Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishuhudia uapisho wa Mhe. Deogratius John Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Chamwino, Dodoma Agosti 29, 2026.
Hapa kuna nukuu ya kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan:
"Nitumie fursa hii, kukupa pole Mheshimiwa Ndejembi. Katika umri mdogo tumekutwisha jukumu kubwa na bila kukushauri. Pole sana."
"Lakini kipekee, nivishukuru sana vikao vya Chama Cha Mapinduzi. Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kupendekeza na kuliridhia jina la Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na hii ni baada ya kuzingatia sifa na vigezo alivyonavyo, ikiwa ni pamoja na umri wake ambao kwa kweli bado ni kijana mwenye nguvu, ari na kasi ya kujituma na kutekeleza shughuli za serikali."
"Lakini kwa kauli moja tuliamua, nafasi ile tuirudishe kwa vijana na tuendelee kulea. Imesomeka kwa kijana, tumerudisha kwa kijana. Sasa kijana tukuombe, ukakue—si kwa umri, lakini ukakue akili. Usiwe samaki. Mheshimiwa Karume mara moja alituambia vijana, alituasa: 'Msiwe kama samaki, kila mkikua akili inaharibika'."
"Kwa hiyo na wewe, wanetu, nenda kakue. Tumekupa majukumu makubwa, ni imani yangu utaweza. "Vilevile, nilishukuru sana Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Mheshimiwa Mussa Azan Zungu kwa kumpitisha na kumwidhinisha Mheshimiwa Makamu wa Rais, kwa kuzingatia yale yale, sifa za ndugu wetu Mheshimiwa Makamu wa Rais."
"Ninapohitimisha hotuba yangu, naomba kwa mara nyingine niwashukuru sana wageni waalikwa mlioitikia wito wetu wa kuja kujumuika nasi katika hafla hii muhimu. Tunawashukuru sana, karibuni Ikulu Chamwino."
"Pia nawashukuru sana mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa mliopo nasi kwa kuja kushuhudia tukio hili muhimu. Hii inaonyesha urafiki, undugu na ushirikiano mlionao kwa taifa letu."
"Laki pia ni kushuhudia mifumo yetu ya Kitanzania, uzuri wa katiba wetu kwamba tunaweza tukabadilisha nafasi kubwa bila kuwa na misukosuko, kwa amani na utulivu. Ahsanteni sana, karibuni sana."