Ubadhirifu wa USD 400,000 za Sekta ya Afya: Philip Mpango alikuwa wapi mpaka aambiwe na Global Fund wenyewe?

Ubadhirifu wa USD 400,000 za Sekta ya Afya: Philip Mpango alikuwa wapi mpaka aambiwe na Global Fund wenyewe?

Hivi unajua maana ya neno " Kusaka hela " za uchaguzi ?
Kwa hiyo unataka kusema mzigo umechukuliwa na CCM kama walivyotaka kuchukua zile USD 500 Milion za elimu kutoka WB? Zitto Kabwe njoo huku!!
 
Aiseeee hela Mwana haramu hata tasisi kubwa takukuru na wapelelezi wanaunda tume hapana tuna pigwa blind mind
 
Ndugu acha kujitia aibu
Soma hii pia
28-01-2020
Nimesoma hiyo report na hicho ndicho ninachokizungumza, MFA ni recever na ku disburse kule zinalokwenda kutumiwa na end user na kusubiri report ya matumizi. Kunapotokea matatatizo katika utekelezaji, sio matatizo ya fund receiver but ni kule kwenye utekelezaji kwa recipients. Nakuuliza tena wewe baada ya kutoa fedha za matumizi ya nyumbani kwa mkeo, huwa unakwenda jikoni kuthibitisha vitu vimenunuliwa na ni kiasi gani?. Ni mpaka uletewe ripoti.

Global Fund wametoa fedha MOF, MOF ime zi disburse kule zinakotumika, ripoti imekuja zimepigwa, ni MOF?.

Waziri yuko right watafuatilia.

Kama watu ni wazito hivi kuelewa vitu vidogo hivi viko strait forward, mtaweza kweli kuelewa vitu complexe kama election rigging?. Ndio maana mgombea anapata wabunge 30 kwenye bunge la viti 230, halafu anawaambia nilishinda urais nikapokwa na mnaamini!.
P
 
Je kazi ya CAG ni nini?
CAG ni mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa fedha za serikali. Bajeti ikiishapitishwa na Bunge, CAG ndie anayeidhinisha zile votes kutoka mfuko mkuu wa hazina kwa ajili ya matumizi yaliyoidhinishwa na Bunge. Na baada ya matumizi CAG anapita kukagua kama zilitumiwa kama zilivyokusudiwa, na kutoa ile Ripoti ya CAG.

Mtoa fedha ni serikali kutoka mfuko mkuu hazina, na mtumiaji ni MDA's, CAG hawezi kutambua matumizi mabaya kama mtumiaji hajaonyesha.

Kuna mara kibao paper work iko clean, CAG anatoa unqualified report, lakini kiukweli tumepigwa!. Hii ni hela ya mzungu, yuko makini ndio maana kaona. Aliyepiga sio mpokeaji MOF bali mtumiaji!.
P
 
Leo pesa zikitolewa kwa ajili ya madawati, ukazitumia kuwekea milango ya madarasa tayari ni matumizi mabaya.
Hivyo yy kama Waziri ilipaswa kujua je pesa zimefanya kazi kusudiwa* ama LA na yy ni mmojawapo waliozipeleka katika matumizi yasiyo sahihi...
Sent using Jamii Forums mobile app
Taratibu za fedha za serikali zinafahamika, fedha zinapotolewa kwa malengo mahsus haswa hizi fedha za wafadhili zinakuwa "ring fenced" huwezi kuzibadilishia matumizi. Fedha unazoweza kuzibadili matumizi ni fedha za mfuko Mkuu wa hazina na kuna utaratibu wake.

Waziri wa Fedha, anapokea na kuzigawa kisha analetewa ripoti, mfadhili ndio amegundua madudu, waziri kasema hoja hizo watazifanyia kazi.
P
 
Pascal Mayalla,
Sentensi yako ya pili ya para ya kwanza imejibu na nainukuu

"Na baada ya matumizi CAG anapita kukagua kama zilitumiwa kama zilivyokusudiwa, na kutoa ile Ripoti ya CAG."

Mengine nimekuachia, hayana mashiko.
 
Ndiyo maana JPM hana mswalie mume na Watumishi wa Umma. Anatumbua tu
Inamsaidiaje akitumbua? Mtu alishapiga bilioni yake moja na mijengo na miradi yake mingine ya kumuingizia kipato ikisimamiwa na mkewe ati unamtumbua! Hapo humtumbui Bali umempa nafasi akazile pesa zake kwa nafasi tena bila amri na masharti!

