Ubadhirifu wa mali ya umma moja ya nguzo muhimu kuimarisha CCM - dola katika ukandamizaji haki nchini

Ubadhirifu wa mali ya umma moja ya nguzo muhimu kuimarisha CCM - dola katika ukandamizaji haki nchini

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,745
Reaction score
1,171
TANU baba mzazi wa CCM aliyezaliwa 07/07/1954 na kuzikwa mwaka 05/02/1977 aliondoka na mambo yake yote.

Kuzaliwa kwa CCM kulichagizwa na sababu ya Muungano wa nchi mbili Tanganyika ambaye ni Marehemu na Zanzibar zote zikiwa nchi zenye mamlaka kamili.

Waasisi waliamini Muungano tu hautoshi,ili wawe na chama imara chenye nguvu kitakacho uunda serikali, hawana budi kuviunganisha vyama vya siasa vya TANU na ASP,na hapo ndipo mwanzo wa kuzaliwa kwa CCM baada ya miaka 13 ya Muungano na kuzika rasmi mfumo wa vyama vingi kabla ya kurudishwa tena mwaka 1992.

TANU

TANU ndiyo chama Cha ukombozi wa Tanganyika kilichopambana na vyama vingine mbalimbali kuleta uhuru,japo msingi na muktadha wa maudhui ya vyama vya ukombozi umefanikiwa kufunikwa na taswira ya TANU dhidi ya vyama vingine,vilivyokuwa kwenye mapambano ya uhuru.

Hivyo utaona sababu za Muungano ndizo zilizopelekea kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977,ikibeba maono ya TANU na ASP katika kuwatumikia wananchi.

Historia ya vyama hivi imejengwa kwa msingi mkubwa katika harakati za mapambano ya kutafuta haki kabla na baada ya uhuru kwa pande zote mbili za Muungano,vikibeba dhima nzito na kubwa ya kutafuta haki dhidi ya dhuluma ya Mkoloni na Sultani.

Vyama hivyo ndivyo vilivyosababisha kupatikana uhuru kwa nchi zote mbili ambazo ndiyo msingi wa mapambano ya haki dhidi ya batili.

ASP pia ni miongoni mwa vyama vya ukombozi katika harakati za kumng'oa Sultani na utawala wake. Na kwa kuwa malengo ya harakati zao yalifanana ukichangia na sababu za kisiasa kuimarisha Muungano ndipo mfumo rasmi uliposimikwa kwa kuzaliwa CCM iliyohodhi mamlaka ya kisiasa na kuuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CCM ilihodhi mamlaka ya kisiasa baada ya muunganiko uliouwa TANU na ASP kwa kuiweka kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 kabla ya mabadiliko ya mfumo wa vyama vya siasa 1992 wenye maudhui ya "CHAMA KUSHIKA HATAMU"

Pamoja na mazonge ya Muungano,Mwl Nyerere alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya Ina generate ubaya,na inapaswa iepukwe na kupingwa na Kila mpenda maendeleo,lakini alisahau ubaguzi huo waliuishi katika msingi wa kuviuwa vyama vingine vya siasa vilivyokuwa na mrengo wa tofauti na CCM yake ya Muungano.

Dhambi hii imeendelea kuitafutana nchi na laana ya kuiuwa Tanganyika itaendelea kuitafuna hii nchi iliyopotezwa kwa sababu ya kisiasa na kuigeuza Tanganyika kuwa shamba la bibi.

Wajenzi wanasema "ukikosea msingi wa nyumba,utajenga nyumba isiyo imara" Msingi wa Taifa hili umekosewa na kukosewa kwa msingi huo kama nilivyosema hapo juu kunaondoa kabisa uimara wa Tanganyika na umadhubuti wa Muungano wenyewe.

Mwl hakuwa malaika wala Mungu,alikosea na alisema tujisahihishe,lakini kwa kuwa msingi ulishakosewa hata nguzo za Azimio la Arusha kwa ajili ya kushikilia Tanzania mpya nao uliweza kuliwa na mchwa wakali wenye njaa ya madaraka.

Azimio la Arusha lilisimika misingi imara ya kuzuia UBADHIRIFU wa mali za umma. Nguzo zile za Azimio zilifanikiwa kuwa na nguvu kwa utashi wa mjenzi aliyekuwa akimiliki nchi kwa wakati huo,lakini haukujengewa msingi imara wa mamlaka ya kisheria na ndiyo maana kung'atuka kwa Nyerere kulisababisha mrithi wake kuling'atua vile vile Azimio la Arusha.

