Husika na kichwa cha habari hapo juu.
Ebana eee ubachelor noma Sana, kilichonikuta Leo siwezi kumaliza mwaka na ubachelor.
Leo nimeamka asubuhi Mimi ni mikazi tu, mikazi na Mimi, nimeamka mapema kuanza kufua nguo chafu za week mbili na nusu [emoji2], sijamaliza nikaanza kuandaa mboga ya mchana mara nikaandaa kifungua kinywa ile narudi kuendelea kufua mboga ya mchana imeiva kazi ya kuiunga [emoji87] mboga imeiva nikaandaa na msosi wa mchana huku kufua kunanisubiri [emoji80] narudi kumalizia kufua vyombo vya jana vyote vichafu kazi ikaanza ya kuviosha ile namaliza toi sio safi kabisa nikahamia toi kuweka mazingira sawia ahhh!
Nimemaliza usafi wa toi usafi wa geto ukanihusu ahhh hapa nipo hoii.
Ebana humu watoto wazuri wanaotaka kuolewa wapo eee, basi watoto wazuri tuonane DM asee tuyajenge mana nishaanza kuwa wife material...[emoji35]
Bango Limekaa Seriouly!