Hivi karibuni kumeibuka Hoja nyingi juu ya uhalali wa Risiti za EFD, kwa sasa EFD ndio risiti maalumu ya Bidhaa kuuza na kununua popote pale Nchini. Lakini risiti hizi zina utata kutokana na uhalali wake.
View attachment 2779752
TRA wana tovuti ya kuhakiki risiti hizi za EFD ambayo ni
TRA RISITI lakini asilimia 80% ya risiti ukijaribu kuzi-hakiki hazionekani kwenye mfumo wa TRA. hasahasa risiti za Mabasi ya Mikoni, risiti za bidhaa madukani(baadhi) risiti za huduma mbalimbali.
Je, huu ni ubadhirifu au upigaji pesa ambazo hazipo kwenye rekodi ya Mapato katik ataifa letu, kama risiti unayo na haipo TRA inamaanisha haijakatwa VAT na hivyo taifa linaingia hasara. tunaomba
TRA Tanzania mtusaidie tupate uelewa zaidi kwenye issue hiii.
Mdau kama unarisiti ya EFD hapo ulipo angalie ilipoandikwa RECEIPT VERIFICATION CODE kisha ingia kwenye link hapo juu ya ku verify utupe screenshort inachokuambia
View attachment 2779753