Ubachelor unaboa sanaaa!

Ubachelor unaboa sanaaa!

Tatizo umeweka makazi mengi halafu mengine yanatisha tisha kama nguo za wiki mbili sijui😀
Ungesema tu vitu simple kama nikiwa napika chai naungua vidole hivyo nahitaji usaidizi.Ungeshawaomba mods wafunge hili tangazo lako mapema.
 
20200714_193355.jpg
 
Vigezo must....

Miaka: 22-25 ikizidi sio mbaya ilimradi anishawishi Tu
Urefu: Kawaida
Rangi: Yoyote
Weka vigezo vyako na unayemuhitaji sasa

Ama unataka yoyote anayejua kufua na kupika mboga?
 
Kuna watu huwa unawalipa wanakusaidia kufanya usafi nyumbani kila weekend.
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu.

Ebana eee ubachelor noma Sana, kilichonikuta Leo siwezi kumaliza mwaka na ubachelor.

Leo nimeamka asubuhi Mimi ni mikazi tu, mikazi na Mimi, nimeamka mapema kuanza kufua nguo chafu za week mbili na nusu [emoji2], sijamaliza nikaanza kuandaa mboga ya mchana mara nikaandaa kifungua kinywa ile narudi kuendelea kufua mboga ya mchana imeiva kazi ya kuiunga [emoji87] mboga imeiva nikaandaa na msosi wa mchana huku kufua kunanisubiri [emoji80] narudi kumalizia kufua vyombo vya jana vyote vichafu kazi ikaanza ya kuviosha ile namaliza toi sio safi kabisa nikahamia toi kuweka mazingira sawia ahhh!

Nimemaliza usafi wa toi usafi wa geto ukanihusu ahhh hapa nipo hoii.

Ebana humu watoto wazuri wanaotaka kuolewa wapo eee, basi watoto wazuri tuonane DM asee tuyajenge mana nishaanza kuwa wife material...[emoji35]

Bango Limekaa Seriouly!
Unataka mke au dada wa kukusaidia usafi ?
 
House maid sina pesa za kumlipa, nataka mke wa kusaidiana nae chores zote....

Khaa!! Huna pesa ya kumlipa House Maid, kwahio unataka mtu wa kukufanyia kazi za ndani bure kwa kisingizio cha ndoa 😂😂
Wanawake tunafanya huo usafi kwa mapenzi yetu na huruma yetu sio kwamba ni SHERIA eti tunaolewa ili kua house girl wako Eboh!!!
 
Hapana sio nataka kuoa ili tu mwanamke aje kufanya usafi kwangu NO, tusaidiane shughuli zote za nyumbani baada nafikiri na kulea familia pia...
Khaa!! Huna pesa ya kumlipa House Maid, kwahio unataka mtu wa kukufanyia kazi za ndani bure kwa kisingizio cha ndoa [emoji23][emoji23]
Wanawake tunafanya huo usafi kwa mapenzi yetu na huruma yetu sio kwamba ni SHERIA eti tunaolewa ili kua house girl wako Eboh!!!
 
Njia rahisi ni kutafuta housegirl azoee hizo kazi, kabla ya kumlipa tangaza kumuoa, hatokudai malipo tena
 
Bachela sugu nipo

Hapa nimetoka kazini nimepika Wali mchafu na nyama za kurosti toka kwenye friji

Hii ni mahesabu ya siku 2 yaani kesho kazi yangu ni kupasha tu viporo vya mboga na huu wali mchafu

Sipendi kula viporo Ila Sina namna [emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom