Uasi mkubwa unakuja CCM

Uasi mkubwa unakuja CCM

Kinana mwenyewe si kasema hakuna mwenye hakimiliki ya mawazo huko CCM? au yeye Ndug. Bulembo alipitiwa usingizi kikaoni hakuipata hiyo kauli?
 
Ni uasi ambao haujapata kutokea ndani ya chama cha mapinduzi CCM.. Baada ya kukaa madarakani muda mrefu sana ni kama kuna kikundi ndani yake kimejikuta kinajiona wao ndio ELITES wa hii nchi, na lolote ama chochote kinachofanyika ni lazima kipate kibali chao.

Imefika mahali kikundi hicho kilichojitengenezea ukwasi na mtandao wa ajabu wenye ufadhili mkubwa wa matajiri waliojatajirikia CCM ambao si watanzania asilia kwa asilimia 100. Kina uwezo wa nani awe nani kwenye nafasi gani.

Ujio wa mwendazake ulifanikiwa kwa kiasi chake kuudhoofisha huu mtandao wa hiki kikundi lakini naye akanaza kuharibu kwa kuanza kutengeneza himaya nyingine mpya ya upande mmoja tena kwa ukatili mkubwa sana.

Hapa kitisho kilikuwa wazi ni vita kati ya himaya mpya ya mwendazake vs mtandao kongwe THE ELITES ... Halafu sasa hiki kirusi kipya cha visiwani chenye vinasaba vingi na The elites! Hili linakolezwa na fununu zisizothibitishwa kwamba Taifa la Tz liko chini ya watoto wa familia moja.. 'Baba mmoja'... Ni TUHUMA!

Yaliyotokea ya mhimili mwingine mpaka kupelekea kujiuzulu, kauli ya mkuu wa kaya kuhusiana na 2025, uteuzi wa baraza jipya la mawaziri na makatibu wakuu pamoja na wengine wote kuna tafsiri moja tuu... Uasi ujao na vita mpya kati ya sukuma gang, mtandao wa the elites , visiwani na bara na chawa wenye maslahi kwa kila upande..

Kila kundi liko chimbo likijiandaa kivyake... Ni mchezo wa kuwindana...uasi mkubwa waja...na ndio nafasi pekee ya walio nje ya mfumo ku take cover!
"Chawa" kizazi hatari kwenye mtazamo wa fikra huru na kujiamini. Chenye sifa ya uoga, uvivu na starehe.Neno uzalendo ni msamiati unaopotea katika jamii yetu sasa na punde utakuwa ni msamiati utakaohifadhiwa katika nyumba za kumbukumbu ya mambo ya kale.
 
CCM si moja. Kuna CCM-Mpina na CCM-January. Kuna CCM-Mwendazake na CCM-Samia. Kuna CCM-Asili na CCM-Yatima. Hizi CCM zote zinahitaji muafaka ili tupate CCM moja.
Team Mwenyekiti ndio team nguvu kwa wakati huo
 
Mi ntaunga mkono sukuma gang. Bora ujiunge na kundi shupavu lenye nia ovu kuliko kujiunga na kundi dhaifu lenye nia ovu.
Hakuna cha sukuma wala pwani, Katiba, Katiba, Katiba.
Kama kufaidika, tufaidike wote na kama kukosa, tukose wote! Kwa Haki!
 
Hakuna cha sukuma wala pwani, Katiba, Katiba, Katiba.
Kama kufaidika, tufaidike wote na kama kukosa, tukose wote! Kwa Haki!

duniani hakuna haki, haki iko mbinguni...
Hakuna siku wote tutafaida duniani, maana hakuna mfumo wa haki hiyo duniani..
 
Wewe hujaelewa,, wayahudi walipofika caanan walikuta wafilisti ndio watawala sa eneo lile ,, wayahudi wakaaanza kwanza kuishi hapo kama immigrants, na walikuwa chini ya utawala wa wafilisti,, mfalme saul(finctional character),amekuja kuanza kutawala miaka mingi baada ya waahudi kutoka misri,, hivyo mahakama ilikuwa ni ya wafilisti
Mwenzetu unasoma biblia gani
 
Hakuna cha sukuma wala pwani, Katiba, Katiba, Katiba.
Kama kufaidika, tufaidike wote na kama kukosa, tukose wote! Kwa Haki!
Neno haki litoe kwenye msamiati wako, HAKI haipo na haitakuja kuwepo, hata kama katika itakuwa nzuri kuliko kawaida.
 
CCM si moja. Kuna CCM-Mpina na CCM-January. Kuna CCM-Mwendazake na CCM-Samia. Kuna CCM-Asili na CCM-Yatima. Hizi CCM zote zinahitaji muafaka ili tupate CCM moja.
Huu mchanganyiko ndio kitanzi chao.
Wacha waparurane kwanza
 
JamiiForums330662192.jpg
 
Back
Top Bottom