Hapo ndipo mwanzo wa madudu mapya ya ubadhilifu wa mali ya umma na ongezeko la ufisadi mkubwa serikali liliposhika hatamu.

Hivyo utaona kuwa kama ilivyofanyika kwa kupotezwa Tanganyika,dhambi Ile Ile ndiyo iliyoitafuna Azimio la Arusha na kuwaingiza mchwa wenye njaa Kali kujitwalia rasilimali za Taifa hili la Tanganyika iliyoko gizani.

Kuzaliwa kwa CCM kama chama kipya kilicho shindwa kuhimili malengo na dhamira ya waasisi wake,kumepelekea chama hiki kugeuzwa kokoro lililobeba Kila aina ya uchafu ulioshindikana.

Kikatoka katika falsafa ya ujamaa na kujitegemea na kuwa chama-dola kilichohodhi mamlaka ya wananchi na kuifutilia mbali misingi yote ya uadilifu kwa viongozi wa umma,na kugeuka kuwa kimbilio la watu wachafu na walafi wa mali za umma.

Ubadhilifu unashamiri Leo kwa uuzwaji wa RASILIMALI za mama Tanganyika umegubikwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya viongozi wa umma.

CCM ya Leo imekosa nguvu ya kuisimamia serikali kwa kuwa viongozi wa chama Chao wanapatikana kwa njia haramu za rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma,kwa kuwa waiba na kujimilikisha rasilimali za wananchi na kuzigeuza mtaji wa kupandia ngazi ya madaraka.

Mbunge anayetokea CCM anasimikwa kuwa mbunge kwa ushindani wa kifedha,anahonga wajumbe wote kwenye Kura za maoni,lakini anakingiwa kifua kwenye uchaguzi wa kiini macho wa vyama vingi na vyombo vya dola ili kulinda maslahi ya Watawala kwenye rasilimali za wananchi.

Hii ndiyo CCM ya Muungano iliyoasisiwa na Waasisi waadilifu. Lakini wameiacha ikiwa imekosa uadilifu na sasa inatamani damu za wananchi wake.

CCM hii ya Muungano imekosa uhalali wa kuwa chama Cha siasa,ambacho dhamira ilikuwa chama Cha wakulima na wafanyakazi.

Umewaacha wakulima,kwa kuwa watawala wake wa chama dola ndiyo wafanyabiashara wanao wanyonya wakulima. Karibu wabunge wake wote ni matajiri wakubwa wanaokwepa Kodi na wamiliki wa viwanda vinavyonunua mazao ya wakulima kwa bei wanayoitaka wao.

Mfumo wa serikali umehodhi haki halali za wafanyakazi za kupandishwa vyeo,kuongezeka kwa mishahara na kupata marupurupu kwa mujibu wa sheria za kazi,hali inayosababisha uadilifu na mmonyoko wa maadili kushuka kwa Kasi ya upepo wa kisulisuli.

Haya yote yanayofanyika chini ya utawala wa chama dola yamegeuzwa ndiyo nguzo imara ya kujisimika madarakani na kuendelea kukandamiza haki za wananchi.

Hata maamuzi yanayofanyika yanachagizwa na dhamira ya utashi wenye lengo la maslahi ya watu wachache,ndiyo maana neno "MFUMO" limebeba dhana nzito sana inayoheshimiwa na watawala wachache kwa maslahi binafsi,mathalani ujenzi wa karakana ya mwendokasi jangwani.

Wataalamu walishauri kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi,lakini majibu ya mahafadhina walioko kwenye mfumo walidai lazima ijengwe kwa kuwa mfumo ndiyo unataka hivyo,na kweli imejengwa itabolewa na itajengwa tena kwa kuwa miradi hii ni White Elephants.

Hayo yote tukidhamiria yataondoka japokuwa msingi ulikosewa wakati wa ujenzi wa Tanzania mpya.

Jawabu ni Katiba mpya ya wananchi itakayozika "mfumo" na kugatua mamlaka na madaraka ya wananchi dhidi ya chombo hiki ambacho ndiyo kinaimarisha nguzo hii izidi kuimarika,saa ya ukombozi ni sasa.
 
Back
Top Bottom