Ubadhirifu katika Risiti za EFD za TRA

Hivi Kuna watu bado mna nguvu ya kufuatilia ulipaji kodi? Nchi hopeless hili unajishughulisha na nini mkuu? Wacha nao wale kwa urefu wa kamba yao!
Wajinga wajinga hawa
Unafatilia kodi kunehemesha familia za watuuu

Pyuuuuuu
 
Washaunda mfumo mwingine hiuko waupigaji.


Hivi kamishana wa TRA na Mwigulu na sakata lile la mfumo mwingine wa bandarini, bado wapo kazini tu?
 
Risiti yoyote ya TRA unayoi verify online lazima iwe na saa, dakika na sekunde. Hivi utaweka Kwa mfumo wa RisitiNumber_hhmmss. Mfano A284849D_170446 kumaanisha kua risiti yenye code A284849D iliyotolewa saa 11 jioni, dakika 04 na sekunde 46.

Kwenye picha uliyoweka hapa juu hujaweka hivyo vitu. Hapo hutopata verification kamwe, hata kama risiti ni halali.
 
Tutahangaika sna watanganyika kwa kichwa cha kizimkazi. YY hata huo muda hana. Na wapigaji wanajua kua kizimkazi anapenda kusafiri mnoooo ndio wanampangia masafari kila leo. Sina uwakika kama kuna mwezi bila safari ili kujua mambo ya nchi yake. Big NO
 

Mkuu, system ya TRA ni kimeo. Wiki mbili zilizopita nilitakiwa kuverify risit za mafuta. Nilihangaika sana kuingiza hizo details (risiti namba na muda) muda mrefu bila mafanikio. Kwa mbinde sana nikafanikiwa kuverify risiti 1 kati ya 3.
Nay hiyo nilivoirudia tena ikagoma.
TRA Tanzania mna kazi ya kufanya kwenye mfumo wenu wa kuverify
 
Mwigulu Nchemba Phd!!!
 

Attachments

  • 1CBBAC7C-4FAB-4A28-8BD3-F6B13010DA52.jpeg
    26.6 KB · Views: 1
Sio kila mauzo yanayofanywa yana VAT. VAT ni kwa wafanyabiashara wenye vigezo waliosajiliwa tu. Mtoa mada utakua umekaririshwa vibaya na wanasiasa wako kwamba kila risiti serikali inapiga hela
 
Ukiona walipa Kodi wanasubiri mtandao urudi ndio wafanikiwe kulipa kodi jua tatizo lipo kubwa sana....
 
Aliyekuwa hapendi kusafiri nje ya nchi aalikuwa anafuatilia hadi senti ya mwisho ndo maana alikuwa anatamba kwamba nchi hii ni tajiri. Sasa tuko na kundi linaloamini kwamba pesa ziko hukoooo kwa mjomba kumbe machawa wanamwingiza chaka namba moja.
 
Sio kila mauzo yanayofanywa yana VAT. VAT ni kwa wafanyabiashara wenye vigezo waliosajiliwa tu. Mtoa mada utakua umekaririshwa vibaya na wanasiasa wako kwamba kila risiti serikali inapiga hela
Wewe nawe huelewi. Usichangie topic iliyokuzidi uwezo. Kua na EFD na mambo ya VAT ni vitu viwili tofauti.

Mfano mafuta ya magari Petrol au Diesel haina VAT lakini Petrol Stations zinatoa EFD Receipt kwenye mauzo ya mafuta.

Nachomaanisha unaweza ukawa huna VAT kutokana na either volume ya sales zako au aina ya bidhaa unayouza haitozwi kodi lakini kutoa EFD receipt ni swala lingine kabisa nje ya mfumo wa VAT.
 
Mkuu kuna kitu kinaitwa Z-Report, ni kama processing ya data from your device kwenda TRA. Ukiwa na EFD ambayo muuzaji haja "run" Z-Report basi EFD yako itakua haisomi TRA.

Kingine ni network. Albert Einstein aliwahi kusema kua ukifanya jambo hilohilo kwa kilirudia rudia kila mara huku ukitegemea litakuja kutoa matokeo tofauti ni Ujinga. Lakini risiti za EFD zime prove wrong hii theory.

Siku mtandao ukikaa vibaya unaweza ukarudia hata mara 10 ndio inakuja kusoma.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…