kabla ya kuhitimisha makala hii tunaona kabisa ni kwa jinsi gani endapo serikali itaanzisha sera ya uanzishwaji wa Viwanda vijijini tofauti na hali ilivyo sasa ambapo viwanda vingi vipo mijini kutakuwa na mgawanyo mzuri wa maendeleo pamoja na idadi ya watu
 
Upvote 2
Back
Top Bottom