Ubadhirifu wa USD 400,000 za Sekta ya Afya: Philip Mpango alikuwa wapi mpaka aambiwe na Global Fund wenyewe?

Ubadhirifu wa USD 400,000 za Sekta ya Afya: Philip Mpango alikuwa wapi mpaka aambiwe na Global Fund wenyewe?

Pascal Mayalla,
Pascal pls for heavens sake STOP defending magufuli and his gangsters, how can a minister not know what is taking place with such funds for sure? acha kutetea wala rushwa na wauaji wa ccm,hii ndio awamu ambayo imeiba hela nyingi kuliko awamu zote COMBINED.
 
Pascal pls for heavens sake STOP defending magufuli and his gangsters, hii ndio awamu ambayo imeiba hela nyingi kuliko awamu zote COMBINED
Mkuu The Seal, ukiondoa awamu ya Nyerere iliyotupatia uhuru, awamu zote zilizofuatia zilikuwa ni awamu za upigaji, Deep Green, Meremeta, Tan Gold, DCP, Radar, EPA, Escrow, etc,

lakini tangu Magufuli and his gangsters, as you call them, wameingia, hakuna scandal yoyote kubwa ya upigaji, ila pia ni katika miaka hii minne tuu ya kwanza, wameleta maendeleo makubwa kuliko awamu zote combined!, flyovers, Interchanges, mabarabara, madaraja, midege, meli, viwanja vya ndege hadi Chato, mahospitali, elimu bure, SGR, Stigler, etc.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni, Magufuli na kikosi chake wanapiga kazi.

P
 
Kama ambavyo donor atahitaji report ya matumizi ya mtonyo aliokupeni, au atafanya aina fulani ya auditing kuhakikisha kweli tonyo lililotolewa limefanya haswa kazi husika, ndivyo ambavyo wao kama wizara wanatakiwa kua wanafanya kaguzi za nmna hiyo, sio hadi kukumbushwa na donor. Siku wakisusa hawa kisa pesa zinatumika vibaya tutakua wageni wa nani sisi.
Naunga mkono hoja, kuna tatizo katika mifumo ya utekelezaji na usinamizi na it's not necessarily wizi but ni data entries kama tuu zile 1.5 Billions ambazo CAG hakuziona ziko wapi sio lazima kuwa zimepigwa.
P
 
Pascal Mayalla,
Pascal, point sio MOF imepiga, point ni kuwa haijui kuwa zimepigwa hadi donor anajua na minister hajui.. Mpaka afuatilie. Vipi mzee.

Hata mfano wako wa jikoni ni very irrelevant kwenye hii mada. Accountability ya donor funds au local finances sio sawa na matumizi ya jikoni hata siku moja.

Huwezi kumu audit wife hela ya chakula na wala hata katumia visivyo huwezi kumu adhibu. Hii ni nature ya mahusiano mliyonayo ya kuaminiana mke na mme. Donor au serikali inahoji hata senti 5 iliyotumika visivyo
 
Pascal Mayalla,
Aisee hoja ya kitoto kweli,hivi unapotska kutetea kwa Nini usitafakari ...hivi unajua kuwa GF wakitos hizo fedha Ni fedha za Serikali.

Msimamizi mkuu wa fedha za Serikali Ni Wizara ya ya Fedha,na Waziriwa Fedha Ni Dr MPANGO?! Ngosha ulikula maharage mabichi SI bure!
 
Mwaka wa uchaguzi huu, nyingine wanaiba hao hao wanaopewa kuzilinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ndio ukweli, mengine yote ugolo. Ni kweli serikali yetu inaiba pesa za wafadhili, kwa kuchepusha pesa kutoka kwenye matumizi waliyoelekeza wafadhili na kupelekwa kwingine ambako siasa ita-play role vizuri kama barabara, reli, Vivuko na Kununua wanasiasa.

