Ubadhirifu, ufisadi, wizi, upigaji, ufisadi mkubwa nchini ni kutokana na mfumo CCM tuliojijengea wenyewe kwa miaka zaidi ya 60

Ubadhirifu, ufisadi, wizi, upigaji, ufisadi mkubwa nchini ni kutokana na mfumo CCM tuliojijengea wenyewe kwa miaka zaidi ya 60

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Watanzania wenzangu tufike mahali tufunguke macho yetu na tuchoke na huu upotevu wa matrilioni ya fedha zetu tulizochuma chini ya jua kali na baridi kali.

Kila siku tumekuwa tukisikia habari za ubadhirifu, tangu enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia, wimbo ni ule ule, uhujumu uchumi, wizi, ubadhirifu, ufisadi, upigaji na sasa sijui tuite jina gani. Haya yote ni matokeo ya kuwa mfumo ule ule mmoja (mfumo CCM) kwa miaka 60! Nchi zote majirani zetu walishaondokana na vyama vikongwe vya enzi ya akina Nyerere, sisi tunategemea nini kutoka CCM?1

Wazungu wanasema don't expect different results with the same procedures, kwamba USITEGEMEE MATOKEO TOFAUTI WAKATI UNAFUATA UTARATIBU ULE ULE!

Watanzania tusikubali kuwa washabiki wa hawa viongozi wanaojifanya kukasirika na kuishia kupiga kelele majukwaani bila kubadilisha chochote. Tuondokane na mfumo CCM la sivyo wachache wanaofaidi wataendelea kufaidi na kuneemeka huku wengine wakiteseka na kufa kwa kukosa mahitaji ya msingi. Tuamke!
 
Back
Top Bottom