Hiki ni kipindi Cha uchaguzi na watumishi walio wengi wameshaziona fursa kwenye siasa na wanajiandaa kuwekeza huko! Hata kina Ummy nao wanataka kurudi na ccm nao wanataka kuhonga ili washinde!
Pesa hizi huenda zipo hazina kwa ajili ya kuiwezesha ccm ishinde!

Haishangazi kwani ni kawaida yao kukwapua pesa za wahisani na kuwaacha walengwa ambao ni wapiga kura wakiteswa na maradhi!
 
Katika TAALUMA ya Audit, wizi (fraud) yoyote ambayo hufanywa kwa watendaji kushirikiana (collusion ) huchukua muda mrefu sana kugundulika na hasa kama kiongozi mkuu kama Waziri akishiriki na pia mthibiti na mkakuguzi mkuu wa Serikali naye akiwemo.

Wafadhili wanayajua haya kwa sababu hupata taarifa kutoka kwa watumiaji (user) amabao hukiri kuwa msaada haujawafikia.

Wafadhili wamekuwwa wanatumia zaidi NGO katika kuhakikisha misaada inawafikia walengwa kwa haraka na bila urasimu wowote.

Ndani ya Serikali kuna urasimu mkubwa na gharama nyingi katika kutekeleza na kutumia pesa za wafadhili. Pesa inaweza kutolewa lakini ikachukua muda wa miezi sita kabla ya kumfikia mlengwa.
Kama ilikuwa shilingi 1bilion basi itakayofika haitazi shs. milioni mia tatu. Milion mia saba itakuwa imepigwa kwenye mambo ya utawala na kuandaa makabrasha.

Pesa ikipita kwenye NGO humfikia mlengwa haraka na kwa kiasi kikubwa pamoja na kuwa hata huko kuna upigaji wa kutisha na hewa nyingi.
 
Pascal Mayalla,
Kaka Paskali;
Ndio sababu kila organization inakuwa na internal controls ambazo zipo designed kufichua abnormality yeyote bila mtu wa juu kabisa kulazimika kuchukua hatua yeyote. Na kwa bahati mbaya; anaetakiwa kuanzisha au kuhakikisha internal controls zinafanya kazi inavyotakiwa ni huyo huyo kiongozi wa juu kabisa.

Mpango hawezi kukwepa lawama.
 
Pascal don’t loose your head
Dr Mpango alijua mapema kuwa Watu wamechapa dola 400,000.00 au zimehamishiwa sehemu nyingine kwa matumizi .Ndio mana akatamka siku ya kupokea msaada. Alichotakiwa ni kutoa taarifa hatua gani zimechukuliwa. Ndio maaana wafadhili wana anza kuchomoa
Ndio maana kuna wanaoogopa zile za elimu zisije kipindi hiki cha uchaguzi.

Bwana mkubwa yule anavyoogopewa akisema "hizo rete huku" nani atabisha.
 
NJOLO,
Hii umenikumbusha kuna mtaa mmoja nilikuwa naishi, kuna shirika moja kubwa la misaada wana makao makuu ya ofisi zao huko..walitaka kuweka lami kipande cha Kilomita kama moja na nusu kutoka barabara kuu, serikali/manispaa wakataka wapewe wao pesa wafanye hiyo kazi, nadhani shirika wakadokezwa kwamba hiyo pesa ikiingia huko kuja kutoka ni baada ya miaka, na tena itakuwa imeshacharangwa.

Jamaa wameishia tu kujenga karavati/daraja kwenye moja ya sehemu iliyokuwa korofi, tena kwa mtindo huo huo wa wao kutoa pesa usimamizi ukafanywa na manispaa, ingawa nao waliweka Mtu wao akasimamia mpaka kazi ikaisha.

Mpaka wa leo hiyo Barabara ipo kiwango cha chagarawe.

Ila ni ishu kabla ya awamu hii.
 
black sniper,
Hayo nayo siyo matumizi yenye tija kuwekeza kwenye miundo mbinu bila kufanya upembuzi yakinifu.

Ethiopia ina madaraja na mabarabara bora na treni za SGR ĺakni watu wake ni maskini wa kunuka. Wengi tunawaona wakiwa wameshikwa au wamekufa kwenye malori wakiwa njiani kwenda South Africa.
 
Back
Top Bottom