Hakuna jibu zaidi ya kuwa pesa zimeibwa na hao hao waliokabidhiwa hata huko wizara ya afya hazikufika.

hII MIRADI YA UKOMA, KIFUA KIKUU, HIV na MAGONJWA YASIOAMBUKIZA. Imefadhiliwa sanaa, na kwa miaka mingi na kimekuwa kichaka cha serikali kuiba pesa za wafadhili.

Hilo linafahamika hata wizarani wanafahamu hilo.
 
Naunga mkono hoja, kuna tatizo katika mifumo ya utekelezaji na usinamizi na it's not necessarily wizi but ni data entries kama tuu zile 1.5 Billions ambazo CAG hakuziona ziko wapi sio lazima kuwa zimepigwa.
P
Aisee..
Naona ktk Uzi huu umekuja na mapambio tolea la 1980s.
 
Pascal Mayalla,
Ndugu Mayalla siku hizi sijui umekuwaje, kitu gani kimekuvuruga umepoteza sana weledi wako wa kuchanganua mambo..umekuwa bendera fuata upepo.

Huna tena uwezo wa koleo kuliita koleo bali koleo umeanza kuiita kijiko na uma umeanza kuuita vidole...sijajua ni kitu gani kimekufanya hivi, yaani huna haibu tena hata serikali ingekuwa imefanya makosa ya kawaida yanayo onekana wazi kwenye macho ya jamii wewe unajaribu kutengeneza hoja za kutetea jambo ambalo si sawa.

Kwa suala hili Dr Mpango unamuondoaje kwenye hatia? Haijalishi alijua mchezo uliofanyika au hakujua kabisa hawezi kukwepa lawama mambo mengine jamii inazidi kukushangaa kwani we ni mtu muhimi sana katika uga huu wa vijana wapenda taifa lao.

Hebu jaribu jaribu kuwa Paskal wa miaka ile. Sote serikali tunaipenda na kuthamini kazi zake lakini penye jema tutapongeza na penye baya tutakosoa.

Siwezi kusifia kila kitu na siwezi kukosoa kila kitu bali nitafuata mstari mnyoofu.
 
Pascal Mayalla,
Hauna tofauti na baba anayemwandikisha mwanae kuanza masomo yake, kisha akaacha majukumu yote kwa mtoto mwenyewe kiasi kwamba hata mtoto akiaga anaenda shule na asifike, hadi mwalimu aje nyumbani aseme mtoto hafiki shule kisha baba nae anamwambia mwalimu HILO NI JUKUMU LAKO, KAZI YANGU ILIKUWA KUMLETA SIKU YA UANDIKISHAJI TU. Umeelewa au niongeze sauti
 
Bajeti ya sekta ya Afya inafadhiliwa na na mataifa ya Ulaya na America kwa takriban 80%. Yaani kwa kila Shillingi inayotumika kutibu binadamu Tanzania, Senti 80 imaletwa na wafadhili kwenye dawa za ukimwi, malaria, Kifua Kikuu, Uzazi wa Mpango, Chanjo za watoto na magonjwa yaliyo sahauliwa.

Unashangaa nchi tegemezi kama hii, wafadhili hao hao wakiuliza kuhusu utawala bora tunawaita mabeberu.

Wale wanaotuletea condom bado wanaendelea kutuletea?
 
Pamoja na kujitapa wanapambana na ufisadi na majizi watumishi wanapiga dili tu kama kawa. Aibu mahakama ya mafisadi imelala usingizi wa pono.Yanayotendeka sawa na baba kuwa mkali home ili mke,watoto wasimuaibishe anapoiba mayai
 
 
 
Pamoja na kujitapa wanapambana na ufisadi na majizi watumishi wanapiga dili tu kama kawa.aibu mahakama ya mafisadi imelala usingizi wa pono.yanayotendeka sawa na baba kuwa mkali home ili mke,watoto wasimuaibishe anapoiba mayai

Mkuu ngoja awamu hii ihishe na CAG mpyaa aje utajua walifanya nini.
Maana kwa sasa hutojua kitu.
hii yenyewe tunajua maana wamekagua wenyewe wazungu, ila sijawahi kuisikia kwa CAG hii.
 
Back
Top Bottom